ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 28, 2013

MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAISI OBAMA WAKATI ALIPOTUA JIONI YA LEO KATIKA JIJI LA RETORIA


 Waandamaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika Jioni ya leo wakati Raisi Obama alipotua Katika Jiji Hilo leo Jioni Juni 28
 Waandamaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya Leo Juni 28
 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo Mapema leo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ametokea Nchini Senegali na Kutua Nchini Afrika Kusini huku Akihitisha Ziara Yake Nchini Tanzania wiki ijayo.
Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu amebeba bango leo Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.Picha Zote na REUTERS/AFP na LUKAZA

3 comments:

Anonymous said...

Pres. Obama ni rais wa wamarekani,waandamanaji walie na rais wao huku afrika kuleta maendeleo yao. Mko dunia ya tatu,Pres. Obama yuko dunia ya kwanza, unampinga nini? We need to respect and listen first b4 reacting with assumptions!!! Mgeni hajasema lililomleta, nyie mmeanza blah blah!! Waafrika tuache kufuata mkumbo wala hamjielewi mnaandamana kwa ajili gani.. Ulizeni wageni wengi waishio Amerika walivyomwombea apite urais na wanazidi kumuombea jinsi alivyopigania watoto wa wageni wapewe nafasi ya kusoma vyuo vikuu, we pray for this man. So please nyie mlioko mbali tafadhali all we need to say to America is Thank you for many things u have done to us.

Anonymous said...

Duu! Majanga!!!!!! Mweee.

Anonymous said...

hawa wa siasa kali wameivamia Africa kwa nguvu zote sasa hao sio raia wa South Africa hiyo ni fujo tu kama unataka kuandamana kwa nini usiandamane kwenu uarabuni mtuachie Africa yetu tumpokee kijana wetu Obama hawa waarabu amani kwao ni tusi kubwa sana ovyoo mnakaribishwa kuishi South Africa mnaleta na sera zenu za maugomvi mliyozoea kwenu