ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 6, 2013

Watani wetu wa Jadi Wachemsha katika World Rugby Sevens Glasgow

 Canada wakijaribu kuizibiti Kenya kufunga goli
kwa picha zaidi bofya read more

 Cheerleaders wakifanya manjonjo uwanjani
 Gemu limekubali
 Hatimaye Kenya yapiga bao Canada
 Kenya wakichuana na Samoa
 Sehemu wa mashabiki, wakati wa mapumziko
 Timu ya Rugby ya Kenya ikimenyana na Canada
 ilikua vuta nikuvute kati ya Kenya na Canada.
washabiki wakifurahia gemu
Timu ya  taifa ya mchezo wa Rugby nchini Kenya ilichemsha vibaya katika michuano ya Rugby sevens iliyofanyika katika uwanja wa Scotstoun, Glasgow siku ya jumamosi tarehe 4 Mei 2013. Walipoteza 17-14 Afrika ya Kusini katika mchezo wao wa kwanza na kufuatiwa  kipigo cha 26-0 kutoka kwa Samoa katika mchezo wa pili. Mchezo wa tatu walishindwa kwa 10- 21 kwa Canada ambayo ilihafifisha matumaini yao ya kufanya kufanya vizuri katika Kombe Kuu la robo fainali katika siku ya pili.

Kutokana na kuchemsha kwao ni dhahiri kocha mkuu Mike Friday aliwapa wakati mgumu wachezaji baada ya matokeo mabaya yaliogubikwa na makosa makubwa ambayo yangeweza kwa urahisi kuepukwa. Kenya walionekana kana kwamba  walipakwa grisi mikononi  kabla ya mchezo kuanza na kufanya kuwa vigumu kupata mpira na kupoteza ki rahisi.

Ingawaje  timu ya Kenya ilicheza  vizuri kwa kiasi fulani  katika mchezo wa kwanza, mchezo wao wa pili dhidi ya Samoa ulikuwa jicho-kidonda na kufanya mashabiki kuuma meno kutokana idadi ya makosa yaliyofanywa. Mchezo wao wa mwisho na Canada walijitahidi kurekebisha makosa yao ya awali na kutia bidii kukaba zaidi na kupunguza nafasi za kupokonywa mpira ingawaje waliishia kushindwa pia.

Kila wakati Kenya ilipokuwa na mpira, wao kuishia kufanya makosa, hivyo kupewa adhabu na penati. Mpaka sasa timu ya Kenya ina pointi 77 na kuwa na matumaini ya kufikia  pointi 100 katika mwisho wa mzunguko. Hiyo ina maana Kenya inatakiwa na kuja na pointi 23 kutoka kwa timu ya Scotland na Uingereza. Kama wanaweza kuchukua pointi nane kwa kushinda Glasgow kisha wao kubakia na pointi 15 kwa kushinda  Uingereza.

Afrika nzima inawakilishwa na Kenya pamoja na South Africa.

Asenteni
Urban Pulse Creative

No comments: