ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 13, 2013

MTUHUMIWA WA BOMU LA ARUSHA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO NA KUSOMEWA MASHITAKA 21

Mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 21 ya mauaji na kujaribu kuua.

Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki dunia katika tukio ambalo lililotokea Mei 5, mwaka huu.

Mawakili wa serikali, Haruna Matagane na Zachariah Elisaria wanadai Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Hata hivyo makosa mengine bado hayajatajwa..

Pia polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo baada ya uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na FBI na polisi wa kimataifa (Interpol), kubaini hawakuhusika kurusha bomu katika kanisa hilo. Differentsesources

No comments: