ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 20, 2013

Balaa jipya Ligi Kuu England

Mabingwa watetezi Manchester United wataanza kutetea taji lao ugenini kwa kuifuata Swansea City ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu chini ya kocha mpya David Moyes huku Manuel Pellegrini ataiongoza Manchester City wakiwa nyumbani dhidi ya Newcastle United hapo Agosti 17.

Ratiba hiyo ya Ligi Kuu ya England iliyotangazwa jana pia itashudia Hull City iliyopanda daraja wakimkaribisha Jose Mourinho kwa mara ya nyingine Chelsea. Roberto Martinez, mni moja wa makocha watatu bora waliofanya uhamisho wao msimu uliopita ataiongoza Everton kuivaa Norwich City siku hiuyo.Huku timu iliyopanda daraja ya Cardiff City watakuiwa wageni wa West Ham United na Crystal Palace wataijaribu Tottenham Hotspur.

Msimu huu inatarajiwa kuwa na ushindani tofauti kwa sababu timu tatu zilizoshika nafasi tatu za juu msimu uliopita hivi sasa zipo chini ya makocha wapya ambao wanatarajiwa kuleta staili mpya ya uchezaji katika klabu zao.

Timu hizo tatu zilizoshika nafasi tatu za juu msimu uliopita katika Ligi Kuu ya England ni Manchester United, Manchester City na Chelsea, ambazpo zinatarajiwa kupata ushindani kutoka kwa klabu kama Tottenham na Arsenal.

Baada ya kocha Alex Ferguson kustaafu kuifundisha Manchester United, kocha mpya wa klabu hiyo David Moyes ataanza kibarua cha msimu mpya wa Ligi Kuu England wa 2013/14 kwa mechi ya ugenini dhidi ya Swansea.

Mechi tano za kwanza za Moyes akiwa anainoa Manchester United ni Agosti 17 dhidi ya Swansea (ugenini), Agosti 24 dhidi ya Chelsea (nyumbani), Agosti 31 dhidi ya Liverpool (ugenini), Septemba 14 dhidi ya Crystal Palace (nyumbani) na Septemba 21 dhidi ya Manchester City (ugenini).

Katika ratiba ya ligi hiyo iliyotangazwa jana inaonyesha kuwa Ligi Kuu ya England itaanza Agosti 17, ambapo kocha Jose Mourinho aliyerejea Chelsea ataanza kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Hull City.

Naye kocha mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini atakabiliana na Newcastle kwenye Uwanja wa Etihad. Timu zilizopandishwa daraja, Cardiff itasafiri kuifuata West Ham wakati Crystal Palace itaikaribisha Tottenham.

Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez ataiongoza timu yake kwenda kucheza na Norwich katika wikiendi ya ufunguzi wakati Liverpool itakuwa mwenyeji wa Stoke City.

Arsenal imepangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Aston Villa, wakati Sunderland itaikaribisha Fulham na Southampton itaifuata West Brom. Msimu huo utamalizika Mei 11 mwakani kwa Manchester United kuifuata Southampton, Chelsea itakuwa wageni wa Cardiff, Arsenal itakaribishwa na Norwich wakati Manchester City itakuwa mwenyeji wa West Ham.

Mechi za washindani wa jadi ni kama ifuatavyo: Arsenal vs Tottenham: Agosti 31 Tottenham vs Arsenal: Machi 15 Manchester City vs Manchester United: Sept 21 Everton vs Liverpool: Novemba 23 Sunderland vs Newcastle: Oktoba 26 Cardiff vs Swansea: Novemba 2.

No comments: