MJI MPYA WA KIGAMBONI ! SASA WANANCHI TUPO NJIA PANDA !
Kauli ya waziri wa Ardhi Bunge inawapa mashaka wakazi wa Kigamboni, Mpango wa siri ya kuwafukuza wenyeji wa Dar na kuwaweka wageni ndio
Agenda ya Wizara ya Ardhi,
Watanzania sasa tuna miaka 51 ya Uhuru,lakini tusipoangalia tutajikuta tunaingia katika migogoro ya Ardhi na uvunjivu wa amani utakaosababishwana Ardhi.
Ni mda mchache tu huko bungeni Dodoma waziri wa ardhi Mhe.Bi Anna Tibaijuka ameliezea bunge kuwa nyumba takribani elfu 30 zitajengwa na makampuni ya Dubai na Wachina, na wakazi wa Kigamboni watakuwa na hisa !
Kauli hiyo ya waziri Anna Tibaijuka inawatia wasi wasi wananchi na kujiuliza maswali mengi kama vile kuwa na hisa katika biashara hipi? nani mmiliki wa Ardhi? mbona wananchi wa Kigamboni hawajapewa taarifa yoyote! hakuna kikako chochote kile kilicho washirikisha wananchi na kujua hatima yao ! mbuge wa Kigamboni.
Mhe.Ndugulile naye kashangazwa na kauli hii ya Waziri....
TATIZO LA KUWAMILIKISHA ARDHI WAWEKEZAJI LITALETA UTATA.....
Wenyeji wa asili ya mikoa ya Dar-es-salaam na Pwani, wamejawa na unyongena kujiona wapo katika kilio cha kusaga meno kwa kuondolewa katika sehemu zao za asili na kutojua wapi watapelekwa, Tabia za baadhi ya wajanja kumiliki mashamba makubwa nalo limekuwa ugonjwa ulijitokeza katika kumiliki Ardhi.
UVUNJWAJI WA SHERIA ZA ARDHI
Migogoro mingi ya Ardhi inatokana na uvunjwaji wa sheria zilizopo na wizara inahusika kwa namna moja au ingine katika kuvunja sheria hizo kuna Ardhi zinazomilikiwa kimila,pia na manispaa, lakini Wizara ya ardhi imekuwa ikiwanyang'anya wazawa na kuwapa wawekezaji wa kigeni ardhi hizo bila ya kuwashirikisha wahusika,wananchi,serikali za mitaa na manispaa.
Ni juzi tu wakazi wa eneo la Tuangoma, njia panda ya Amani beach huko Kimbiji walijikuta wanabobolewa majumba na kulazimishwa kulipwa fidia la Sh.700,000 kwa heka ! na muwekezaji wa Kichina ndio kaanza
kazi ! Wanajeshi nao wanajaribu kuwatishia maisha wanye mashamba ili wapate mashamba ya bure. Serikali ilitupie jicho tatizo la Ardhi tusije tukawa watumwa katika nchi yetu

2 comments:
Ndugu wananchi mkae mkielewa kua tokea mwalimu jullias.k.nyerere afariki dunia. na mambo yote yamekufa. nchi imeuzwa.
KUSEMA KWELI MNATUWEKA NJIA PANDA, TATIZO LINAWEZEKANA WAKUU WAJADILI TUJUE TUPO WAPI, MAANA HATUJIELEWI!
Post a Comment