ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 18, 2013

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA YANAYOENDELEA HAPA NCHINI GHANA

 Watanzania wakipunga mikono wakati wa ufunguzi wa mikutano ya watumishi wa umma barani Afrika hapa Nchini Ghana.
 Afisa Tawala Mwandamizi wa Wizara ya Fedha  Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Merkion Ndofi akimkaribisha mwananchi  wa Ghana katika  banda la Wizara ya Fedha
 Bw. William Ghump  amabaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mkurungezi wa Utawala na Utumishi Bw. Peter Mapigano wa Benki ya Posta Tanzania  pamoja  Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma  wakipanga mkakati wa uelimishaji umma katika banda la Wizara ya fedha.
 Mkuu wa Kitengo cha Mikopo kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha Bi. Christina Ngonyani akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa Ghana  juu ya umuhimu wa mikopo kwa Watumishi wa  Serikalini.
 Afisa Tawala Mwandamizi wa  Wizara ya Fedha, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Merkion  Ndofi akiwaeleza wanafunzi wa Ghana juu ya utendaji kazi wa Idara ya Utawala katika wizara ya Fedha Nchini Ghana.
 Mkuu wa Kitengo cha Mikopo ya Watumishi wa Umma wa Wizara ya Fedha Bi. Christina Ngonyani akiwa na Afisa Tawala Mwandamizi  Bw. Merkion  Ndofi , wakitoa ufafanuzi  kuhusu utendaji wa kazi za Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali  kwa wageni waliotembelea banda la Wizara ya fedha.
 Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi Bw. Peter Mapigano wa Benki ya Posta  Tanzania akitoa maelezo juu ya utendaji kazi na huduma mbalimbali ambazo Benki ya Posta inatoa kwa wananchi .
 Waziri wa Utumishi wa Umma ,Ofisi ya Rais Bi. Celina Kombani na Katibu Mkuu Bw. George Yambesi  walipotembelea banda la Wizara ya Fedha  hapa nchini Ghana.
Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi Ingiahedi Mduma akifafanua  jambo kwa  Bw. Eugene Koranteng Henaku wa Umoja wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Serilkali za Mitaa  Nchini Ghana.Picha zote na Scola Malinga- Hazina -Tanzania

No comments: