Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia
Serikali imetangaza zabuni ya kusambaza madawati kwenye shule za msingi zilizoko katika mikoa 21 ya Tanzania Bara, yatakayotengenezwa kwa fedha zilizorejeshwa katika ufisadi wa ununuzi wa rada huku mikoa minne mipya ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe, ikiwa haitajwi kama mikoa kwenye mgawo huo.
Kwa mujibu wa tangazo lililochapishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwenye magazeti mbalimbali jana, mbali na kusambaza, zabuni hiyo inahusisha pia kutengeneza madawati hayo.
Hadi Aprili, mwaka huu, fedha hizo maarufu kama ‘chenji ya rada’ zilizorudishwa kwa Serikali ya Tanzania na Kampuni ya kutengeneza vifaa vya kivita ya BAE System ya nchini Uingereza, zilikuwa zimeongezeka kutoka Sh. bilioni 73.7 hadi Sh. bilioni 78.7.
Ongezeko la fedha hizo lilielezwa na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, bungeni, Aprili 10, mwaka huu. Tangazo hilo limetaja mikoa hiyo 21 na wilaya zake zote kuwa ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga, Lindi, Mtwara, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa na Kilimanjaro.
Mingine ni Ruvuma, Singida, Kagera, Kigoma, Mara, Mbeya, Mwanza, Rukwa, Shinyanga na Tabora.
Pauni milioni 29.275 (Sh. bilioni 66) zilirudishwa kwa Serikali ya Tanzania na kampuni hiyo, ambayo iliiuzia Tanzania rada hiyo ambayo baadaye ilibainika kuwa kiasi cha fedha zilizotolewa na serikali, ni kikubwa ukilinganisha na thamani halisi ya rada yenyewe.
Waziri Ghasia, aliliambia Bunge kuwa kiasi hicho sasa kimeongezeka kutokana na kupanda kwa thamani ya fedha na riba ya benki hadi kufikia kiasi hicho cha Sh. bilioni 78.7.
Alisema Sh. bilioni 59.1 zitatumika kununulia vitabu vya kiada na vitabu vya viongozi vya walimu.
Pia itatumika kununua mihutasari pamoja na miongozo ya mihutasari kwa ajili ya shule za msingi na asilimia 25, ambazo ni sawa na Sh. bilioni 19.7 zitatumika madawati katika shule za msingi.
Kuhusu ununuzi wa madawati, alisema mchakato umeanza na awali ilipendekezwa kuwa madawati yanunuliwe kwa ajili ya halmashauri tisa zenye upungufu mkubwa wa madawati, lakini baadaye ilibadilishwa kuwa kununulia madawati hayo yasambazwe katika halmashauri zote kwa usawa.
Alisema kamati endeshi ya fedha hizo za chenji ya rada, iliamua madawati yatakayonunuliwa yawe ya kukaliwa mwanafunzi mmoja.
Taasisi Uchunguzi wa Makosa ya Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza ilibaini kuwa baadhi ya maofisa wa serikali ya Tanzania na mawakala wa ununuzi walitumika kupandisha bei baada ya kushawishiwa na kampuni ya BAE.
Kufuatia hali hiyo, Kampuni ya BAE System ilitakiwa kuilipa Serikali ya Tanzania fedha hizo, ambazo zilitakiwa kuelekezwa katika sekta ya elimu.
Ununuzi wa rada hiyo uliofanyika mwaka 1999, ulizua mjadala mkali na kusababisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara kwa mara kuhoji gharama kubwa za ununuzi wake.
Kashfa hiyo pia iliwahi pia kumhusisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, kipindi hicho, baada ya kukutwa na dola za Marekani milioni moja (Sh. bilioni 1.2) katika akaunti yake ya benki iliyoko katika kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza.
SFO ilichunguza kujiridhisha kama fedha hizo za Chenge, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), zilikuwa na uhusiano na biashara hiyo ya rada.
Kutokana na kuhusishwa na kashfa hiyo, Chenge ambaye alikuwa Waziri wa Miundombinu, alilazimika kujiuzulu wadhifa huo, Aprili 20, 2008.
Februari 13, mwaka juzi, aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kuwa yeye ni mwadilifu, mtu safi, hakutenda kosa lolote katika kashfa ya rada.
Alisema uchunguzi uliofanywa na vyombo husika, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na SFO, ulibaini kuwa yeye ni mtu safi.
Ununuzi wa rada hiyo ulipingwa na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza, Clare Short, kwamba nchi maskini kama Tanzania haukupashwa kununua rada yenye gharama kubwa, akituhumu kuwako kwa rushwa katika ununuzi huo.
Hata hivyo, viongozi wa serikali ya Tanzania walipuuza ushauri huo.
BAE walikubali kulipa fedha hizo mahakamani baada ya kukiri kosa la kutokuweka rekodi zake za kiuhasibu sawasawa juu ya mgawo wa kamisheni iliyotolewa kwenye fedha hizo zikikadiriwa kuwa ni zaidi ya dola milioni 12, hivyo kukwepa uwezekano wa kutiwa hatiani kwa kosa la rushwa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment