Saturday, May 25, 2013

RAMA MLA VICHWA VYA WATU NA MAMA YAKE WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Rama na mama yake, Khadija Ally wakipelekwa mahakamani chini ya ulinzi mkali baada ya kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Salome yaliyotokea Aprili 25, mwaka 2008.
Rama akihojiwa.
Mama mzazi wa mtoto Salome Yohana (3) akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya mwanaye.
Rama na mama yake wakiwa mahakamani.
Rama akiwa kalala kwenye majani.

KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  baada ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu) alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla Watu, ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Khadija Ally yeye ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome. 
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments: