Mwenyekiti wa jumuia ya watanzania wasabato walioko Marekani
iitwayo Tanzania Adventists in the United States (TAUS), Bwana Jeoffrey Ngullu,
amewatangazia watanzania wote kwamba mkutano mkuu wa kiroho kwa mwaka umekaribia.
Bwana Ngullu, aishie Philadephia, jimbo la Pennsylvania, amesema kufuatia
kufana kwa mkutano wa mwaka jana ulifanyika Washington D.C, uongozi wa TAUS
umeamua mkutano wa mwaka huu (TAUS Retreat 2013) ufanyike Houston TX. TAUS
inawaalika wote kujumuika, kufahamiana na kujifunza pamoja.
TAREHE ZA MKUTANO:
Julai 11-14, 2013
MAHALI- Oak SDA School,
11735 Grant Road, HOUSTON, TEXAS 77429 USA
MGENI RASMI:
Mchungaji Lucas Nzungu wa Arusha University, Tanzania
Gharama za mkutano ufikapo TX- ikiwemo chakula, usafiri na
hoteli (Holiday Inn)- ni $292.50 kwa mtu aliye tayari ku’share’ chumba (double
bed). Kwa wanaotaka chumba cha pekee jumla yao ni $465. Kuna wafadhili kadhaa
TX wanaoweza kusaidia gharama za malazi, usafiri na chakula ufikapo Houston.
Tafadhali wafahamishe mapema kama utahitaji ufadhili huo.
No comments:
Post a Comment