Akizungumza na Mwananchi jana Profesa J alisema hajajiunga na Chadema ili kugombea ubunge mwaka 2015, isipokuwa kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama hicho akiwa kama kijana.
“Kujiunga na siasa si dhambi na haina maana kwamba nina mpango wa kugombea jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sihitaji kugombea hata udiwani ila ni kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama ili kuyafikia malengo,” alisema.
Alisema yeye ni mfuasi wa Chadema tangu mwaka 2005 na amekuwa karibu na chama kwa nyakati nyingi lakini kwa sasa ameamua kuingia rasmi katika chama kama chachu katika kuongeza harakati kwa vijana.“Nimeingia ili nisaidie hiki chama kuikomboa Tanzania kwani kwa muda mrefu niliokaa katika chama hiki nimegundua kuwa wamedhamiria kumkomboa msanii, kijana wa kawaida na wakubwa kwa wadogo hivyo nadhani nipo sahihi katika uamuzi wangu.”
“Natambua mimi ni mwanamuziki, sawa nina mashabiki wengi lakini haina maana kwamba sina haki ya kuchagua chama ninachoona mimi kinanifaa, lakini siwezi kusita kufanya kazi sehemu yoyote au wakati wowote chama kikinitaka nifanye kwa wakati husika,” alisema Profesa J.
Profesa J juzi alijiunga rasmi na chama hicho baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema mjini Dodoma na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akiwa sambamba na msanii mwingine wa hiphop Kulwa Kinega maarufu kama K wa Mapacha ambaye alikabidhiwa kadi hiyo na Mbunge wa Ubungo John Mnyika.
Mwananchi
1 comment:
I respect Prof Jay's decision but, unless he also has some political ambitions, it's more likely that the political party he chose to join will gain at the expense of his own music career. Good luck to him, though!
Post a Comment