Advertisements

Thursday, May 30, 2013

UPDATES ZA MSIBA WA NGWAIR NA MAENDELEO YA M2 THE P

Msanii M2 the P anaendelea vizuri, leo ameweza kuongea na ametolewa ICU kupelekwa wodini
-Mwili wa Albert Kenneth Mangwair unatarajiwa kuwasili jijini Dar Jumamosi Juni 1, 2013 na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
-Ngwair anatarajiwa kuagwa siku ya Jumapili katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar.
-Msanii Bushoke alaani watu wanaotoa taarifa zisizo sahii kuhusu sababu za kifo cha Ngwair. Baadhi ya wasanii ambao wamefika kumuona msanii M to the P ni Bushoke ambaye yeye yuko Afrika ya Kusini kwa wazazi wake pamoja na watanzania wengine wanaoishi huko wamesema hali yake inaendelea vizuri.

Rafiki wa karibu wa M to the P ambaye amesema yeye anaishi na M to the P na ni kama kaka yake kwani wanakaa nyumba moja, Bright Job amesema M to the P hatumii aina yoyote ya dawa za kulevya.. Bado watanzania wanataka kujua ni nini kilichotokea Afrika ya Kusinii kusababisha madhara makubwa kwa wasanii hao na habari masai.co nayo inatafuta chanzo cha madhara hayo..

#N.B kuna baadhi ya WaTz walioko south ndio wanaotuma taarifa zisizo za kweli REST IN PEACE#

No comments: