TAWI LA CCM
WASHINGTON DC, MARYLAND&
VIRGINIA
SALAMU ZA POLE KWA WATANZANIA WENZETU- ARUSHA
MAY 5,2013
Chama cha Mapinduzi tawi la Washington DC, Maryland na
Virginia, tumesikitishwa na tukio la mlipuko siku ya Jumapili, Mei 5 2013 mjini
Arusha.
Chama cha Mapinduzi tawi la DMV tuna laani vikali
shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya
kwa Taifa letu la Tanzania. Tukio hilo la kusikitisha limepoteza mtanzania
mwenzetu na kusababisha wengine 40 kupata majeraha na maumivu makali.
Tunaamini serikali itafanya kazi yake ya kuwasaka
wahusika na wote walioshiriki kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Tunatoa rambi rambi kwa watanzania wenzetu
walioathirika kwa kuondokewa na wapendwa wao na wale wote waliopatwa na majeraha
katika tukio hilo. Mwenyezi mungu awape nafuu ili warejee kwenye shughuli zao
za kila siku.
Mungu ibariki Tanzania
UONGOZI WA TAWI LA CCM
WASHIGTON DC, MARYLAND NA VIRGINIA
MAREKANI
No comments:
Post a Comment