ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 1, 2013

NJOMBE WASEMA NO KWA UPINZANI


Zahanati ya Kiji cha Samaria ikiwa katika hatua nzuri za ujenzi, Zahanati hii inajengwa kwa fedha za Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ,pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Ndugu Nape Nnauye wakishirikiana na wananchi kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Samaria.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ndugu Esterina Kilasi . 

Kilimo Kwanza ndio njia pekee ya kutukomboa wakulima ,pichani Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa na wakulima ambao wapo chini ya shirika  la kilimo(NADO) katika kijiji cha Igwachanya,wilaya wa Wanging'ombe mkoani Njombe
Umati wa wakazi wa wilaya ya Wanging'ombe waliojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  katika ofisi za CCM wilaya hiyo ,pichani Katibu Mkuu wa CCM akiwasalimia wananchama na wapenzi wa CCM wa wilaya hiyo.
kwa picha zaidi bofya raed more
Katibu Mkuu wa CCM Taifa ,Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kuweka moja ya mizinga ya nyuki ya Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Wanging'ombe ,ambapo jumla ya mizinga 50 imewekwa na Katibu mkuu ameahidi kuongeza mizinga 25.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa ufugaji nyuki wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe.

Mradi wa ufugaji wa kisasa wa Nyuki ambao umezinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.


Katibu Mkuu wa CCM akiwasili Mlangali

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Wangamiko, Mlangali, mkoani Njombe.

Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Ndugu Nape Moses Nnauye akihutubia na wakazi wa Mlangali, wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.



Joseph Kihongo akionyesha kadi yake ya Chadema kwa wakazi wa Mlangali na kuikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kisha kukabidhiwa kadi ya CCM.

Umati wa wakazi wa Mlangali ukila kiapo cha kuwa wana CCM.

Katibu Mkuu wa CCM akiondoka Mlangali baada ya kufanya mkutano wa nguvu kwa wakazi wa kitongoji hicho.

Mapokezi ya aina yake kwa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika kata ya Luduga wilaya ya Wanging'ombe,  Mei 31 ,2013.


Oscar Mbafu (mwenye kofia) akisoma utenzi wake mahiri ambao ulizikonga nyoyo za wakazi wa Luduga, Utenzi wake huo pia utachapishwa kwenye gazeti la Uhuru  hivi karibuni.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Luduga ,wilaya ya Wanging'ombe,ambapo aliwasifia kwa kuwa wachapakazi na amewasisitiza hakuna miujiza katika suala la kuleta maendeleo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Jumuiya  ya Wazazi Chadema Wilaya ya wanging'ombe.
Picha na Adam H. Mzee

Wakazi wa Mkoa wa Njombe na Vitongoji vyake wamesema kwa sasa hakuna nafasi ya vyama vya upinzani katika mkoa wao, hayo yamesemwa jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Mlangali,wilaya mpya ya Wanging'ombe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka wananchi wa Njombe kutodanganyika na mwanasiasa yeyote atakayeahidi miujiza,"asije wanasiasa kutoka upinzani ama CCM atakayeahidi miujiza huyo atakuwa muongo, CCM inaahidi kile kinachoweza kutekelezeka na kama hakitowezekana sasa kitasema lini kitatekelezeka".
 Katibu Mkuu alifurahishwa kwa jinsi vijana wa Kitongoji hicho walivyo jasiri kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii, na kuamua kuwapa mtaji wa shillingi milioni 10 za kitanzania, mifuko 20 ya kukamilishia ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM Wangamiko na kuchangia mizinga 25 ya nyuki kwa Jumuiya ya Wazazi ya Wilaya ya Wanging'ombe.



No comments: