Mwanamke huhitaji pongezi anapofanya jambo zuri. Siku zote hutaka mwenzi wake ndiye awe wa kwanza kumpongeza kwa mafanikio yoyote anayoyapata. Inapotokea hapati kile anachokitarajia kutoka kwa mume/mchumba/mpenzi wake ni hapo ndipo maumivu mengi ya ndani kwa ndani humzingira.
Kila anayeumia, huhitaji faraja ili ajipoze. Sasa basi, wewe unapokaa mbali naye, ukaweka kinyongo kwa mafanikio yake, mwisho humsababisha amuone mwingine ambaye anaweza kusherehekea naye. Hicho ni kipindi ambacho nafasi yako ya kusalitiwa ni kubwa mno.
Amefaulu mtihani, amepata kazi au amepandishwa cheo kazini kwake, wewe ndiye unayeweza kukamilisha sherehe yake. Unapaswa kuhakikisha anakuona wewe ni sehemu ya mafanikio yake. Kitendo cha kumpongeza kwa maneno, kumkumbatia au kugonga glasi na kusherehekea pamoja, hufanya ajione mwenye furaha iliyotimia.
Kisaikolojia, japo wengi hulikataa hili kwa maneno lakini ndani yao huongozwa na mfumo jike. Kwamba hawawezi kwenda bila wazazi na wanapopata wapenzi, hujiona si wakamilifu wa kutenda mpaka wapewe mkono wa mwongozo kutoka kwa wenzi wao.
Ni athari hii ya kisaikolojia iliyopo ndani yao ndiyo huwafanya wajione wanyonge pale wanapowakosa wapenzi wao nyakati za kusherehekea mafanikio. Nilishaeleza kwamba mwanamke ni rahisi kuhamisha hisia na kusaliti, vilevile ni wepesi kujikosoa na kurejea kwa wenzi wao.
HISIA ZA KUFIKA MWISHO WA UHUSIANO
Kuna wakati, anaweza kuwaza kwamba uhusiano umefika mwisho. Jinsi mnavyowasiliana au mnavyoshirikiana katika mambo mbalimbali, picha anayoipata ndiyo humjengea taswira ya kuelekea ukomo wa mapenzi yenu. Hapo anaweza kujikuta anafikiria mtu mbadala.
Sasa basi, ni wajibu wako kuhakikisha unamfanya aone uhusiano wenu upo hai. Uhusika wako ndiyo unaompa tafsiri hasi au chanya. Je, unashirikiana naye vizuri? Mnawasiliana inavyotakiwa? Kama ndivyo, utakuwa umeweza kukamilisha nguvu ya upendo dhidi ya wasiwasi unaoweza kumwandama. Uhusiano wenu utakuwa imara.
Tafadhali sana, ni kosa kubwa sana kukaa mbali naye wakati anapokueleza wasiwasi wake kuhusu uhusiano wenu. Hawezi kuja malaika kutoka mbinguni ambaye anaweza kumhakikishia kwamba yupo kwenye uhusiano salama, kama siyo wewe mwenyewe. Hebu kaa naye karibu na umwondoe katika wasiwasi.
Pointi ya kuzingatia katika kipengele hiki ni kuwa mwanamke anapofikiria kuwa uhusiano upo ukingoni, kutokana na matendo yake mwenyewe au mwenzi wake, hapo ni sawa na njia panda au biashara iliyo sokoni, akitokea mnunuzi atambeba jumla. Aghalabu, akiwa katika mawazo haya, hujikuta ameangukia popote.
UHUSIANO UNAPOKUWA HAUMFURAHISHI
Asili ya mwanamke ni kupenda deko. Apate mwanaume ambaye atamfanya ajisikie au ajione sawa na malkia. Atakapokuwa naye, wazungumze na kupeana michapo sanjari na stori za kuchekesha. Hapo hujiona amefika. Mambo mengine ni ziada kwake.
Unapotaka kuushinda moyo wa mwenzi wako ili akupende kwa dhati, hakikisha anakufurahia na anafurahia mapenzi yako kwake kila siku.
Ukipotea njia, usimlaumu mtu, kwani atakaa shingo juu, kuangaza yule ambaye anaweza kumfurahisha. Hapo ni sawa na njiapanda ya kukusaliti.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment