Juu na chini ni Aneth Bell ni mcheza sindimba maarufu toka kwenye group ya Bay Sindimba Sisters tokea jiji la Wajanja Oakland - California, ambaye atakua mmoja ya Watanzania atakayetumbuiza kwa kucheza ngoma ya asili ya Kimakonde maarufu kama Sindimba siku ya Tamsha la utamaduni wa Kiswahili na miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo itakayofanyika July 6, 2013. Tamasha hili litawajuisha Mhe. Rais Mustahafu Ali Hassan Mwinyi ambaye atakuwa mgeni rasmi, mabalozi mbalimbali wa nchi zinazoungumuza lugha ya kiswahili ukiwemo Ubalozi wetu wa kudumu umoja wa kimataifa New York, Wahadhiri wa kiswahili kutoka vyuo mbalimbali vya Kiswahili hapa Marekani wakiwemo VOA, wasanii Shilole, Masanja toka Tanzania na wasanii mbalimbali kutoka hapa Marekani, Wabunifu wa mitindo mbalimbali, Watoto wetu wa darasa la kiswahili DMV kutumbuiza kwa nyimbo mbalimbali za kiswahili. Tamasha hili halina kiingilio na litaanzaia saa 4 asubuhi kwa kuhudhuriwa na watu wote wakiwemo watoto ambao ndio walengwa wakuu kwa kutambua mchango wao wa kuendeleza lugha ya kiswahili na utamadunui wake kizazi hadi kizazi. Saa 11 jioni tutakua na mapumziko na tutakutana tena saa 1 jioni kwa chakula cha jioni na burudani ya muziki wa Disko mpaka saa 9 alfajiri. Kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 9 alfajiri ni kwa watu wazima tu na burudani zote zitafanyika kipindi cha kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni. Usiku itakua muziki wa disko tu hakutakua na onesho la aina yeyote.

1 comment:
Huyu dada nilishamuona ana kipaji sana. Sikujua kama kunawatanzania wanaweza kudumisha utamaduni wao kama hivi.
Big up bro Luke. Unaigusa sana jamii mungu aendeleze baraka zako na maisha tele. See you siku ya sherehe yako.
Post a Comment