Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu maandamano ya kupeleka kilio cha wana Mtwara Ikulu,ambapo yameahirishwa kupisha ujio wa Rais wa Marekani Barrack Obama,kushoto ni Ofisa Chama hicho Mikidadi Ibrahimu.Picha na Michael Jamson
Dar es Salaaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimeahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu kwa sababu Rais Jakaya Kikwete, atakuwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Smart Partnership na kushughulikia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani.
Maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumfikishia Rais Kikwete ujumbe kuhusu vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.
Hata hivyo kuahirishwa kwa maandamano hayo kunakuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote na kwamba polisi watapambana na yeyote atakayakaidi amri hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema: “Tumepokea barua kutoka Ikulu, kutuomba tusitishe maandamano hayo kwa sababu Rais ambaye ndiye mpokeaji wa maandamano hayo atapokea wageni mbalimbali watakaoingia nchini,” alidai.
Mtatiro alisema barua hiyo ilieleza kuwa haitawezekana Rais kupokea maandamano ya CUF kwa kuwa atakuwa akipokea wageni mbalimbali.
“Sisi tulimwandikia Rais barua kuwa Juni 29 mwaka huu tutakuwa na maandamano ya kuelekea Ikulu,hatukujua kama kutakuwa na ugeni wa marais siku hiyo...tumeahirisha,”alisema.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment