Dar es Salaam. Manispaa ya Kinondoni inaendelea na utoaji wa elimu na maelekezo jinsi ya kuwapokea na kuwatendea wageni ambao wataambatana na Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi mwaka huu.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Sebastian Mhowera alisema kazi hiyo inaendelea vizuri na maofisa biashara wanatembelea hoteli moja hadi nyingine kutoa elimu na kuwahimiza wamiliki kuimarisha usalama.
Mhowera alisema wageni hao ambao wanatarajiwa kuanza kuwasili nchini Juni 28 mwaka huu, robo tatu wanatarajiwa kukaa hoteli zilizopo katika wilaya hiyo.
Hoteli nyingi zikiwa ni zile za ufukweni mwa bahari na maeneo mengine.
Alisema maeneo mengine yanafanyiwa maandalizi ya kawaida.
1 comment:
Hao maafisa biashara wananjua nini kuhusu customer service na usalama?
Post a Comment