ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 10, 2013

KESI YA LWAKATARE YAAHIRISHWA, KUSIKILIZWA KESHO ASUBUHI

Lwakatare akifunguliwa pingu.
Baadhi ya wanachadema waliofika mahakamani leo.
Lwakatare (kulia) na mtuhumiwa mwenzake Ludovick wakiwa mahakamani leo.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare, kwa mara nyingine ameshindwa kuwekewa dhamana leo katika kesi inayomkabili ya kujaribu kumwekea sumu Dennis Msaki iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuru jijini Dar es Salaam. Sababu za kuahirishwa kesi hiyo ni madai ya hakimu kuwa hakuweza kupata muda wa kupitia mafaili ya kesi hiyo maana alikuwa likizo. Lwakatare amerudishwa Segerea na kesi yake imetajwa kurudishwa mahakamani kesho asubuhi (Juni 11 mwaka huu). (picha kwa hisani ya GPL)

No comments: