Ni kipindi kingine tena cha wanajumuiya ya Wanzania Houston kupiga kura na kuwachagua viongozi wa juu wa Jumuiya.
Uchaguzi huu unategemewa kuwa wa vishindo kutokana na watu wengi kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hasa nafasi ya Uenyekiti.
Pia baadhi ya wanajumuiya wamejitolea kuudhamini/kuufadhiri Uchaguzi huu katika masuala ya Ukumbi na Vinjwaji.
Nafasi zinazogombaniwa ni:
1. Mwenjekiti wa Jumuiya
2. Makamu mwenyekiti
3. Katibu wa Jumuiya
4. Mweka Hazina
5. Makamu mweka Hazina
Mikakati yote ya kuufanya Uchaguzi huu ufanikiwe ipo chini ya kamati ya Uchaguzi ambayo itatangaza majina ya wagombea na tarehe rasmi ya Uchaguzi. Kamati inawaomba wanajumuiya kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali na kufika kupiga kura pale siku itakapotangazwa.
Kamati ya Uchanguzi inaongozwa na wanajumuiya ambao baadhi yao ni waanzilishi wa Jumuiya hii na wengi wao ni wakongwe katika kuishi ndani ya jumuiya hii.
Majina ya Wanakamati ya Uchaguzi ni kama ifuatavyo:
1. Mrs. Anna Kavugha
2. Mr. Juma Maswanya
3. Mr. Stephen Maonyesho
4. Mr. Leonard Tenende
5. Ms. Honeymoon Aljabri
6. Ms. Kemi Kagirwa
Pia natangaza rasmi kwamba sitagombea tena au kutetea nafasi yangu ya uenyekiti kwa kipindi kijacho ili kutoa changamoto mpya kwa maendeleo ya Jumuiya. Nachukua nafasi hii kuwashukuru wanajumuiya ya Watanzania Houston kwa nafasi waliyotupa ya kuwatumikia, pia kuomba tusameane pale tulipokoseana. Nawashukuru viongozi wenzangu, viongozi wa wanajumuiya mbalimbali za Watanzania hapa US ambao mlishirikiana na uongozi wangu.
Pia naushukuru Ubalozi wa Wanzania washington.
Asanteni,
Novastus Simba, Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania Houston(THC).
No comments:
Post a Comment