Advertisements

Monday, August 12, 2013

KWA MAOMBI YA WENGI, HII NDIYO RASIMU YA KATIBA MPYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika  Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.

KWA UFUPI 
Rasimu ya Katiba ina Ibara 240.
MISINGI:
uhuru, haki, udugu na amani

TUNU ZA TAIFA:
Utu,uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi uwajibikaji na lugha ya kiswahili,

-Mgombea Urais umri miaka 40,
-Kiwango cha kura za ushindi za urais ziwe zaidi ya asilimia 50,
-Matokeo ya urais kupingwa mahakamani (surpime cort).

MADARAKA YA RAIS:
-Kubaki kama yalivyo kwenye uteuzi wa viongoz wa ngaz za juu,
-Kushirikiana na taasisi nyingine,na kushauriwa na vyombo vya ulinzi na usalama kuteua nafasi nyingine.

BUNGE,
-Bunge kuwa na madaraka ya kumshitaki Rais,
-Ukomo wa ubunge ni vipindi vitatu,
-wananchi kuwa na uwezo kumuondoa mbunge,
-Spika asiwe mbunge wala kiongoz wa chama cha siasa,
TUME YA UCHAGUZI,
-Kuitwa Tume Huru ya uchaguzi,
-wajumbe kuomba nafasi na kufanyiwa usaili na Kamati ya uteuzi,
-M/kt wa kamati ya uteuzi ni Jaji Mkuu,

MAHAKAMA;
-Kuunda suprime court (itakayosikiliza kesi za matokeo ya Uchaguzi nafasi ya Urais).

MUUNGANO;
Serikali tatu,
Mambo ya muungano yamepungua kutoka 22 hadi 7,

BUNGE LA MUUNGANO;
Mawaziri wasizidi 15,
Wabunge 70!
Hamna mahakama ya kadhi.
DHANA YA RASIMU SIFURI YA MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU KATIBA MPYA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA SURA
Rasimu ina Sura 15, ibara 130 na nyongeza tatu.
Sura ya kwanza inahusu Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na watu wake. uk. 1-4
Sura ya pili inahusu maadili na misingi mikuu ya taifa. uk. 5-7
Sura ya tatu inahusu haki kuu za binadamu na wajibu muhimu uk.7-21
Sura ya nne inahusu serikali ya shirikisho uk. 22-42
Sura ya tano inahusu Bunge la shirikisho uk. 43-63
Sura ya Sita inahusu mahakama kuu ya shirikisho uk. 64-67
Sura ya Saba inahusu Mahakama ya Rufani ya Shirikisho uk. 68-73
Sura ya nane inahusu vyombo vya dola vya Tanganyika na Zanzibar uk. 74-78
Sura ya Tisa inahusu sekretarieti ya Maadili uk. 79-80
Sura ya kumi inahusu masharti kuhusu fedha za Shirikisho uk. 81-88
Sura ya ya Kumi na moja inahusu madaraka ya umm auk. 88
Sura ya kumi na mbili inahusu majeshi ya ulinzi uk. 89
Sura ya kumi na tatu inahusu mamlaka ya kutunga katiba uk. 90-92
Sura ya Kumi na nne inahusu Tuma mbalimbali za taifa uk. 92-99 na
Sura ya kumi na tano inahusu mengineyo uk. 99-105
NYONGEZA:
Rasimu sifuri ina nyongeza tatu kama ifuatavyo:
(i) Nyongeza kuhusu mambo ya shirikisho
(ii) Nyongeza kuhusu mambo yasiyo ya shirikisho na
(iii) Nyongeza kuhusu idadi ya wizara za shirikisho
1
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA SHIRIKISHO YA TANZANIA NA WATU WAKE
TANGAZO LA JAMHURI
1. (1) Nchi yetu ni Tanzania na ni jamhuri ya shirikisho iliyoundwa kutokana na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na itaitwa Jamhuri 

ya Shirikisho ya Tanzania;
(2) Eneo la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni eneo lote la Tanganyika na bahari yake pamoja na eneo lote la Zanzibar na bahari yake;
(3) Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni nchi moja yenye dola moja na vyombo mbalimbali vya utekelezaji wa mamlaka ya dola;
(4) Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana.
WATU WA TANZANIA
2.(1) Uraia wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni wa kuzaliwa kwa wenyeji wa nchi na kuasilishwa kwa wageni;
(2) Wananchi wa Tanzania wataitwa Watanzania na watakuwa na haki ya uraia kwa mujibu wa Katiba hii na sheria zitakazotungwa na Bunge la 

Shirikisho la Tanzania kwa ajili hiyo;
(3) Watu wote waliokuwa raia wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1964 ni raia wa Tanzania;
(4) Mtu yeyote ambaye amezaliwa baada ya tarehe 26 Aprili, 1964 hali wazazi wake wote wawili wakiwa raia wa Tanzania ni raia wa Tanzania;
(5) Mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania baada ya tarehe 26 Aprili, 1964 hali mmoja wa wazazi wake ni raia wa Tanzania ni raia wa Tanzania isipokuwa kama ataamua vinginevyo;
2
(6) Bunge laweza kutunga sheria itakayoweka masharti ya kuwawezesha watu wasiokuwa raia wa Tanzania kuwa raia kwa kuasilishwa.
DOLA YA KIDEMOKRASIA.
3.(1) Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na haki za binadamu zilizotamkwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na katika 

Mkataba wa Haki za Binadamu na za Watu wa Umoja wa Afrika zitakuwa na nguvu za kisheria na zitachukuliwa kama ni sehemu ya Katiba hii.
(2) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania halitatunga sheria inayofuta au kupunguza nguvu haki za binadamu zilizoainishwa katika 

katiba hii, na mahakama zitafafanua na kufasiri haki hizo kwa kuzipatia nguvu kadri inavyowezekana badala ya kinyume chake;
(3) Sheria yoyote inayobadili masharti yanayogusa haki za binadamu zilizoainishwa katika katiba hii itapitishwa kwa azimio la Bunge 

lililoungwa mkono na kura zisizopungua theluthi mbili ya wabunge wote na kwa hali yoyote ile Bunge halitatunga sheria inayofuta mfumo wa vyama vingi vya siasa.

MFUMO WA SHIRIKISHO
4.(1) Utawala wa dola utafuata mfumo wa shirikisho utakaozingatia mgawanyo wa mamlaka ya dola kati ya mihimili mitatu yenye mamlaka ya 
utendaji, utoaji haki, na kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma;
(2) Muhimili wenye mamlaka ya utendaji utakuwa na Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
(3) Muhimili wenye mamlaka ya utoaji haki utakuwa na Mahakama Kuu ya Shirikisho, Mahakama Kuu ya Tanganyika, Mahakama Kuu ya Zanzibar na 
Mahakama ya 3 Rufani ya Shirikisho na vyombo vingine vya utoaji haki vitakavyoundwa kwa mujibu wa Katiba hii na sheria za nchi;
(4) Muhimili wenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma utakuwa na Bunge la Shirikisho, Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;

MGAWANYO WA MADARAKA
5.(1) Pamoja na mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya dola, kutakuwa pia na mgawanyo wa madaraka na shughuli za dola kati ya mambo ya 

Shirikisho kwa upande mmoja, na mambo ya Tanganyika na mambo ya Zanzibar kwa upande wa pili kama ilivyoorodheshwa katika Nyongeza ya 

Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii;
(2) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti yaliyomo katika Katiba hii, 

Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
(3) Mihimili mitatu ya dola, yaani vyombo vya kutunga sheria, Mahakama na serikali vitafanya shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliana kila 

mmoja ukichunga na kudhibiti utendaji kazi wa mwingine;
(4) Katika kutekeleza majukumu yake kama ilivyoagizwa kwenye ibara ndogo ya kwanza ya ibara hii, vyombo vya dola vyenye mamlaka ya 

Shirikisho vitakuwa na kipaumbele cha kwanza kuliko vyombo vya dola vinavyotekeleza mamlaka ya Tanganyika na Zanzibar; ilmradi kwamba 

majukumu yaliyokabidhiwa kwa Tanganyika na Zanzibar hayatakabidhiwa na kutekelezwa na vyombo vya dola vya Shirikisho. Majukumu 

yaliyokabidhiwa kwa Shirikisho yanaweza kukabidhiwa kwa vyombo vya dola vyenye mamlaka vya Tanganyika na vya Zanzibar ili yatekelezwe na 

vyombo hivyo kwa niaba ya Shirikisho.
4
VYAMA VYA SIASA
6.(1) Wananchi wanao uhuru wa kuunda vyama vya siasa kwa mujibu wa Katiba hii na vitawajibika kuuwezesha umma kujenga hoja, kauli na 

ushiriki katika uendeshaji wa dola kwa njia za kidemokrasia;
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa Tanzania yatafanywa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria 

zilizotungwa na Bunge la Shirikisho la Tanzania kwa ajili ya hiyo;
(3) Bunge halitaweka masharti yanayokera au kukwamisha uanzishaji wa vyama vya siasa ama masharti ya uandikishaji na uendeshaji wa vyama 

vya siasa yanayokinzana, kuvunja masharti au haki nyingine zilizowekwa na Katiba hii.
SURA YA PILI
MAADILI NA MISINGI MIKUU YA TAIFA 

MAADILI
7. Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni nchi inayoongozwa na viongozi wenye kuamini na kufuata maadili yafuatayo:-
(a)Kuwa uongozi ni dhamana na utatumika kwa ajili ya maslahi ya Taifa na ya wananchi wote kwa ujumla na kamwe hautatumika kwa maslahi 

binafsi, ubaguzi, upendeleo au kwa ajili ya kujilimbikizia mali;
(b)Kuwa mali na rasilimali za umma zitatumiwa na kulindwa kwa maslahi ya Taifa na kamwe viongozi wa umma hawatatumia nafasi na mamlaka 
waliyokabidhiwa kutwaa, kuiba, kufuja au kujibinafsishia mali na rasilimali za umma;
(c) Kuwa rushwa na ufisadi ni maangamizi ya Taifa, hivyo viongozi hawatashiriki katika rushwa au ufisadi;
(d)Viongozi hawatafanya mambo yanayoleta mgongano wa maslahi kati ya maslahi yao binafsi na maslahi ya taifa;
5
(e) Viongozi wa umma hawatafanya biashara, kuajiriwa au kuifanyia kazi taasisi yoyote binafsi kwa ajili ya kujinufaisha binafsi.
MISINGI
8. Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia, haki na usawa, hivyo Taifa litaongozwa na kuishi kulingana 

na misingi mikuu ifuatayo:-
(a)Kwamba chanzo cha mamlaka ya dola ni wananchi kwa hivyo mamlaka za dola zitapata uhalali wake kutokana na ridhaa ya wananchi na 

serikali zote tatu na mabunge yote matatu yatawajibika kwa wananchi;
(b)Kwamba ufisadi, ujinga, maradhi na umaskini ni maadui wa Taifa kwa hivyo lengo kuu la sera, sheria na serikali zote tatu na juhudi za 

wananchi wote ni kuwaangamiza maadui hawa;
(c) Kwamba wananchi wanayo haki ya kushiriki katika shughuli za mamlaka za dola kwa mujibu wa Katiba hii;
(d)Kwamba Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni nchi moja na wananchi wake wote ni ndugu;
(e) Kwamba haki, usawa na ustawi wa kila mwananchi ndio ngao ya umoja, undugu, mshikamano na amani ya taifa;
(f) Kwamba kuheshimu na kulinda utu na haki zote za binadamu na pia kutii Katiba na sheria ndio msingi mkuu wa utamaduni Taifa;
(g)Kuhakikisha kuwa hakuna unyonyaji wa mtu na mtu mwingine;
(h)Kwamba maliasili, mazingira na utajiri wa Taifa ni rasilimali za Taifa kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania wa kizazi cha sasa na 

vizazi vijavyo na kamwe hazitafujwa, kupokonywa au kuvunwa kinyume cha maslahi ya taifa;
(i) Kuhakikisha kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa kwa ulinganifu na kwa uadilifu;
(j) Kuhakikisha kwamba kila kitendo cha mamlaka ya dola au cha kiongozi yeyote mwenye madaraka kina lengo la kuliletea taifa manufaa kwa 

maana ya kuweka maslahi ya taifa mbele kabla ya kujali maslahi binafsi:
6
(k)Kwamba ni wajibu wa dola kumwandaa raia kielimu na kiujuzi ili kumwezesha kila mmoja kumudu kupata na kuendesha shughuli halali za 

kujipatia riziki yake ama kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri;
(l) Kwamba haki za binadamu zilizotamkwa na Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu la mwaka 1948 kuhusu haki za Binadamu na zilizotamkwa 

katika Mkataba wa Haki za Binadamu na za Jamii wa Umoja wa Afrika wa mwaka 1981 vitachukuliwa kuwa ni sehemu ya Katiba hii;
(m) Kwamba dola na vyombo vyake vyote vitatoa haki na fursa sawa kwa raia na wananchi wote wa Tanzania bila ya kujali jinsia, rangi, 

kabila, dini, imani ya kisiasa wala hali ya mtu;
(n)Kwamba aina zote za dhuluma, uonevu, vitisho, ukandamizaji, ufisadi, ubaguzi, upendeleo na rushwa zinakuwa mwiko na kukomeswa kabisa;
(o)Kwamba shughuli zote za uendeshaji wa mamlaka za dola zitafuata misingi ya uwazi, ukweli na uwajibikaji na kuwa Bunge la Jamhuri ya 

Shirikisho ya Tanzania litakagua na kudhibiti utendaji wa vyombo-dola pamoja na kuridhia mikataba muhimu ya umma. Baraza la Wawakilishi la 

Tanganyika na la Zanzibar yatafanya hivyo kwa mamlaka za Tanganyika na Zanzibar kila moja kwa eneo lake;
(p)Kwamba serikali itazisaidia na kuziimarisha taasisi za kijamii ili ziweze kutoa huduma za kuharakisha shughuli za maendeleo ya wananchi 

na kukuza utamaduni wa kidemokrasia.
9. (1) Katika utetekelezaji wa kazi na wajibu wake, mamlaka zote dola zitakuwa na jukumu na wajibu wa kutii na kuzingatia maadili na 

misingi yote iliyotamkwa kwenye Sehemu hii ya Katiba hii.
(2) Misingi hii itakuwa chanzo cha sera na sheria za nchi.
7
SURA YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU
HAKI YA USAWA
10.(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake na ni marufuku kumtesa, umtweza au kumdhalilisha mtu;
11.(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria;
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na Mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania au inayotumika nchini kuweka 

sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake isipokuwa kama imefanyika hivyo ili kurekebisha athari mbaya ya 

ubaguzi wa jinsia au kundi lolote la watu;
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na Jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria;
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au na mamlaka yoyote inayotekeleza madara yake chini ya sheria yoyote au katika 

utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi;
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno “kubagua”maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu 
mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, jinsia, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, dini, rangi au hali yao ya maisha kwa 
namna ambayo watu wa aina fulani wanafanyiwa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa masharti au vikwazo au masharti ya vipingamizi 
ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au
wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima;
(6) Kwa madhumini ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba:-
(a) wakati haki na wajubu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi na mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa 
na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama ao chombo hicho kinginecho kinachohusika, kwamba shauri hilo litasikilizwa bila kuchelewa na kwamba utoaji wa haki utatawala taratibu zilizowekwa na sheria kusaidia usikilizaji na ufanyaji wa maamuzi;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku mtu kukamatwa kuathibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia 

kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati wa kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa 

mambo ya jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
12. (1) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa wajibu wa mtu kufanya kazi, na
9
haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi na bila 

kuathiri haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake;
(2) Bila ya kuathiri uhuru na haki ya kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na vipaji vyake, kila raia 

anayo haki ya kupatiwa elimu hadi kufikia upeo wowote kulingana na vipaji vyake, na Bunge litatunga sheria na serikali itaweka taratibu za 

kuhakikisha kuwa fursa ya elimu imetolewa sawa kwa wananchi wote;
(3) Serikali itahakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesah kupata elimu na mafunzo katika ngazi zote za 

shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.
HAKI YA KUISHI
13.(1) Kila mtu anayo haki ya kuishi, kuwa huru na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake;
(2) Ni marufuku kwa mtu, taasisi au mamlaka yoyote kuharibu au kuteketeza kwa sababu zozote zile mfumo au miundombinu ya maisha ya mtu, 

kundi au jamii ya watu bila kumshirikisha. Mtu, kundi au jamii itakayoathiriwa na pia kuchukua hatua za kufidia kwa ukamilifu na 

kurerejesha mfumo au miundombinu mbadala ya ile iliyoharibiwa au kuteketezwa;
(3) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru na kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru, na kuishi kwa uhuru, 

itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa na kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu, kunyang’anywa uhuru au 

vinginevyo, isipokuwa tu:-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria inayohusu upelelezi wa makosa ya jinai; au
10
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokaa mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
14.(1) kila mtu anastahili kuheshimiwa na kulindiwa usiri wa nafsi yake, jinsia yake, umbile lake, maisha yake binafsi na ya familia yake 

na unyumba wake, na pia heshima, usiri na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake binafsi;
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Bunge litatunga sheria kulinda heshima, usiri na usalama wa mtu, 

familia na maskani binafsi visiingiliwe kinyume cha Katiba na sheria za nchi;
15.(1) Kila raia wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na kuishi 

katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutiswa kuhama au kufukuzwa kutoka katika shirikisho.
(2) Sheria za nchi zitaweka taratibu na mipaka ya haki iliyolindwa na ibara hii bila bila kuvunja, kudhoofisha au kwenda kinyume cha ibara 

hii.
HAKI YA KUWA NA FAMILIA
16.(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa na familia, kuoa na kuolewa kwa hiari bila kuwekewa pingamizi kutokana na rangi, kabila, dini, jinsia, 

itikadi au hali yake ya maisha;
(2) Ndoa itafungwa kati ya mume na mke kwa hiari na familia itakuwa kitengo muhimu katika mfumo wa jamii kitakacholindwa na kustawishwa 

kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi;
(3) Wanandoa watakuwa sawa na kufaidi haki sawa kwa mujibu wa katika hii;
(4) Watoto ni hazina na rasilmali kuu ya taifa hivyo Mamlaka za dola na za kijamii zitahakikisha kuwa kila mtoto anapata 11
ulinzi, hifadhi, lishe, tiba, malezi na elimu bora. HAKI YA KUMILIKI MALI
17. (1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali binafsi kwa njia halali ama peke yake au kwa ushirikiano na mtu yeyote mwingine;
(2) Ni marufuku mtu yeyote ambaye anamiliki mali binafsi kwa halali kunyang’anywa au kutaifishiwa mali yake;
(3) Ikiwa ni lazima kwa maslahi ya taifa mali binafsi kutaifishwa, basi mamlaka ya dola itashauriana na mwenye mali na kukubaliana thamani 

ya fidia ilmradi kwamba hakuna mali itakayotaifishwa kabla ya thamani iliyokubaliwa na mwenye mali kulipwa; (4) Ikiwa mali inayotaifishwa 

ni ardhi basi mamlaka ya dola itahakikisha kuwa pamoja na masharti ya Ibara ndogo ya (3), raia aliyetaifishiwa ardhi yake anapewa ardhi 

mbadala na muda wa kutosha kujenga makazi mbadala;
HAKI YA KUANDAMANA
18. Raia wanayo haki ya kuandamana kwa amani bila kizuizi na utakuwa wajibu wa Mamlaka ya dola kuhakikisha kuwa raia wanapoandamana kwa 

amani hawabugudhiwi, na kunyanyaswa na vyombo vya usalama.
HAKI YA UHURU WA MAWAZO
19. (1) Kila mtu anao uhuru wa kuwa na mawazo yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea au kutoa habari na dhana zozote 

kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati;
(2) Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa za matukio mabalimabali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za 

binadamu na pia taarifa kuhusu masuala muhimu kwa jamii.
12
(3) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vinayo haki ya kupata habari kutoka taasisi za umma na binafsi kwa mujibu wa Katiba hii.
20.(1) Kila mtu anao uhuru wa kuamini dini aipendayo na pia haki ya kubadili dini au imani yake bila kuingiliwa, kutishwa au kulazimishwa;
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini ni jambo la hiari la mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini 

hazitaingiliwa na Mamlaka yoyote ile ya dola;
(3) Ifahamike kwamba neno “dini” katika Katiba hii ni pamoja na madhehebu ya dini, imani na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na 

neno hilo.
HAKI YA KUSHIRIKIANA
21.(1) Kila mtu ana haki ya kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa 

mawazo hadharani, na kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani, itikadi au 

maslahi mengineyo;
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii na ibara ya 6.(3) ya Katiba hii, haitakuwa halali kuandikishwa kwa chama 

cha siasa ambacho kutokana na Katiba, kanuni au sera zake:-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(b)kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania kinyume cha Katiba hii;
(c) kinapigania matumizi ya shari na mapambano ya silaha kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa;
13
(d)kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(e) Hakina kanuni inayoruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia ya kidemokrasia.
(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti yatayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo vilivyowekwa na 

Katiba hii;
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama cha siasa au chama chochote cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya 

itikadi au falsafa yake;
(5) Utaratibu wa vyama vya siasa kuweka wagombea katika uchaguzi wa viongozi wa ngazi zote za vyombo vya uwakilishi vya dola 

hutamlazimisha raia kuwa mwanachama wa chama cha siasa ili kupata sifa ya kuteuliwa kuwa mgombea.
(6) Bila kujali masharti ya ibara ya 21 kuhusu haki ya kushirikiana, Ssheria ya Bunge inaweza kuweka mipaka ya matumizi ya haki hiyo kwa 

baadhi ya watendaji wakuu wa vyombo vya dola ili kulinda uhuru, ubora wa utendaji wa wakuu hao na imani ya umma kwa ujumla kwa vyombo 

wanavyoviongoza.
HAKI YA KUPIGA NA KUPIGIWA KURA
22.(1) Kila mwananchi aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga au kupigiwa kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania 

na wananchi;
(2) Bunge litatunga sheria na kuweka masharti yanayolinda na kuwezesha utekelezaji wa haki ya kupiga au kupigiwa kura ilmradi kwa mujibu 

wa ibara hii watu wafuatao hawatakuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa na wananchi nchini Tanzania;-
(a) Raia wa nchi nyingine;
(b)Mgonjwa wa akili;
14
(c) Mhaini;
(d)Mwaanchi asiye na hati ya kupiga kura
(3) Katika kutekeleza wajibu wake uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii na masharti ya ibara ya 21(6) ya Katiba hii, Bunge 

litatunga sheria itakayozuia haki ya watu wafuatao kupigiwa kura katika uchaguzi unaofanywa na wananchi nchini Tanzania:-
(a)Mwananchi ambaye kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii hana sifa za kuteuliwa kama mgombea
(b)Mwananchi ambaye kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 21(2) ya Katiba hii hana sifa za kupiga kura.
(4) Bunge litatunga sheria ya Uchaguzi na kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo;
(a) utaratibu endelevu na wa kudumu wa uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa 

wanachi unaofanywa nchini Tanzania;
(b) utaratibu wa kudumu wa kutunza na kuhakiki wapiga kura waliomo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura;
(c) utaratibu wa kumwezesha mpiga kura aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu nyingine au kuhamisha usajili wake wa kupiga kura;
(d) Kutaja wajibu na shughuli za Tume za Uchaguzi na utaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwa na Tume hizo;
(e) Kila yalipotumika maneno ”uchaguzi unaofanywa na wananchi nchini Tanzania” ieleweke kuwa maneno hayo yana maana ya uchaguzi wa Rais wa 

Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, Magavana wa Tanganyika na Zanzibar, Wabunge wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, Wajumbe wa Baraza la 

Wawakilishi la Tanganyika na la Zanzibar na Madiwani wa Serikali za Mitaa za Tanganyika na Zanzibar na kwamba uchaguzi huo utafanyika 

katika vipindi vya mara kwa mara vilivyowekwa na sheria ya uchaguzi katika mazingira huru, ya siri na haki.
15
HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA UTAWALA
23.(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 22 ya Katiba hii kuhusiana na masharti ya kupiga na kupigiwa kura kila raia wa Tanzania anayo 

haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia uwakilishi kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au 

yanayolihusu Taifa.
HAKI YA KUFANYA KAZI
24.(1) Kila mtu anayo haki na hiari ya kufanya kazi anayoipenda na ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa raia wanawezeshwa kielimu, 

kiujuzi na rasilmali kuweza kujishughulisha kiuchumi kujipatia riziki halali kwa ajili ya maisha yao;
(2) Kila raia anayo fursa na haki sawa, kwa masharti ya usawa, ya kushika nafasi yoyote iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi
(3) Kila mtu, bila ya ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira wa haki unaolingana ujuzi na kazi yake, na watu wote wanaofanya 

kazi kulingana na uwezo na ujuzi wao watapata malipo kulingana na kiasi cha sifa na kazi wanayoifanya;
(4) Kila mtu anao wajibu wa kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali ya uzalishaj mali na kujitahidi kufikia malengo ya 

uzalishaji binafsi na yale ya pamoja;
(5) Ni marufuku mtu yeyote kufanyishwa kazi ya shuruti na kwa madhumiuni ya ibara hii ifahamike kwamba kazi yoyote haitahesabiwa kuwa ni 

kazi ya shuruti endapo kazi hiyo ni-
(a) kazi inayobidi ifanywe kutokana na hukumu au amri ya mahakama
(b) Kazi inayobidi ifanywe na askari wa jeshi lolote katika kutekeleza majukumu yao;
16
(c) Kazi yoyote ambayo mtu inabidi aifanye kutokana na kuwapo hali ya hatari au baa lolote linalotishia uhai wa mtu, watu au usalama wa 

jamii.
UHURU WA KUJIAMULIA MAMBO. 
25,(1) Raia wa Tanzania kwa pamoja wanayo haki ya kujiamulia mambo yao wenyewe na kukubaliana katika mambo yanayohusu uhuru wa nchi, siasa 

na jinsi ya kujiletea maendeleo ya uchumi na utamaduni;
(2) Raia wa Tanzania kwa pamoja wanayo haki ya kumiliki na kuvuna na pia wanao wajibu wa kuhifadhi rasilimali asili na utajiri wa nchi yao 

na ni marufuku kwa mtu yeyote au mamlaka ya dola au binafsi kuweka saini mkataba wowote unatwaa au kudhoofisha haki hii au kuruhusu 

umiliki na uvunaji wa rasilmali asili na utajiri wa nchi kuwa mikononi mwa watu wasio raia au mashirika ya nje pasipo na ubia wa raia wa 

Tanzania;
(3) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania litatunga sheria kuweka masharti yatakayohakikisha kuwa umilikaji, uvunaji na uhifadhi wa 

rasilimali asili na utajiri wa nchi vinafanywa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ya Katiba hii;
(4) Watanzania wanayo haki ya kulinda na kuendeleza utamaduni wao pamoja na mifumo ya maisha, uchumi na mila bora zinazoendana utamaduni 

wao;
WAJIBU WA KUTII NA KULINDA KATIBA
26. (1) Kila mtu anao wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za nchi;
(2) Kila mtu anayo haki kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Katiba hii, kuchukua hatua za kuilinda Katiba hii na sheria za nchi;
(3) Bila kuathiri masharti ya ibara hii kila mtu anayo haki ya kupinga kufutwa, kubadilishwa au kuvunjwa kwa 17
Katiba hii kinyume na utaratibu uliowekwa na Katiba hii.
(4) kila mtu anao wajibu wa kuiheshimu mali ya mtu mwingine, kulinda mali asili, utajiri wa nchi, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote 

inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.
(5) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka na umoja wa Taifa.
ULINZI WA TAIFA
27.(1) Ulinzi wa Taifa ni wajibu wa kila mwananchi na utapewa kipaumbele katika sera, sheria na shughuli za Mamlaka ya dola;
(2) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania. linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi ya nchi 

na kushiriki katika ulinzi wa Taifa;
(3) Mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania hatakuwa na haki ya kuweka saini kwenye mkataba wa kusalimu amri au 

kukubali kutekwa kwa nchi au wa sehemu yoyote ya nchi, kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko wa Tanzania;
(4) Bila ya kujali masharti yoyote yaliyomo katika Katiba hii, hakuna mtu au Mamlaka yoyote itakayokuwa na haki ya kuwazui raia wa 

Tanzania kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi;
(5) Uhaini ni jinai kuu dhidi ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kosa la uhaini na Mahakama 

Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, atapewa adhabu ya kifo;
(6) Uhaini maana yake ni kitendo cha mtu yeyote:-
(a) Kumuua, au kujaribu kumuua au kula njama ya kumua Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania; au
18
(b) Kuanzisha vita au kusaidia adui katika vita dhidi ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania.
MASHARTI YA KULINDA JAMHURI
28.(1) Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni Taifa linaofuata urithishano wa mamlaka ya dola wa kijamhuri na hivyo raia yeyote wa Tanzania 

hatapewa haki, hadhi au cheo maalum kwa msingi wa nasaba;
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa raia yeyote wa Tanzania msingi wa nasaba;
(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa 

namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
NGUVU YA SURA YA HAKI ZA BINADAMU
29. (1) Haki za Binadamu zilizoainishwa na kulindwa na sura hii ya Katiba ni za msingi kwa binadamu wote na walengwa maalumu waliotajwa 

kwenye ibara za Katiba hii na hivyo hazitadhoofishwa, kufutwa au kuzidiwa nguvu na masharti ya sheria nyingine yoyote;
(2) Baraza la Kutunga Katiba halitafuta sura hii ya haki za binadamu au kuifanyia marekebisho yanayoidhoofisha kwa namna yoyote ile;
(3) Sheria zote za Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na za Tanganyika na Zanzibar zitafungamana na masharti ya Katiba hii na kila itokeapo 

kwamba sheria, kanuni au mila yenye nguvu za kisheria inayotumika nchini inapingana na masharti ya Katiba hii, basi iwavyo vyovyote vile 

sheria au kanuni hiyo itakuwa batili kwa kiwango inachopingana na Katiba hii;
(4) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sura hii ya haki za Binadamu hayabatilishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria 

yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya-
19
(a) ulinzi na usalama wa Taifa;
(b)kutekeleza hukumu au amri ya mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai au la jinai;[je tuiondoe ibara hii?]
(4) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika sehemu hii ya sura hii ya Katiba au haki yoyote katika sheria yoyote inayohusu haki na 

wajibu wake limevunjwa, linavunjwa au linaelekea kuvunjwa na mtu, taasisi au mamlaka yoyote katika jamhuri ya Shirikisho la Taanzania 

anayo haki ya kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Shirikisho au Mahakama Kuu ya Tanganyika au Zanzibar kulinda, kurejesha au kutetea 

haki yake;
(5) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania linaweza kutunga sheria inayoweka utaratibu wa kufungua mashauri yatokanayo na sura hii ya 

haki za binadamu kwenye Mahakama za Shirikisho au Mahakama za Tanganyika au Zanzibar kwa namna ambayo itarahisisha haki kupatikana kwa 

njia fupi na rahisi;
(6) Bila ya kuathiri nguvu na mamlaka ya Mahakama za nchi yaliyowekwa na katiba hii, itakaposikiliza na kutoa hukumu yake kuhusu shauri la 

kuvunjwa kwa haki za binadamu kwa mujibu wa Katiba hii, Mahakama zitakuwa na mamlaka ya kutoa amri ya zuio; tamko kuwa kitendo, sheria au 

kanuni inayolalamimiwa ni batili; amri ya malipo ya fidia au amri ya kurejeshewa haki iliyotwaliwa au kuvunjwa;
(7) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika katiba hii, Mahakama za nchi kwa kadri itakavyoagizwa na katiba hii au sheria za 

nchi zitakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa kwa mujibu wa ibara hii na rufaa kutoka 

hukumu za mahakama hizi zitapelekwa kwenye Mahakama za ngazi ya juu kulingana na mfumo na utaratibu uliowekwa na sheria.
20
SURA YA NNE
HALI YA HATARI NA MASHARTI YAKE
30. (1) Mbali na masharti ya ibara ya 29(1), sheria yoyote iliyotungwa na Bunge haitakuwa batili kwa sababu tu kwamba inawezesha hatua 

kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, ambazo zinakiuka masharti ya haki za binadamu zilizolindwa na Katiba hii;
(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati usio wa hali 

ya hatari;
(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayataidhinisha mtu kunyang’anywa haki yake ya kuwa hai;
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii na ibara zifuatazo za sehemu hii “wakati wa hali ya hatari” maana yake ni kipindi chochote ambapo Tangazo 

la Hali ya Hatari, lililotolewa na Rais kwa kutumia uwezo aliopewa katika ibara ya 31, linatumika.
31. (1) Bila ya kuathiri Katiba hii Rais aweza kutangaza hali ya hatari katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania au katika sehemu yake 

yoyote;
(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari kama:-
(a)Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania iko katika vita; au
(b)kuna hatari kwamba Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita; au
(c) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Tanzania au sehemu yake 

yoyote ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee; au
(d)karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa la kimazingira ambalo linatishia jamii katika Tanzania;
21
(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Tanzania nzima, au katika Tanganyika nzima au Zanzibar nzima, Rais atatuma mara 

moja nakala ya tangazo hilo kwa spika wa Bunge ambaye, ataitisha mkutano wa Bunge, ndani ya siku zisizozidi tatu, ili kuitafakari hali ya 

mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote, la 

kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais;
(4) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibu wa ibara hii litakoma kutumika:-
(a)wakati wowote ambapo Bunge litalitangua tangazo hilo kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya 

wajumbe wote.
(b)endapo zitapita siku saba tangu tangazo lilipotolewa kabla ya kupitishwa azimio lililotajwa katika ibara ndogo ya (3);
(c) iwapo litafutwa na Rais;
(d)baada ya kupita muda wa miezi mitatu tangu tangazo hilo lilipothibitishwa na Bunge na kikao cha Bunge hakijapiga kura iliyoungwa na 

theluthi mbili ya wabunge wote kuongeza muda mwingine wa hali ya hatari;
(e) baada ya kupita jumla ya miezi kumi na miwili tangu hali ya hatari itangazwe na mazingira yenyewe yamebadilika kwa kurejea hali ya 

amani na utulivu.
(5) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusu nyakati na utaratibu ambao utawawezesha Rais kupata ushauri wa watu au taasisi 

fulani nchini Tanzania kabla ya kuchukua hatua za kutangaza hali ya hatari au kutangaza vita;
(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge 

inayohusu utangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii, yatatumika tu katika sehemu ya Tanzania ambapo hali hiyo ya 

hatari imetangazwa.
22
SURA YA TANO
SERIKALI YA SHIRIKISHO
SEHEMU YA KWANZA
RAIS
32. (1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
MAMLAKA YA RAIS
33.(1) Rais wa Shirikisho la Tanzania atakuwa na mamlaka yafuatayo:
(a) Uteuzi wa wakuu wa majeshi, na viongozi wote wa dola ambao lazima wateuliwe na rais kwa mujibu wa katiba hii;
(b) Kuunda serikali na kuteua baraza la mawaziri
( c) Kudhibiti nidhamu ya
watendaji wa umma © Mkuu Ljamhuri ya muungano AIS ATAKUWA
33. (1) Kutakuwa na Serikali ya Shirikisho ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Shirikisho katika Jamhuri ya Shirikisho la 

Tanzania;
(2) Mamlaka ya Serikali ya Shirikisho yatahusu utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo yote ya Shirikisho;
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Shirikisho juu ya mambo yote ya Shirikisho yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la 

Tanzania, vyombo vya Shirikisho lilivyoundwa na
23
Katiba hii na vyombo vingine vilivyokabidhiwa utekelezaji wa mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba hii;
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Shirikisho yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja 

au na vyombo vya Shirikisho vilivyoundwa na Katiba hii au kwa Rais kukabidhi madaraka hayo kwa watu na vyombo vingine kwa mujibu wa katiba 

hii;
(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayatahesabiwa kwamba-
(a)yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au mamlaka yoyote ambayo si Rais; au
(b)yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka yoyote ambayo si Rais.
34. (1) Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Shirikisho zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Umma.
(2) Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika Sheria iliyotungwa na 

Bunge na kanuni zilizowekwa na vyombo vya Shirikisho kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii.
35. (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii Rais kwa kushauriana na Tume zinazohusika atakuwa na mamlaka ya 

kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho;
(2) Mamlaka ya kuwateua watu kushika nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho, na pia mamlaka ya kuwapandisha vyeo 

watu hao, kuwaondoa katika madaraka, kuwafukuza kazi na mamlaka ya kudhibiti nidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi 

Rais, Tume zinazohusika na mamlaka mengineyo yaliyotajwa na kupewa 24
madaraka kuhusu nafasi yoyote au aina ya nafasi za madaraka kwa mujibu wa Katiba hii.
36. (1) Katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote au chombo chochote anapotakiwa 

kupata ushauri au ushiriki kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, laweza kuwasilisha kwa 

Rais wa Mahakama ya Rufani azimio la kumwomba Rais, wa Mahakama athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili hawezi 

kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio kama hilo, Rais wa Mahakama ndani ya siku saba atateua bodi ya utabibu ya watu wasiopungua 

watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matabibu ya Tanzania, na bodi hiyo itachunguza suala hilo na 

kumshauri Rais wa Mahakama ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakiri ushahidi wa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha 

kwamba Rais kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na iwapo Rais wa Mahakama hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku 

saba baada ya kuliwasilisha kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesebiwa kwamba kiti cha Rais, kiwazi na masharti 

yaliyomo katika ibara ndogo ya (3) yatatumika;
(3) Ikitokea kwamba kiti cha Rais kiwazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha Rais kiwazi kutokana 

na sababu nyingine yoyote, na endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa 

na mmojawapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani:-
(a)Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi
(b)Waziri Mkuu na kama nafasi yake iwazi au kama nayeye hayupo au ni mgonjwa; basi.
25
(c) Gavana wa Tanganyika au, Zanzibar kwa mlolongo huo;
(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (a), (b) na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Rais 

kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza kazi na shughuli hizo 

mara tu mtu huyo mwingine anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kutekeleza kazi na shughuli za Rais.
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake 

kutokana na maradhi ya mwili au akili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Waziri Mkuu wa Shirikisho ataapishwa na 
atakuwa Rais na uchaguzi wa Rais utafanyika ndani ya miezi mitatu isipokwa tu pale ambapo muda wa Bunge uliobakia hauzidi miezi sita uchaguzi wa Rais utasubiri uchaguzi mkuu;
(6) Ifahamike kwamba kiti cha Rais hakitakuwa wazi na Rais hatahesabiwa kwamba hayuko katika Jamuhuri ya Shirikisho endapo Rais:-
(a)atakuwa yupo nchini lakini hayupo katika mji ambao makao makuu ya Serikali ya Jamuhuri ya Shirikisho yapo;
(b)atakuwa hayupo katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania kwa kuwa yuko safarini kikazi; au
(c) atakuwa si mgonjwa mahututi au yapo matumaini kuwa atapata nafuu na kurejea kazini katika kipindi cha miezi kumi na miwili tangu 

alazwe hospitalini.
(7) Iwapo kutatokea lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika ibara ndogo ya (6) na Rais akiona kuwa inafaa kukabidhi madaraka yake kwa muda 

basi aweza kutoa maagizo kwa maandishi ya kumteua yeyote kati ya watu waliotajwa katika ibara ndogo ya (3) ya ibara hii ili mtu huyo 

atekeleze madaraka ya Rais wakati yeye hayupo au ni mgonjwa, na mtu huyo atakayetekeleza madaraka hayo ya Rais kwa kufuata
26
masharti yoyote yatakayowekwa na Rais katika hati ya kukabidhi madaraka ya Rais;
(8) Kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo, Rais hatakuwa na mamlaka ya kutekeleza mamlaka yake aliyokabidhi katika kipindi kile 

ambacho amekabidhi mamaka ya Rais na hajarejea kazini;
(8) Rais aweza, akiona inafaa kufanya hivyo, na baada ya kushauriana na Waziri Mkuu kumwagiza kwa maandishi Waziri yeyote kutekeleza kazi 

na shughuli zozote za Rais ambazo Rais atazitaja katika hati ya maagizo yake na Waziri aliyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara 

hii ndogo, atakuwa na mamlaka ya kutekeleza kazi na shughuli hizo kwa kufuata masharti yoyote yaliyowekwa na Rais, lakini bila ya kujali 

masharti ya sheria nyingine yoyote; isipokuwa kwamba-
(a)Rais hatakuwa na mamlaka ya kukabidhi kwa Waziri kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo kazi yoyote ya Rais aliyokabidhiwa na sheria 

yoyote inayotokana na masharti ya mkataba wowote uliotiwa sahihi na Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania iwapo kisheria Rais haruhusiwi 

kukabidhi kazi hiyo kwa mtu mwingine yoyote.
(b)Rais hatakuwa na mamlaka ya kukabidhi kwa Waziri kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo kazi au mamlaka yoyote ya Rais 

aliyokabidhiwa na sheria yoyote ambayo ni lazima yatekelezwe na Rais mwenyewe;
(c) Ifahamike kwamba maagizo yanayotolewa na Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo, ya kumwagiza Waziri yeyote kutekeleza kazi 

yoyote ya Rais, hayatahesabiwa kwamba yanamzuia Rais kutekeleza kazi hiyo yeye mwenyewe.
(9) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii, mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanywa kwa ajili ya kuwasilisha kwa Rais wa 

Mahakama azimio kuhusu hali ya afya ya Rais utahesabiwa kuwa ni mkutano halali ikiwa theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza hilo 

wamehudhuria, na
27
itahesabiwa kuwa Baraza limepitisha azimio hilo ikiwa litaungwa mkono kwa kauli ya wajumbe walio wengi waliohudhuria mkutano na kupiga 

kura;
(10) Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katika ibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais kwa mujibu wa ibara 

hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge, kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake, kufuta uteuzi wowote uliofanywa na 

Rais au kuteua mtu yeyote kushika nafasi ambayo Katiba hii imekabidhi mamlaka ya uteuzi kwa Rais mwenyewe;
(11) Mtu yeyote atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kama ni Mbunge hatapoteza kiti chake katika 

Bunge wala hatapoteza sifa zake za kuchaguliwa kuwa Mbunge kwa sababu tu ya kutekeleza kazi na shughuli za Rais kwa mujibu wa masharti ya 

ibara hii.
37. (1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa Sheria itakayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa 

Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata masharti ya Katiba hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha Rais kitakuwa kiwazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi hiyo 

itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a)baada ya Bunge kuvunjwa;
(b)baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bunge kwanza;
(c) baada ya Rais kupoteza sifa za kuchaguliwa au kushika Kiti cha Rais;
(d)baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba hii, na Bunge kupitisha azimio la kumwondoa katika madaraka ya Rais;
(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 36 ya Katiba hii kwamba Rais hawezi kumudu kazi na shughuli zake;
28
(f) kama Rais atavunja Katiba hii au Sheria ya Maadili ya Viongozi;
(g) baada ya Rais kufariki
(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tu ya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
38. (1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania isipokuwa tu kama:-
(a)ni raia wa kuzaliwa wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ya Uraia,
(b)ametimiza umri wa miaka arobaini,
(c) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;
39. (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi 

kingine cha miaka mitano kushika kiti hicho;
(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano kushika kiti cha Rais;
(3) Mtu aliyewahi kuwa Gavana wa Tanganyika au wa Zanzibar hatapoteza sifa za kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la 

Tanzania kwa sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Gavana wa Tanganyika au wa Zanzibar.
40. (1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 37 na inalazimu 

uchaguzi wa Rais kufanyika, kila raia mwenye sifa mujibu wa Katiba hii na Sheria ya Uchaguzi anayependa kugombea kiti cha Rais atatekelza 

mchakato wa uteuzi ili kuwa mgombea katika uchaguzi wa Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania
29
(2) Ifahamike pia kwamba mtu yeyote atakayependa kugombea Kiti cha Rais bila kupitia chama chochote cha siasa atawasilisha jina lake kwa 

Tume ya Uchaguzi baada ya kutimiza masharti ya kuungwa mkono na wapiga kura sawa kama wagombea walioteuliwa na vyama vya siasa;
(3) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na saa itakayopangwa Tume, 

na mtu hatakuwa amependekezwa kama hajaungwa mkono na wananchi wapiga kura kwa idadi na kwa namna itayotajwa na Sheria iliyotungwa na 

Bunge.
(4) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu ambaye 

anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilisha jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au kumkataa kwa mujibu wa masharti ya 

ibara hii na ya Sheria iliyotungwa na Bunge;
(5) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania utafanywa siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria 

iliyotungwa na Bunge.
(6) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika Sheria iliyotungwa na Bunge kwa 

ajili hiyo.
(7) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo amepata zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa 

au, kama uchaguzi umerudiwa kwa sababu ya kutopatikana mgombea mwenye zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa atatangazwa yule 

aliyepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine;
(8) Endapo mgombea wa kiti cha Rais hakuchaguliwa, basi Tume itamtangaza kuwa mbunge wa taifa ikiwa atakuwa amepata asilimia moja ya kura 

alizopata mshindi wa kiti cha Rais.
30
41. (1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali 

yoyote ile itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku ishirini na moja;
(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika ibara ndogo 

ya (5), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais;
(3) Rais atashika kiti cha Rais hadi:-
(a)Siku ambapo Rais Mteule atakula kiapo cha Rais; au
(b)Siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
(c) Siku atakapojiuzulu; au
(d)Atakapoondolewa kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(4) Iwapo Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania inapigana vita dhidi ya adui na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bunge laweza 

mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wa miaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii isipokuwa kwamba muda 

wowote utakaoongezwa kila mara hautazidi miezi sita, na kwamba nyongeza hiyo kwa jumla isizidi miezi kumi na miwili;
(5) Kila Rais Mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka ya Rais ataapa mbele ya Rais wa Mahakama ya 

Rufani, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria 

iliyotungwa na Bunge.
42. (1) Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo, na atakapostaafu atapokea malipo ya Rais Mstaafu ambayo ni sawa na asilimia themanini 

ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, kiinua mgongo, malupulupu malipo na stahili nyinginezo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge 

na malipo yote hayo na stahili nyinginezo vitatokana na Akaunti
31
ya Fedha ya Shirikisho na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii;
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais akiwa madarakani kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(3) Rais hatakuwa mwajiriwa wa muda au wa kudumu wa mtu, taasisi au mamlaka yoyote na hatamiliki wale kufanya shughuli nyingineyo ya 

kiuchumi nje ya kazi na wajibu wake wa Rais.
(4) Mali na shughuli za kiuchumi za Rais Mteule vitahesabiwa na kukabidhiwa kwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali kabla Rais Mteule hajala 

kiapo cha Rais na vitaendeshwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na kukabidhiwa tena kwake miaka kumi baada ya kustaafu kama Rais.
43. (1) Bila ya kuathiri Katiba hii, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali ya vita kati ya Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania na nchi 

yoyote;
(2) Baada ya kutangaza vita, Rais atapeleka mara moja nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi 

wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani ya siku tatukuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha mkutano wa Bunge ili kuitafakari hali ya mambo na 

kupitisha au kutopisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita lililotolewa na Rais litakaloungwa mkono wa kura za wabunge wasiopungua 

theluthi mbili ya wabunge wote.
44. (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza baada ya kushauriana na chombo kitakachoundwa na 

sheria ya Bunge kwa ajili hiyo kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a)kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa
32
msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b)kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu 

hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d)kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu 

ya kutoza, au kuchukua kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vingenevyo kingechukuliwa na Serikali ya Shirikisho.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa ibara 

hii;
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa na mahakama kwa mujibu wa sheria za Shirikisho
45. (1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha 

mashtaka ya aina yoyote dhidi yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai alilotenda akiwa Rais katika kutimiza shughuli au mamlaka 

yake ya Rais; [ je tuifute ibara hii ili ibakie ibara ndogo ya tatu?]
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri la daawa 

kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, 

ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya daawa kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au kutumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi 

kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa
33
inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina la mdai, anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa 

analodai;
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46(10), itakuwa ni marufuku kumshitaki au kufungua 

mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo 

lolote alilofanya akiwa Rais katika utekelezaji wa shughuli na mamlaka yake ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.
46. (1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 45 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo 

itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii;
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais:-
(a)ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinavunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b)amekiuka masharti ya ibara ya 42 (3) na (4) ya Katiba hii;
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama:-
(a)taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa 

Spika siku thelethini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyotenda Rais, na ikipendekeza 

kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais iundwe ili ichunguze na kuleta mashtaka rasmi
34
dhidi ya Rais au ripoti rasmi ya kulithibitishia Bunge kuwa Rais hana hoja ya kujibu;
(b)wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta 

hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano wala 

kuliahirisha Bunge, lipige kura juu ya hoja ya kuundwa kwa Kamati Maalum ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais na kama ikiungwa mkono na 

Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote, atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais;
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao:-
(a)Rais wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b)Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(c) Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanganyika
(d)Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya zanzibar; na
(e) Wabunge wawili waliochaguliwa ba Bunge
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kwa hiyo kazi na madaraka ya Rais 

yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 36(3) ya katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na 

mashtaka yaliyotolewa dhidi yake;
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya uchunguzi kuundwa, itakaa, kuchunguza na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na 

kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge;
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku ishirini na moja, Kamati Maalum ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya 

Rais itatoa taarifa yake kwa Spika
35
ambaye ataiwasilisha bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(8) Taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais itawasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (7) Rais Mtuhumiwa akiwepo 

Bungeni, na kabla ya kuiijadili taarifa hiyo, Bunge litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha litaijadili na kupiga kura;
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais kwa 

theluthi mbili ya Wabunge wote, Spika atatangaza matokeo hayo na kumpa Rais Mtuhumiwa fursa ya kujiuzulu na kisha Spika atatangaza hapo 

hapo kuwa kiti cha Rais ki- wazi;
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya 

pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
47. (1) Bila ya kuathiri Katiba hii, viongozi wakuu wa vyombo vya dola katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania watawajibika, kila mmoja 

wao katika kutekeleza madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au Katiba ya Tanganyika au ya Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa wanalinda 

Katiba hii na kuimarisha na kudumisha umoja wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kila mmoja wapo wa viongozi wakuu wa vyombo vyote vya dola katika Jamuhuri ya 

Shirikisho la Tanzania kabla ya kushika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii ataapa kuitetea na kudumisha Katiba hii pamoja na umoja wa 

Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya ibara hii:-
36
(a)Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(b)Rais wa Mahakama ya Rufani
(c) Spika wa Bunge,
(d)Gavana wa Tanganyika;
(e) Gavana wa Zanzibar;
(f) Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Shirikisho,
(g) Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanganyika
(h)Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar,
(i) Spika wa Baraza la wawakilishi la Tanganyika
(j) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
SEHEMU YA PILI
MAKAMU WA RAIS
48. (1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya shirikisho kwa jumla, na hususan:-
(a)atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata wa mambo ya Shirikisho;
(b)atafanya kazi atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.
(2) Endapo Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania atatoka sehemu moja ya Jamuhuri, basi Makamu wa Rais atatoka sehemu ya pili ya 

Jamuhuri;
(3) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais, na atongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au 

shughuli zozote atakazokabidhiwa na Rais;
(4). Makamu wa Rais atachaguliwa katika uchaguzi mmoja pamoja na Rais na atashika madaraka ya Makamu wa Rais siku hiyo hiyo Rais 

anaposhika madaraka;
37
(5) Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na 

utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge;
(6) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi:-
(a)Rais atakapoacha kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania,
(b)akifariki dunia akiwa katika madaraka,
(c) atakapojiuzulu kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania.
SEHEMU YA TATU
BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI
WAZIRI MKUU
49. (1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Shirikisho atakayeteuliwa na Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika 

madaraka yake ataapa mbele ya Rais wa Mahakama ya Rufani Kiapo cha kuilinda na kuitetea katiba hii na ataapa mbele ya Rais kiapo 

kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge;
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku saba baada ya kuapishwa kushika madaraka yake, Rais atamteua mbunge yeyote 

anayeelekea kuwa ataweza kuongoza Baraza la Mawaziri kutekeleza sera za serikali ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania kwa mujibu wa Katiba 

hii kuwa Waziri Mkuu wa Shirikisho;
(2) Hati ya uteuzi wa Waziri Mkuu itawasilishwa Bungeni na Spika na uteuzi wake utakamilika baada ya kupigiwa kura na kuungwa mkono na 

kura za Wabunge walio wengi;
38
(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi:-
(a)siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
(b)siku atakapojiuzulu; au
(c) siku Rais atakapomteua mtu mwingine kuwa Waziri Mkuu; au
(d)siku ambapo ataapa kushika kiti cha Rais,au
(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu wa masharti mengineyo ya Katiba hii.
50. (1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya 

Shirikisho;
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni;
(3) Waziri Mkuu atatekeleza maamuzi yote ya Baraza la Mawaziri na maamuzi yote ya Bunge;
(4) Bila ya kuathiri Ibara hii, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza 

kwamba yatekelezwe.
51.(1) Rais atakuwa na mamlaka ya kuteua mwananchi yeyote asiye mbunge ila mwenye sifa za kuchaguliwa kama mbunge, kushika nafasi ya 

uwaziri katika serikali ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
(2) Serikali ya Shirikisho, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya Serikali ya Shirikisho kwa 

jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, watawajibika mmoja mmoja na kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za 

Serikali ya Shirikisho.
52. (1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au waziri yoyote endapo itatolewa
39
hoja kupendekeza hivyo na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii;
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyoya ibara hii, hoja yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au waziri 

yoyote haitatolewa Bungeni endapo:-
(a)haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu au waziri yoyote kwa mujibu wa Katiba hii wala hakuna madai kwamba Waziri Mkuu 

au waziri yoyote amevunja katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b)haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;
(c) haijapita miezi sita tangu hoja ya namna hiyo ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.
(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au waziri yotote haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama:-
(a)taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa kwa Spika, 

siku angalau kumi na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa Bungeni,
(b)Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa;
(4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itapitishwa tu iwapo itaungwa mkono na Wabunge 

walio wengi;
(5) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au waziri yeyote itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha azimio 

hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya kura ya 

kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au Waziri yeyote atatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua mtu mwingine kuwa Waziri Mkuu.
BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI
40
53. (1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Waziri Mkuu na Mawaziri wote;
(2) Kutakuwa na Wizara 15 kwa mujibu wa Ibara hii kama ilivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Tatu ya Katiba hii na Rais hataunda wizara mpya 

nyingine isipokuwa kwa ushauri wa Bunge;
(3) Waziri Mkuu ndiye atakayeongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri na endapo hayupo basi mikutano itaongozwa na Waziri yeyote 

atakayechaguliwa na mkutano miongoni mwa wajumbe wake;
(4) Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa 

mujibu wa masharti ya Katiba hii, litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo;
(5) Rais atawajibika kufuata ushauri wa Baraza la Mawaziri;
(6) Rais au Makamu wa Rais wanaweza kuhudhuria Mikutano ya Baraza la Mawaziri;
(7) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa mikutano hiyo 

isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.
54. (1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 53 watateuliwa na kuondolewa madarakani na Rais baada 

ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(2) Pamoja na Mawaziri waliotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua au 

kuwaondoa Mawaziri wa Nchi na Naibu Mawaziri ambao wote hawatakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri;
41
(3) Rais aweza kuteua Naibu Mawaziri ambao watawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao kwa idadi ambayo haitazidi 

idadi ya mawaziri.
(4).Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine 

chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
55. (1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.
(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa ki- wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a)endapo mwenye madaraka atafariki dunia;
(b)ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa na sifa za kuwa mbunge;
(c) ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;
(d)iwapo atachaguliwa kuwa spika;
(e) iwapo atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;
(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais Mteule hajashika madaraka hayo
(g) iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
56. Mawaziri na Naibu Mawaziri watalipwa mshahara, posho na malipo mengineyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
57.(1) Kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Shirikisho ambaye katika ibara zifuatazo za Katiba hii atatajwa tu kwa kifupi kama 

“Mwanasheria Mkuu” ambaye atateuliwa na kuondolewa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge.
42
(2) Mtu yeyote hatastahili kuteuliwa kushika madaraka ya Mwanasheria Mkuu isipokuwa tu kama kwa mujibu wa Katiba hii ana sifa maalum, 

zinazomwezesha kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani na amekuwa na hizo sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano;
(3) Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali ya Shirikisho juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo, atawajibika kutoa ushauri 

kwa Serikali ya Shirikisho kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria 

zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza, na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa kwake na Katiba 

hii au na sheria yoyote.
(4) Katika kutekeleza kazi na shughuli zake kwa mujibu wa ibara hii, Mwanasheria Mkuu atakuwa na haki ya kuhudhuria na kusikilizwa katika 

mahakama zote nchini;
(5) Mwanasheria Mkuu atalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
(6) Mwanasheria Mkuu atashika madaraka yake hadi:-
(a)Uteuzi wake utakapofutwa na Rais, au
(b)Mara tu kabla ya Rais Mteule kushika madaraka ya Rais.
58. Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri ambaye atakuwa ndiye mtendaji mkuu katika ofisi ya Baraza la Mawaziri, na atatekeleza 

shughuli zifuatazo kwa kufuata maagizo ya jumla au maalum atakayopewa na Waziri Mkuu yaani:-
(a)kuandaa ratiba ya mikutano ya Baraza na kutayarisha orodha ya shughuli za kila mkutano;
(b)kuandika na kuweka kumbukumbu za mikutano ya Baraza;
(c) kutoa taarifa na maelezo ya maamuzi ya Baraza kwa kila mtu au chombo cha umma kinachohusika na uamuzi wowote; na
43
(d)kutekeleza kazi na shughuli nyingine zozote atazoagizwa mara kwa mara na Waziri Mkuu.
SURA YA SITA
BUNGE LA SHIRIKISHO
SEHEMU YA KWANZA
BUNGE
59. (1) Kutakuwa na Bunge la Shirikisho ambalo litakuwa ndicho chombo kikuu cha utungaji wa sheria, uwakilishi na ushirikishwaji wa 

wananchi wa Tanzania katika shughuli dola na udhibiti wa umma wa shughuli za serikali;
(2) Bunge litaundwa na Spika na wabunge wa aina zote zilizotajwa katika ibara ya 64 ya Katiba hii ambao idadi yao haitazidi mia mbili.
60. (1) Kwa mujibu wa ibara ya 59(1) ya Katiba hii, mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo yote ya Shirikisho yatakuwa mikononi mwa 

Bunge;
(2) Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la Tanganyika au la Zanzibar inahusu jambo lolote katika mambo ambayo yako 

chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote 

ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi la Tanganyika au la Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili na itateguka.
(3) Isipokuwa kama imetajwa vinginevyo katika sheria yenyewe sheria yoyote iliyotungwa na bunge kuhusu mambo ya Shirikisho itatumika 

Tanganyika na Zanzibar.
(4) Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na Bunge kwa upande mmoja na Rais kwa upande mwingine kwa mujibu wa masharti ya 

Katiba hii, basi jambo hilo 44
litahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na pande zote kwa mujibu wa madaraka 

yao kuhusu jambo hilo.
61.(1) Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanganyika 

au Zanzibar yasiyo mambo ya Shirikisho, Katiba hii itakuwa na nguvu katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania nzima endapo Katiba ua 

Sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika katiba hii, Katiba hii ndiyo itakuwa na nguvu, na Katiba au Sheria hiyo nyingine, 

kwa kiasi inachokiuka Katiba hii itakuwa batili;
62. (1) Bunge litakuwa ndicho chombo kikuu cha Shirikisho ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri 

Serikali ya Shirikisho na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza:-
(a)kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya Umma na Serikali ya Shirikisho ambayo yako katika wajibu wake;
(b)kujadili na kufanya maamuzi kuhusu utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kufanya maamuzi kuhusu mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali ya Shirikisho, na 

kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d)kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) Kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Shirikisho na ambavyo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.
(f) Kujadili na kuridhia uteuzi wa Rais wa viongozi wa serikali ya Shirikisho waliotajwa katika Katiba hii.
(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii Rais atawajibika kufuata na kutekeleza maamuzi yote ya Bunge.
45
63. (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.
(2) Kwa madhumuni ya Katiba hii maneno “maisha ya Bunge” maana yake ni ule muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge jipya limeitishwa 

kukutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine 

wa kawaida kufanyika.
SEHEMU YA PILI
WABUNGE NA UCHAGUZI WA WABUNGE
WABUNGE
64. (1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani:-
(a)Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania.
(b)Wabunge waliochaguliwa kwa uwiano wa uwakilishi ambao idadi itakuwa nusu na idadi ya Wabunge wa kuchaguliwa katika majimbo ya uchaguzi, 

ilmradi kwamba asilimia hamsini ya hao wawe ni wanawake;
(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi la Tanganyika kutoka miongoni mwa wajumbe wake, ilmradi kwamba hamsini ya hao 

wawe wanawake;
(d)Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar kutoka miongoni mwa wajumbe wake, ilmradi kwamba asilimia hamsini ya 

hao wawe wanawake;
(e)Wabunge wanawake wasiopungua asilimia hamsini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a) waliochaguliwa na vyama vya siasa vilivyoshiriki 

katika uchaguzi mkuu;
(2) Rais na Makamu wa Rais hawakuwa wabunge;
46
65. (1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge 

endapo:-
(a)ni raia wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na nane, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika 

Kiswahili au Kiingereza.
(b)Ni raia safi ambaye hajahukumiwa kwa kosa la uvunjaji wa maadili ya uongozi na ufisadi,.
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge:-
(a)Ikiwa mtu huyo anao au kwa hiari yake amejipatia uraia wa nchi nyingine yoyote; au
(b)Ikiwa kwa mujibu wa Sheria inayotumika katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa 

akili; au
(c) Ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania na kupewa adhabu ya kufungwa gerezani kwa muda 

unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu au maadili;
(d)Ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa 

linloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma.
(e) Ikiwa mtu huyo bado ni mwajiriwa katika nafasi ya afisa mwandamizi katika utumishi wa umma;
(f) Ikiwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa aina yoyote mtu huyo amezuiliwa 

kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa Wabunge.
(3) Ifahamike kuwa mtu aweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge wa kuwakilisha Wilaya ya uchaguzi katika uchaguzi Mkuu wowote ikiwa wakati huo 

yeye amesimama katika
47
uchaguzi wa kugombea kiti cha Rais ilmradi kwamba akichaguliwa kuwa Rais ubunge wake unabatilika;
(4) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka 

yanayohusika na shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguzi wa Wabunge au shughuli za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa 

Wabunge, isipokuwa kwamba Sheria kama hiyo haiwezi kuweka masharti yatakayomzuia Spika wa Bunge asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha 

wilaya ya uchaguzi, wala masharti yatakayosababisha mtu aliyechaguliwa kuwa Spika kupoteza kiti hicho cha Spika au kiti chake cha kawaida 

katika Bunge.
(5) Kwa madhumuni ya ibara hii ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezani ikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewa badala ya 

adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwa sababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwa kulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyo 

hautahesabiwa.
(6) Kwa ajili ya ufafanuzi wa maelezo kuhusu sifa za uchaguzi yaliyomo katika ibara zifuatazo, kila atakapotajwa katika Katiba hii kwamba 

utekelezaji wa jambo lolote wahitaji mtu mwenye sifa za mtu anayestahili kuchaguliwa kama mbunge, basi, isipokuwa kama yahitajika 

vinginevyo, ifahamike kuwa sifa zinazohusika ni zile zinazomwezesha mtu kuchaguliwa kuwa Mbunge kama ilivyoezwa katika ibara ndogo ya (1) 

na (2) ya ibara hii.
66.(1) Kila mbunge atatakiwa, kabla ya kumaliza siku thelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama Mbunge kujiondoa katika shughuli 

zote za kibiashara na ajira zinazoweza kujenga mazingira ya mgongano wa masilahi kwa mujibu wa sheria za nchi;
(2) Kila mbunge atatakiwa, kabla ya kumaliza siku thelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama Mbunge
48
kuwakilisha kwa Spika nakala mbili za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo 

ya (2) ya ibara ya 65.
(3) Tamko rasmi linalotakiwa kuwasilishwa kwa Spika kwa mujibu wa masharti ya ibara hii litatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa 

kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge
67. (1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a)Ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au 

asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(b)Ikiwa jimbo analoliwakilisha limepiga kura ya kutokuwa na imani na Mbunge wake na kumtaka asiendelee kuwa Mbunge wa jimbo hilo na 

kwamba uamuzi huo umeshawasilisha kwa Spika wa Bunge.
(c) Ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma.
(d)Ikiwa ni Mbunge wa uwiano, kama atajiuzulu kuwa mwanachama wa chama kilichomteua;
(e) Iwapo mbunge atachaguliwa kuwa Spika.
(f) Kwa mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 72, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi 

kwa mujibu wa masharti hayo;
(g) Iwapo atafariki dunia;
(h)Iwapo atachaguliwa kuwa Rais;
(i) Iwapo atajiuzulu;
(2) Iwapo halitatokea jambo mojawapo kati ya hayo yaliyotajwa kwenye Ibara ndogo ya (1) ya Ibara hii, Mbunge ataendelea kushika madaraka 

yake kama mbunge mpaka wakati wa uchaguzi mkuu utakaofuata;
49
(3) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti yatakayomwezesha mbunge kukata rufaa, kwa mujibu wa Sheria kupinga hukumu ya 

kuthibitishwa kwake kuwa ni mtu mwenye ugonjwa wa akili au kupinga kupatikana kwake na hatia kwa kosa la aina iliyotajwa kwa mujibu wa 

masharti ya ibara ya 65(2) (c) na (d) ya Katiba hii na Sheria hiyo yaweza kueleza kwamba hiyo hukumu iliyopingwa na huyo mbunge 

haitatiliwa nguvu kisheria mpaka umalizike kwanza muda utakaotajwa katika Sheria hiyo.
68.Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi wa Serikali, madaraka aina iliyotajwa katika ibara ya 65 (2) (e) ataamua:-
(a)Kuwa mgombea uchaguzi wa Rais au Mbunge,
(b)Kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa kinyume na masharti ya ajira, mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma 

tangu tarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombea uongozi katika chama cha siasa.
69.Wabunge wote wa aina zote watalipwa mshahara, posho na malipo mengineyo kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
TUME YA UCHAGUZI
70. (1) Kutakuwa na Tume huru ya Uchaguzi ya Shirikisho ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais, kutokana na majina 

yatakayopendezwa kwake na sekta za jamii husika kama ilivyoagizwa na ibara hii:-
(a) Mjumbe mmoja kutoka kila chama cha Siasa kilichoweka mgombea Urais na chenye wagombea wa ubunge katika angalau majimbo ya uchaguzi 

kumi ya Tanganyika na mawili ya Zanzibar,
(b) Mjumbe mmoja anayewakilisha mashirika na taasisi zisizo za kiserikali zinazoshughulikia uongozi wa jamii;
(c) Mjumbe mmoja anayewakilisha taasisi za kidini za kikristo
50
(d) Mjumbe mmoja anayewakilisha taasisi za kidini za kiislamu
(e) Mjumbe mmoja anayewakilisha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa
(f) Mjumbe mmoja anayewakilisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(g) Mjumbe mmoja anayewakilisha Jeshi la Polisi
(h) Mjumbe mmoja anayewakilisha Wizara ya Fedha
(2) Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho itachagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wake yenyewe na wajumbe wake watakula kiapo cha uaminifu 

mbele ya Rais wa Mahakama ya Rufani kabla ya kuanza utekelezaji wa majukumu yake;
(3) Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho itaajiri sekretariat na watendaji wake na kuendesha shughuli za uchaguzi kwa uhuru bila vitisho wala 

ushawishi wa mtu, taasisi au mamlaka yoyote kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge;
(3) Majina yatakayopendekezwa kwa Rais kama ilivyoelezwa katika ibara ndogo ya (1) (e) hadi (h) yatatokana na watu ambao siyo wanachama wa 

chama chochote cha siasa;
(4) Kila uteuzi utakaofanywa na Rais kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1) sharti uthibitishwe na Bunge.
(5) Wajumbe wa Tume mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka 

sehemu moja ya Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Jamuhuri ya Shirikisho la 

Tanzania na uchaguzi huo uwe umefanyika katika mkutano wa kwanza wa Tume ya Uchaguzi.
(6) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi yaani:-
51
(a)Waziri au Naibu Waziri, Jaji wa Mahakama Kuu, Mahakama ya Shirikisho, mahakama au ya Rufaa au afisa mwandamizi kwenye utumishi wa 

Serikali
(b)Mbunge, mjumbe wa Baraza la wawakilishi au Diwani
(7) Bila ya kuathiri masharti ya ibara hii, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote kati ya mambo 

yafuatayo:-
(a)Ukimaliza muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa, na ieleweke kwamba mjumbe anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kimoja kingine, au
(b)Ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingefanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya 

Shirikisho,
(8) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na 

maradhi, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe na kwamba uamuzi huo utathibishwa na Bunge;
(9) Kila itokeapo kwamba nafsi ya mjumbe wa Tume ya uchaguzi iwazi, basi mjumbe mwingine atateuliwa kulingana na sekta anapotoka kwa 

mujibu wa taratibu zilizowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge;
(10) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho yatakuwa:-
(a)Kusimamia na kuratibu uandikishwaji wa wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,
(b)Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki wa Rais, Wabunge, na Madiwani,
(c) Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge na madiwani,
(d)Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
52
(11) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake, Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho itakuwa ni idara inayojitegemea, na mkuu 

sekretariat yake atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na Tume na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya Sheria iliyotungwa 

na Bunge.
(12) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kuiwezesha Tume kuendesha uchaguzi huru na wa haki 

kila mara unapofanyika uchaguzi wa wananchi nchini Tanzania;
(13) Tume ya Uchaguzi yaweza kutekeleza shughuli zake bila kujali kwamba kuna nafasi miongoni mwa viti vya Wajumbe au kwamba Mjumbe 

mmojawapo hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi kati ya wajumbe wote wa Tume;
(14) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kuwateua maofisa wa Tume wa kusimamia uchaguzi wa 

Madiwani, Wabunge na Rais katika ngazi ya majimbo ya uchaguzi na kwenye vituo vya kupigia kura kwa jinsi ambayo itawapa wananchi na 

wagombea kuwa na imani kuwa uchaguzi unaofanywa na wananchi nchini Tanzania ni huru na wa haki;
(15) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho haitalazimika kufuata amri au 

maagizo ya mtu, taasisi au mamlaka yoyote, ilmradi kwamba Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho italazimika kufuata na kutekeleza amri zote za 

Mahakama Kuu, Mahakama ya Shirikisho na Mahakama ya Rufani;
(16) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho itashauriana mara kwa mara na Tume za 

Uchaguzi ya Tanganyika na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar;
53
(17) Itakuwa ni marufuku watendaji walio kwenye ajira ya Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu 

kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura kwa mujibu wa Katiba hii;
(18) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (16) watendaji watakaokuwa kwenye ajira ya Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho ni :-
(a)Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote walioajiriwa na Tume katika masharti ya kudumu,
(b)Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi waliotajwa kwenye ibara ndogo 70(1) (e) hadi (h),[ibara hii tutaifuta]
(c) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika majimbo ya uchaguzi;
(18) Baada ya kumaliza muda wake katika Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho itakuwa ni marufuku kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kuwa mtumishi wa 

serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar kujihusisha na siasa mpaka muda wa miaka mitano uwe umepita tangu 

kuacha kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
MAJIMBO YA UCHAGUZI
71.(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyo katika ibara hii, Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania itagawanywa katika majimbo ya 

uchaguzi kwa idadi ya wapiga kura na kwa namna itakavyoamuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho, ilmradi kwamba majimbo ya uchaguzi ya 

Zanzibar hayatapungua ishirini na tano;
(2) Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho, itakuwa na mamlaka ya kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi na ikisha kufanya hivyo itawasilisha 

maamuzi yake Bungeni kwa uthibitisho;
(3) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi yaweza mara kwa mara, na angalao kila baada ya miaka kumi, kuchunguza 

mgawanyo wa Jamuhuri ya Shirikisho la 54
Tanzania katika majimbo ya uchaguzi, na yaweza kubadilisha majimbo ya uchaguzi kama matokeo ya uchaguzi huo au kutokana na matokeo ya 

hesabu ya watu wote katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania ili kila mara uwepo uwiano unaoridhisha wa wawakilishi na wapiga kura;
(4) Endapo baada ya uchaguzi kufanywa Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho inafanya mabadiliko katika majimbo ya uchaguzi, basi mabadiliko hayo 

yataanza kutumika wakati Bunge litakapovunjwa tena baada ya kutokea mabadiliko hayo;
UCHAGUZI NA UTEUZI WA WABUNGE
72.(1) Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika katika majimbo yote ya uchaguzi kila mara baada ya Bunge kuvunjwa;
(2) Ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo la uchaguzi kitakuwa ki- wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na 

kuvunjwa kwa Bunge basi mshindi wa pili katika matokeo ya uchaguzi wa Mbunge wa jimbo hilo atatangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mbunge wa 

jimbo hilo.
(3) Bila ya kujali masharti ya ibara hii yaliyotangulia, ifahamike kwamba ikiwa tarehe ya kuvunja Bunge imetangazwa au inafahamika 

kuonekana na matukio yaliyoelezwa katika ibara ndogo ya (3) ya ibara ya 90, basi uchaguzi wa namna hiyo hautafanywa katika kipindi chote 

cha miezi sita ya nyuma ikihesabiwa tangu tarehe hiyo.
73.(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi watachaguliwa na wanachi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na vile vile masharti ya 

Sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba hii inayoweka utaratibu kuhusu uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi;
(2)Kutachaguliwa Mbunge mmoja tu katika jimbo la uchaguzi;
55
(3) Mgombea uchaguzi katika jimbo la uchaguzi atatakiwa atimize masharti yafuatayo:-
(a)awe wamependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa,
(b)awe amepata uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho kuwa mgombea kwa mujibu wa Katiba hii na sheria ya uchaguzi,
(c) Kama ni Mgombea binafsi awe ametimiza masharti ya ugombea binafsi yaliyowekwa na Katiba hii na sheria ya uchaguzi;
74.(1) Kwa madhumuni ya uchaguzi wa Wabunge Wanawake Viti Maalumu na wabunge wa uwiano waliotajwa katika ibara ya 64 (1) (b) na (e) ya 

Katiba hii, vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria ya uchaguzi iliyotungwa na Bunge, 

vitapendekeza kwa Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho listi ya majina ya wateule wanaostahili kuteuliwa kuwa wabunge kwa mujibu wa ibara hiyo 

mapema kabla ya siku ya kupiga kura;
74. (2) mara baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho itakiarifu kila chama kilichoshiriki kwenye uchaguzi 

idadi ya wabunge kinachostahili kupata kwa mujibu wa ibara ya 64 (1) (b) na (e) na pia kuthibitisha kuchaguliwa kwao kuwa waunge kwa 

mujibu wa katiba hii na Sheria ya Uchaguzi;
75. Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na Baraza la wawakilishi la Zanzibar yataweka utaratibu yatakayofuata kwa ajili ya kufanya 

uchaguzi wa Wabunge waliotajwa katika ibara ya 64(1) (c) ya Katiba hii.
76. (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, sheria yaweza kuweka masharti yanayofafanua utaratibu utakaotumiwa na vyama vya 

siasa kupendekeza listi ya majina ya Wabunge wa aina iliyotajwa katika ibara ya 64 (1) (b) ilmradi kwamba jina la kwanza likiwa la jinsia 

moja, jina linalofuata litakuwa la jinsia tofauti;
56
(2) Kwa ufafanuzi wa Ibara ya 64 (1) (e) kuhusu Wabunge wa uwakilishi wa uwiano, Wabunge wa aina hiyo watachaguliwa wakati wa uchaguzi wa 

Rais na Wabunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Bunge.
(3). Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala:-
(a)Kama uchaguzi au uteuzi wa mtu yeyote kuwa Rais ulikuwa halali au sivyo, au
(b)Kama uchaguzi au uteuzi wa mtu yeyote kuwa mbunge ulikuwa halali au sivyo;
litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu ya Shirikisho.
(4) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala kama uchaguzi au uteuzi wa mtu yeyote kuwa Diwani ulikuwa halali au sivyo 

litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu ya Tanganyika au Zanzibar;
(5) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo:-
(a) Jinsi watu wanavyoweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Shirikisho kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwa mujibu wa 

masharti ya ibara hii,
(b) Sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo, utaratibu wa kufungua shauri na masharti yanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri 

kama hilo na,
(c) Kutaja mamlaka ya Mahakama ya Shirikisho juu ya shauri kama hilo na kueleza utaratibu wa kusikiliza shauri lenyewe.
(6).Kutakuwa na haki ya kukata rufaa mbele ya Mahakma ya Rufani ya Shirikisho kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Shirikisho juu ya shauri 

lolote lililosikilizwa kwa ujibu wa masharti ya ibara hii.
(7) Ikiwa shauri lililofunguliwa mbele ya Mahakama Kuu ya Shirikisho linahusu haki iliyolindwa na ibara ndogo ya (3) (a) ya ibara hii, 

shauri hilo lazima limalizike katika muda wa siku
57
14 tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho.
SEHEMU YA TATU
MADARAKA NA HAKI ZA WABUNGE
SPIKA NA NAIBU WA SPIKA
77. (1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuwa Wabunge ambaye atakuwa ndiye 

kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge;
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya ibara 

hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika;
(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla ya kumaliza siku kumi na tano tangu kuchaguliwa kwake, kuwasilisha kwa Rais 

tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 69. Tamko hilo 

litatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge;
(4) Rais atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja ya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo 

ya (3) ya ibara hii;
58
(5) Spika atatakiwa kuwasilisha kwa Rais nakala mbili za taarifa rasmi ya maelezo ya mali ya huyo Spika na, kadri itakavyokuwa, mali ya 

mke au mume wake. Spika atatoa taarifa hiyo kwa kutumia fomu maalum iliyowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge na 

atatoa taarifa ya namna hiyo mara kadri itakavyoagizwa Sheria hiyo;
(6) Masharti ya ibara ya 71 yatatumika pia, kwa kadri itakavyowezekana, kwa taarifa ya mali yoyote itakayotolewa na Spika, kwa mujibu wa 

masharti ya ibara hii;
(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a)Ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi 

wa Spika; au
(b)Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa, lakini masharti haya yatatumika bila 

ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya Katiba hii; au
(c) Ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui 

theluthi mbili ya Wabunge wote; au
(d)Ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii; au
(e) Ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya Kanuni ya Jinai, kuhusu tamko 

rasmi lolote lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii; au
(f) Ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii kabla ya 

kumalizika muda uliowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa Sheria iliotungwa na Bunge;
59
(g) Ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(8) Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge (ispokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha Spika kitakuwa ki wazi;
(9) Mtu yeyote ambaye si Mbunge atakayechaguliwa kuwa Spika, atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake, kuapishwa katika Bunge 

kiapo cha uaminifu;
(10) Spika hatakuwa Mbunge.
78. (1) Kutakuwa na Naibu Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa Wabunge;
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya ibara 

hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu Spika;
(3) Naibu wa Spika, atakoma kuwa Naibu wa Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika, litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a)Ikiwa mtu huyo atakoma kuwa Mbunge; au
(b)Ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo kama asingekuwa Naibu Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za 

uchaguzi wa Naibu Spika; au
(c) Ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu wa Spika kwa azimio la Bunge.
79. (1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge jipya, na katika kikao cha kwanza chochote 

mara baada ya kutokea nafasi katika kiti cha Spika.
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu wa Spika wakati wowote katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya utakaoteuliwa na 60
Bunge na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge mara baada ya kutokea nafasi katika kiti cha Naibu wa Spika.
(3) Uchaguzi wa Spika, na vile vike uchaguzi wa Naibu wa Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa 

na Kanuni za Bunge ili mradi Spika na Naibu Spika watakuwa watu wenye jinsia tofauti na wote wawili hawatatatoka sehemu moja ya Jamuhuri 

ya Shirikisho la Tanzania.
OFISI YA BUNGE
80. (1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Spika kulingana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi Serikalini.
(2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye mtendaji mkuu katika Ofisi ya Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bunge kwa kuzingatia 

masharti ya Katiba hii.
81. (1) Kutakuwa na Sekretariati ya Bunge itakayokuwa na waajiriwa mbalimbali katika utumishi wa serikali kwa idadi itakayoagizwa na Tume 

ya Utumishi Serikalini;
(2) Sekretariati ya Bunge itakuwa na watumishi kwa idadi na ngazi za utumishi itakavyoamuliwa mara kwa mara na Tume ya Utumishi 

inayohusika baada ya kushauriana na Katibu wa Bunge;
(3) Sekretariati ya Bung ifafanya kazi zake chini ya uongozi wa Katibu wa Bunge kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa Bunge na wa 

Wabunge kwa mujibu wa Katiba hii.
UTARATIBU WA SHUGHULI BUNGENI
82. (1) Bunge laweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake;
61
(2) Kanuni za kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli za sekretariati ya 

Bunge na pia utekelezaji wa shughuli za Bunge ndani ya Bunge na zile Kamati za Bunge.
83. (1) Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu katika majimbo yote isipokuwa yale ambako uchaguzi umefutwa ili kufanywa upya, 

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ataitisha na kulihutubia Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu kutangazwa matokeo hayo;
(2) Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa tu kama baada ya kufanya marekebisho yaliyopendekezwa na Wabunge 

kwenye bajeti au mswada wa uliopendekezwa na serikali ambao ni ya msingi katika sera za serikali bado Bunge limekataa kupitisha bajeti au 

mswada huo;
(3) Endapo jambo lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii limetokea basi Uchaguzi Mkuu mpya wa Rais na Wabunge utaitishwa katika 

muda usiozidi miezi mitatu tangu Bunge kuvujwa;
(4) Rais hatalivunja Bunge ikiwa kabla ya mambo yaliyotajwa kwenye ibara ndogo ya (2) ya ibara hii kutokea, tayari Spika aliisha kupokea 

taarifa rasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalum ya Uchuguzi wa Mashtaka Dhidi ya Rais kwa madhumuni ya kumuondoa Rais madarakani 

kwa mujibu wa Katiba hii;
(5) Muda wa maisha ya Bunge ukimalizika Bunge litahesabiwa kuwa limevunjwa: isipokuwa kwamba muda huo ukiisha wakati wowote ambapo Jamhuri 

ya Shirikisho ya Tanzania iko kaktika vita; Bunge laweza mara kwa mara kuongeza muda huo uliotajwa katika ibara ya 65 ya Katiba hii kwa 

muda usiozidi miezi sita mara kwa mara lakini maisha ya Bunge hayawezi kuongezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa muda unaozidi 

miezi kumi na miwili.
62
(6) Kukitokea hali ya hatari ambayo Rais anaona inasababisha kuitisha mkutano wa Bunge na iwapo wakati huo Bunge limevunjwa na matokeo ya 

kura katika majimbo yote hayajatangazwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 83(1) ya katiba hii, basi, Rais aweza kutoa taarifa maalum ya 

kuitisha Bunge na kuagiza kwamba Spika na watu wote waliokuwa wabunge mara tu kabla halijavujwa wahudhurie mkutano huo wa Bunge na watu 

hao pamoja na huyo spika, watahesabiwa kuwa ndio Wajumbe wa Bunge kwa madhumuni ya Mkutano huo na watahesabiwa hivyo mpaka usiku wa manane 

wa siku yatakapotangazwa matokeo ya kura kwenye majimbo yote kwa mujibu wa ibara ya 83 (1) ya Katiba hii.
UTARATIBU WA KUTUNGA SHERIA.
84. (1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kufuata utaratibu wa kujadili na kupitisha Miswada ya Sheria ambayo hatimaye 

itabidi ipate kibali cha Rais;
(2) Muswada hautakuwa sheria mpaka uwe umepitishwa na Bunge na kukubaliwa na Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii;
(3) Baada ya Muswada kuwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, Rais aweza kuukubali au kuukataa, na iwapo Rais atakataa 

Muswada basi ataurudisha kwa Bunge pamoja na maelezo ya sababu zake za kuukataa Muswada huo;
(4) Baada ya Muswada kurudishwa kwa Bunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, hauwezi kupelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali 

chake kabla kumalizika muda wa miezi mitatu tangu uliporudishwa, isipokuwa kama katika hatua ya mwisho kwenye Bunge kabla haujapelekwa 

tena kwa Rais Muswada huo umeungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote;
(5) Iwapo Muswada umerudishwa kwa Bunge na Rais, halafu ukaungwa mkono kwenye Bunge na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya 

Wabunge wote kama 63
ilivyoelezwa katika ibara ndogo ya (3) na kupelekwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake kwa mara ya pili kabla haujamalizika muda wa 

miezi mitatu tangu uliporudishwa, basi Rais atatakiwa kuukubali Muswada huo kabla ya kumalizika muda wa siku ishirini na moja tangu 

Muswada huo ulipowasililishwa kwake la sivyo Muswada huo utakuwa sheria isipokuwa tu kama muswada huo ni wa bajeti itabidi Rais alivunje 

Bunge na masharti ya Ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 83 yatatumika;
(6) Masharti yaliyomo katika ibara hii au katika ibara ya 65 ya Katiba hii hayatalizuia Bunge kutunga Sheria na kuweka masharti ambayo 

yaweza kukabidhi kwa mtu yeyote, chombo chochote au kwa idara yeyote ya Serikali madaraka ya kuweka kanuni zenye nguvu ya kisheria au 

kuzipa nguvu ya kisheria kanuni zozote zilizowekwa na mtu yeyote, chombo chochote au idara yoyote ya Serikali.
MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE
85.(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii ni mamlaka ya Bunge kusimamia na kudhibiti mapato na matumizi ya serikali na 

litafanya hivyo kwa kujadili, kupitisha au kukataa mswada wowote au sehemu ya mswada unaohusu mambo yafuatayo:-
(i) Kutoza kodi au kubadilisha kodi;
(ii) Kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au kubadilisha kiwango hicho;
(iii) Kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa Serikali ya Shirikisho.;
(2) Ifahamike kwamba hakuna kodi mpya itakayotozwa na chombo chochote bila idhini ya Bunge katika mwaka wa Fedha unaohusika.
86. (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote 

katika Jamhuri ya Shirikisho la 64
Tanzania, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge;
(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa kwa kosa la jinai, 

kufunguliwa shauri la madai mahakamani au Bungeni kutokana njambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni 

kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
87. (1) Bunge laweza kujiunda kama Baraza la Taifa la Kutunga Katiba kwa ajili ya kubadilisha masharti ya Katiba hii kwa mujibu wa hati ya 

kukasimu mamlaka hayo iliyotolewa na Baraza la Taifa la Kutunga Katiba;
(2) Bila kujali masharti mengine ya Katiba hii hakutakuwa na mamlaka yoyote yenye uwezo wa kupunguza au kufuta masharti yoyote ya Katiba 

hii yahusuyo Haki za Binadamu;
(3) Katika utekelezaji wa wajibu wake kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, Bunge laweza kupitisha hoja ya mabadiliko makubwa ya 

katiba au kutungwa kwa katiba mpya kwa hoja iliyopitishwa kwa kura za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote;
(4) Iwapo hoja ya kufanya marekebisho makubwa ya Katiba au kutungwa kwa katiba mpya itapitishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (3) ya ibara 

hii, basi Bunge litaweka ratiba ya Tume ya Katiba, Baraza la Taifa la kutunga Katiba na kura ya maoni ya kuthibitisha Katiba.
88. (1) Pamoja na kazi zake nyingine zilizotajwa katika Katiba hii, Bunge litakuwa pia na wajibu wa kuidhinisha uteuzi utakaofanywa na 

Rais kwa vyeo vifuatavyo:-
(a)Waziri Mkuu;
(b)Waziri;
(c) Balozi;
(d)Gavana wa Benki Kuu;
(e) Mwanasheria Mkuu;
65
(f) Mkurugenzi wa Mashtaka;
SURA YA SITA
MAHAKAMA KUU YA SHIRIKISHO
89.(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Shirikisho ambayo itaitwa “Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania” itakayokuwa na mamlaka 

yasiyo na mipaka ya kusikiliza mashauri ya jinai, daawa na upatanishi kwenye mambo ya Shirikisho, kutoa hukumu na amri zenye nguvu ya 

kisheria kuzidi mahakama nyinginezo zilizoko chini yake, kutafsiri Katiba ya Shirikisho, Tanganyika, Zanzibar na sheria za nchi na kufanya 

kila jambo lihusulo utoaji wa haki kwa mujibu mila za kisheria zinazotumika Tanzania ambazo hufanywa na mahakama kuu na kwa mujibu wa 
Katiba na sheria za nchi;
(2) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka utaratibu na masharti ya kupeleka mashauri Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania 

ili idadi kubwa ya mashauri yawasilishwe kwanza mahakama za ngazi ya chini na Mahakama Kuu za Tanganyika na Zanzibar;
(3) Mahakama Kuu za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na mamlaka ya kupokea na kusikiliza mashauri kuhusu mambo ya Shirikisho, ilmradi tu 

kwamba mahakama hizo hazitapokea na kusikiliza mashauri kuhusu tafsiri ya katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, uchaguzi wa Wabunge 

na Rais na uhaini:
(4) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania itakuwa huru na itafanya shughuli na kutekeleza wajibu wake bila kuingiliwa, 

kushinikizwa au kutishwa na mtu, kikundi cha watu, taasisi au Mamlaka yoyoye;
(5) Uteuzi, nidhamu, ajira, mishahara na malupulupu ya majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya
66
Tanzania vimelindwa na kudhaminiwa na Katiba hii na sheria nyingine za Shirikisho;
(6) Majaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho watatoka miongoni mwa majaji wa Mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama Kuu ya Zanzibar, na 

watateuliwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania kwa kushauriana na Jaji Kiongozi wa Tanganyika na Jaji Kiongozi wa Zanzibar 

kutokana na orodha iliyopendekezwa na Tume ya Ajira ya Mahakama ya Shirikisho;
(7) Jaji wa Mahakama ya Shirikisho atatumikia wakati wa uadilifu wake hadi kufikia umri wa miaka sitini na tano na kustaafu kwa masharti 

yaliyowekwa na katiba hii na sheria zinginezo bila muda wake wa utumishi kuongezwa kwa njia yoyote ile;
(8) Ili kutekeleza masharti ya ibara ndogo ya tano ya ibara hii, kipindi cha miaka miwili kabla ya kustaafu kwa Jaji kitatumika kumalizia 

mashauri aliyoanza kuyashughulikia na ni marufuku Jaji anayetarajiwa kustaafu kukabidhiwa mashauri mapya katika kipindi hicho;
MAMLAKA YA MASHAURI YA KATIBA
90. (1) Mbali na mamlaka yake mengine, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania itakuwa na mamlaka ya mwanzo na ya asili 

kusikiliza mashauri yanayotokana na Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, Katiba ya Tanganyika na ya Zanzibar;
(2) Endapo shauri la kikatiba litafunguliwa Mahakama Kuu ya Shirikisho kwa mujibu ibara hii, mahakama hiyo itaitwa “Mahakama Maalumu ya 

Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania” na itakuwa na mamlaka ya kulisikiliza na kutoa uamuzi wa usuluhishi au hukumu yenye nguvu ya 

kisheria juu ya suala lolote linalohusika na tafsiri ya Katiba au sheria za nchi;
67
(3) Pande zenye haki ya kufungua shauri la kikatiba mbele ya Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni:-
(i) Serikali ya Shirikisho;
(ii) Serikali ya Tanganyika;
(iii) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
(iv) Raia wa Tanzania ikiwa ni pamoja ya taasisi zenye uhai wa kisheria ambazo pia ni raia wa Tanzania.
(4) Shauri lolote la kikatiba litakalofunguliwa mbele ya Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania litasikilizwa na 

jopo la majaji watatu;
(5) Jopo la majaji watatu wa Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania litakuwa na angalau jaji mmoja kutoka sehemu 

tofauti ya Shirikisho, ilmradi kwamba ikiwa shauri limeletwa mbele ya mahakama na serikali ya upande mmoja wa shirikisho, basi majaji 

wawili watatoka sehemu iliyoleta shauri mahakamani;
(6) Kila upande kwenye shauri la kikatiba unawajibika kutii na kutekeleza amri za Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la 

Tanzania, isipokuwa kwamba kama upande mmoja umekata rufaa, basi utekeklezaji wa hukumu na amri ya mahakama utasuburi rufani imalizike 

kwanza.
(7) Ieleweke pia kwamba upande wowote katika shauri la kikatiba unaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa 

usuluhishi utakaotolewa na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania iwapo uamuzi huo kama ukitekelezwa utapelekea 

kuvunjwa kwa Katiba hii;
MAMLAKA YA RUFAA
91 (1) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania itakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa kutoka kwenye Mahakama Kuu ya Tanganyika 

na ya Zanzibar kuhusiana na mambo yote ya Shirikisho isipokuwa yale mambo ambayo 68
yenyewe ina mamlaka ya asili na ya pekee ya kusikiliza mashauri yake kwa mara ya kwanza;
(2) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu utaratibu wa kupeleka shauri mbele ya Mahakama Kuu ya Shirikisho na 

uendeshaji wa shauri au kesi ya jinai pamoja na utaratibu wa rufaa kwenda Makama ya Rufani ya Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania, ilmradi 

kwamba sheria yoyote haitatungwa inayoweka vipengele vya kiufundi vinavyodhoofisha au kutwaa haki ya mlalamikaji au mtuhumiwa mbele ya 

sheria.
SURA YA SABA
MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMUHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA
92.(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamuhuri ya Shirikisho ya Tanzania itakayojulikana kwa kifupi kama “Mahakama ya Rufani”, ambayo 

mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii, Katiba za Tanganyika na Zanzibar na sheria nyingine yoyote;
(2) Mahakama ya Rufani itakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufani yoyote kutoka Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania, Mahakama 

Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, Mahakama kuu ya Tanganyika na Mahakama Kuu ya Zanzibar;
(3) Kazi ya Mahakama ya Rufani itakuwa ni kusikiliza na kutoa uamuzi wa mwisho juu ya kila rufaa inayotolewa mbele ya Mahakama ya Rufani 

kutokana na hukumu au uamuzi wa namna nyingine yeyote wa Mahakama za ngazi ya chini yake;
(4) Sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Bunge Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania yaweza kuweka masharti 

yatakayoeleza utaratibu wa kupeleka rufaa mbele ya
69
Mahakama ya Rufani, nyakati na sababu za kukata rufaa na namna Mahakama ya Rufani itakavyoshughulikia rufaa hizo;
93. (1) Kutakuwa na Rais wa Mahakama ya Rufani ambaye katika ibara zifuatazo kwenye Katiba hii atajwa tu kwa kifupi kama ”Rais wa 

Mahakama” na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani wasiopungua sita, ambao angalau wawili watatoka Zanzibar;
(2) Kikao cha Mahakama ya Rufani kitaundwa na jopo la majaji watatu, kikao kamili kitaundwa na jopo la majaji watano na Kikao Maalumu 

kitaundwa na jopo la majaji saba.
(3) Rais wa Mahakama atachaguliwa na Baraza la Uchaguzi wa Rais wa Mahakama litakaloundwa na majaji wote wa Mahakama ya Rufani, Mahakama 

Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, Mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama Kuu ya Zanzibar;
(4) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania laweza kutunga sheria itakayoweka utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Mahakama na masharti ya 

utumishi wake;
(5) Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania itakuwa na mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa Rais wa Mahakama kwa 

mujibu wa Katiba hii na sheria itakayotungwa kwa ajili hiyo:
(6) Rais wa Mahakama atachaguliwa kutoka miongoni mwa majaji wa Mahakama ya Rufani na atakuwa ndiye Kiongozi wa Mahakama Tanzania kwa 

kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa kwa kipindi kingine kimoja:
(7) Majaji wengineo wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais wa Mahakama, baada ya kushauriana Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho ya 

Tanzania kutoka miongoni mwa majaji wa Mahakama Kuu au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu
70
waliopendekezwa na Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Shirikisho;
(8) Iwapo itatokea kwamba:-
(a)Kiti cha Rais wa Mahakama ki- wazi; au
(b)Rais wa Mahakama hayupo Tanzania; au
(c) Rais wa Mahakama ameshindwa kutekeleza kazi yake kwa sababu yoyote ile, basi Jaji Rufani aliyeteuliwa kwanza kwenye cheo hicho 

atashika nafasi ya Kaimu Rais wa Mahakama na huyo Kaimu Rais wa Mahakama atatekeleza kazi za Rais wa Mahakama mpaka atakapoteuliwa Rais wa 

Mahakama mwingine na kushika madaraka ya kiti cha Rais wa Mhakama au mpaka Rais wa Mahakama mwenyewe ambaye alikuwa hayupo Tanzania 

atakaporejea kazini.
(9) Ikitokea kwamba kiti cha jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani kiwazi au ikiwa Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani atateuliwa kuwa Kaimu 

Rais wa Mahakama au atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote ile, au kama Rais wa Mahakama atashauriwa na Msajili wa Mahakama ya 

Rufani kuwa kazi za Mahakama ya Rufani zilivyo wakati huo zahitaji ateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani, basi Rais wa Mahakama aweza, 

baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumteua Jaji wa Mahakama ya Rufani au Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa watu 

waliopendekezwa na na Tume Kuajiri ya Mahakama ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya 

Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (7) ya ibara hii;
(10) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii, ataendelea 

kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani muda wowote utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake, au, kama muda haukutajwa, mpaka 

uteuzi wake utakapofutwa na Rais wa Mahakama, lakini bila ya kujali kwamba muda wake wa kazi umemalizika au kwamba
71
uteuzi wake umefutwa, mtu huyo aweza kuendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani mpaka akamilishe shughuli nyingine 

yoyote inayohusika na rufaa au mashauri mengine yoyote ambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla ya uteuzi wake haujafutwa;
(11) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 105 ya Katiba hii (inayotaja idadi ya 

Majaji wa Mahakama ya Rufani) na masharti ya ibara ya 112 ya Katiba hii (inayoeleza mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani), inatamkwa 

rasmi kwamba Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (9) ya ibara hii, atakuwa na mamlaka 

kamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na kwamba atatekeleza kazi zake kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(12) Kazi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani haitafutwa wakati yupo mtu aliyeshika madaraka ya kiti cha Jaji wa Mahakama ya Rufani.
94.Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri lolote katika Mahakama ya ngazi iliyo chini ya mahakama ya 

Rufani.
95.(1) Kila Jaji wa Mahakama ya Rufani atatumikia wakati wa uadilifu wake hadi kufikia umri wa miaka sitini na tano ambapo atastaafu kwa 

hiari yake mwenyewe, au umri wa miaka sabini ambapo atastaafu kwa lazima kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba hii bila uwezekano 

wa muda wake wa utumishi kuongezwa kwa njia yoyote ile;
(2) Ili kutekeleza masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, kipindi cha miaka mitatu kabla ya kustaafu kwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa 

kitatumika kumalizia mashauri aliyoanza kuyashughulikia na ni marufuku Jaji Rufani anayetarajiwa kustaafu kukabidhiwa mashauri mapya 

katika kipindi hicho;
72
96.Jaji wa Mahakama ya Rufani hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapishwa kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika 

na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
97.Jaji wa Mahakama ya Rufani hatateuliwa kushika nafasi yoyote katika Serikali au Bunge.
98.(1) Katika kila rufaa suala linalohitaji uamuzi wa Mahakama ya Rufani litaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa 

Mahakama ya Rufani waliosikiliza rufaa;
(2) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani aweza kutekeleza madaraka yoyote ya Mahakama ya Rufani ambayo nahusu kutoa uamuzi wa mwisho juu ya 

Rufaa, isipokuwa kwamba:-
(a) Katika rufaa yoyote iwapo Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeombwa kutekeleza madaraka hayo atatoa uamuzi ambao mwombaji haridhiki nao, 

basi atakuwa na haki kutaka rufaa yake ifanyiwe marejeo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ambao watakuwa na mamlaka ya mwisho 

ya kuthibitisha, kubatilisha au kubadilisha amri, agizo au uamuzi wa namna nyingine wowote uliotolewa na jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani 

kwa mujibu wa masharti ya ibara hii,
(b)Katika rufaa yoyote iwapo jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani limetekeleza madaraka ya kutoa uamuzi ambao mwombaji haridhiki 

nao, basi atakuwa na haki kutaka rufaa yake ifanyiwe marejeo na jopo la majaji watano wa Mahakama ya Rufani ambao watakuwa na mamlaka ya 

mwisho ya kuthibitisha, kubatilisha au kubadilisha amri, agizo au uamuzi wa namna nyingine wowote uliotolewa na majaji watatu wa Mahakama 

ya Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara hii;
(2) Kwa mujibu wa Ibara 95(1) ya katiba hii, Jaji wa Mahakama ya Rufani aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya 

kushindwa kutekeleza kazi yake kutokana na maradhi au kwa sababu ya tabia mbaya
73
inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji, Sheria ya maadili ya viongozi wa umma, au kanuni za maadili za majaji na ataondolewa kazini kwa 

mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii;
(3) Iwapo Rais wa Mahakama kwa kushauriana na Jaji Mkuu baada ya kupata taarifa ya maandishi ya Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Shirikisho 

ataona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazini linahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:-
(a) Rais wa Mahakama atateua Tume ya Majaji watatu wa Mahakama Rufani kutoka katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais wa Mahakama na itamshauri kama huyo Jaji anayechunguzwa aondolewe 

kazini au aadhibiwe kwa namna nyingine yoyote kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii;
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais wa Mahakama kwamba Jaji ambaye habari zake 

zimechunguzwa ana hatia, basi atamwondoa kazini Jaji huyo;
(5) Ikiwa suala la kumuondoa Jaji kazini limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya 

ibara hii, Rais wa Mahakama atamsimamisha kazi Jaji huyo anayehusika hadi uchunguzi utakapokamilika na uamuzi kuchukuliwa ama kumwondoa 

kazini au kutomwondoa kazini;
(6) Ikiwa tuhuma zilizotajwa kwenye ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii zinamhusu Rais wa Mahakama, basi masharti ya ibara ndogo ya (3), (4) 

na (5) ya ibara hii yatatekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania;
TUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA SHIRIKISHO
74
99.(1) Kutakuwa na Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Shirikisho ambayo itakuwa na mamlaka ya kuajiri watumishi wote wa mahakama za Jamhuri ya 

Shirikisho ya Tanzania na pia mamlaka ya kupendekeza majina ya watu wanaostahili kuteuliwa kushika nafasi ya jaji wa Mahakama Kuu ya 

Shirikisho na Mahakama ya Rufani ya Shirikisho;
(2) Wajumbe wa Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Shirikisho watakuwa kama wafuatao:-
(a)Mwenyekiti wa Tume ambaye atakuwa mtu mwenye sifa ya kuteuliwa kuwa Jaji Rufaa wa Mahakama ya Rufaa ya Shirikisho;
(b)Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ambaye atateuliwa kwa ajili hiyo na Rais wa Mahakama;
(c) Jaji mmoja wa Mahakama Kuu ya Shirikisho ambaye atateuliwa na Jaji Mkuu;
(d)Majaji Wakuu wa Mahakama Kuu za Zanzibar na Tanganyika;
(e) Marais wa Chama cha Mawakili cha Tangantika na cha Zanzibar;
(f) Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria ya Shirikisho;
(3) Mtu hataweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Shirikisho ikiwa mtu huyo ni Mbunge.
100.(1) Pamoja na madaraka yake mengine, Tume itakuwa na madaraka ya kupendekeza kwa Rais Jaji Mkuu na Rais wa Mahakama majina ya watu 

wenye sifa za kuteeuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho na Mahakama ya Rufaa;
(2) Tume itakuwa na madaraka ya kuajiri na kudhibiti nidhamu na kushughulikia maendeleo ya watumishi wa idara ya Mahakama ambao siyo 

majaji;
75
(3) Tume itashughulika na mambo yote yanayohusu mshahara, marupurupu na malipo mengine ya majaji katika Mahakama Kuu ya Shirikisho na 

Mahakama ya Rufaa.
SURA YA NANE
VYOMBO VYA DOLA VYA TANGANYIKA,
NA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA TANGANYIKA NA YA ZANZIBAR
101.(1) Kutakuwa na Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka katika Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote 

yasiyo ya Shirikisho kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaundwa na kutatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Tanganyika na 

Zanzibar;
(3) Kiongozi Mkuu wa wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Zanzibar ataitwa Gavana wa Tanganyika na Gavana wa 

Zanzibar;
(4) Kutakuwa na kiapo rasmi cha Gavana wa Tanganyika na cha Gavana wa Zanzibar kitakachosimamiwa na Jaji Mkuu wa Tanganyika na Jaji Mkuu 

wa Zanzibar ambapo viongozi wote wawili wataapa kuitii, kuilinda na kuitetea Katiba hii, kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamuhuri ya 

Shirikisho la Tanzania, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar.
76
102. (1) Magavana wa Tanganyika na Zanzibar watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
(2) Serikali za Mitaa na Halmashauri zake zitaundwa katika kila wilaya kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
(3) Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na la Zanzibar laweza kutunga sheria kuweka taratibu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa na 

Halmashauri zake, ilmradi mambo kuhusu muundo wa Halmashauri na wa Serikali za Mitaa na pia utawala na matumizi ya ruzuku kutoka serikali 

ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania yatatawaliwa na Katiba hii na sheria za Shirikisho;
SEHEMU YA PILI
MABARAZA YA WAWAKILISHI
103. (1) Kutakuwa na mabaraza mawili ya wawakilishi, moja la Tanganyika na jingine la Zanzibar ambayo yatakuwa na mamlaka ya kutunga 

sheria kuhusu mambo yasiyo ya Shirikisho, kujadili, kusimamia na kudhibiti shughuli za Serikali za Tanganyika na Zanzibar;
(2) Mabaraza ya wawakilishi yatakuwa na wajumbe wanaolingana na idadi ya majimbo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume za Uchaguzi za 

Tanganyika na Zanzibar;
(3) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar, ilmradi kutakuwa na aina 

zifuatazo za wajumbe wa Baraza yaani:-
(a)Wajumbe waliochauguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi,
(b)Wajumbe waliochaguliwa kwa uwiano wa uwakilishi ambao idadi yake haitazidi nusu ya wajumbe
77
waliochaguliwa kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi na asilimia thelathini ya hawa wawe ni wanawake;
(c) Wajumbe wanawake wasiopungua asilimia thelathini ya jumla ya wajumbe wa kuchaguliwa kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi;
(3) Magavana wa Tanganyika na Zanzibar hawatakuwa sehemu ya Mabaraza ya Wawakilishi ila watakuwa na wajibu wa kuweka saini kukubali au 

kukataa mazimio ya miswada ya sheria iliyopitishwa na mabaraza hayo kwa mujibu wa Katiba za majimbo hayo;
(4) Mamlaka na shughuli za Mabaraza ya Wawakilishi zitatawaliwa na Katiba ya Tanganyika na ya Zanzibar,Sheria na Kanuni zilizotungwa na 

Mabaraza hayo.
SEHEMU YA TATU
MAHAKAMA KUU ZA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
MAMLAKA NA UHURU
104.(1) Kuatakuwa na Mahakama Kuu ya Tanganyika ambayo itaundwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika.
(2) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo itaundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
(3) Mahakama Kuu za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri, kutoa hukumu na amri zenye nguvu za kisheria, kutoa 

tafsiri ya sheria za Tanganyika na Zanzibar kwenye mambo yasiyo ya Shirikisho na kufanya kila jambo lihusulo utoaji wa haki kwa mujibu wa 

Katiba hii, Katiba za Tanganyika na Zanzibar na sheria za nchi na pia zitakuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayotokana na mambo ya 

Shirikisho kama itakavyoagizwa na katiba hii na sheria zilizotungwa na Bunge;
78
(4) Rufaa kuhusu mashauri yatokanayo na mambo yasiyo ya Shirikisho zitapelekwa Mahakama ya Rufaa ya Shirikisho na rufaa zitokanazo na 

mambo ya Shirikisho zitapelekwa Mahakama Kuu ya Shirikisho;
(5) Mahakama Kuu za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa huru na zitafanya shughuli na kutekeleza wajibu wake bila kuingiliwa, kushinikizwa au 

kutishwa na mtu, kikundi cha watu, taasisi au Mamlaka yoyoye;
(6) Uteuzi, nidhamu, ajira, mishahara na malupulupu ya majaji wa Mahakama Kuu za Tanganyika na Zanzibar vimelindwa na kudhaminiwa na 

Katiba hii na Katiba za Tanganyika na Zanzibar.
(7) Katiba na sheria za Tanganyika na Zanzibar zinaweza kuunda Mahakama au Mabaraza ya utoaji wa haki kulingana na mahitaji ya huduma za 

utoaji haki kwa wananchi, ilmradi kwamba Mahakama na Mabaraza hayo yawajibike kwa Mahakama Kuu na yatii na kuheshimu Katiba hii, Katiba za 

Tanganyika na Zanzibar na sheria za Shirikisho.
(8) Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar zitaweka utaratibu unaofanana na utaratibu uliowekwa katika Katiba hii kuhusu suala la Jaji 

na Mahakama Kuu kuondolewa katika madaraka yake.
HATI ZA AMRI ZA MAHAKAMA
104. (1) Hati za amri za Mahakama za Tanzania katika mashauri ya madai na ya jinai zaweza kupelekwa mahali popote nchini Tanzania na 

maagizo hayo yaweza kutekelezwa mahali popote nchini Tanzania kwa kufuata masharti yafuatayo:-
a. Iwapo Mahakama imetoa amri ambayo utekelezaji wake utafanyika kwenye eneo ambalo mahakama hiyo haina mamlaka, basi amri hiyo 

itatekelezwa na Mahakama yenye mamlaka huko ilikopelekwa hati; na
79
b. Iwapo sheria inayotumika huko ilikopelekwa hati imeweka masharti kwamba hati zilizotolewa na Mahakama ya mahali pengine ni lazima 

ithibitishwe kwanza na Mahakama yenye mamlaka mahali hapo inapotumika Sheria hiyo, basi kila hati iliyotolewa na Mahkama ya mahali pengine 

itabidi ithibishwe kwanza kwa mujibu wa sheria hiyo kabla maagizo yaliyomo katika hati hiyo hayajatekelezwa.
(2) Iwapo mtu amekamatwa mahali popote nchini Tanzania kwa mujibu wa hati ya kuamuru kukamatwa kwake iliyotolewa na mahakama iliyoko 

mahali pengine nchini Tanzania, basi mtu huyo atahesabiwa kuwa yuko chini ya ulinzi halali na atasafirishwa kupelekwa mbele mbele ya 

Mahakama iliyotoa hati hiyo;
(3) Masharti yaliyomo katika ibara hii hayatazuia Sheria kuweka utaratibu kwa ajili ya kupeleka nje ya Tanzania hati zilizotolewa na 

Mahakama za Tanzania kwa ajili ya kukidhi hukumu na masharti mengineyo ya sheria;
SURA YA TISA
SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
105.(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa 

umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya katiba hii na sheria ya maadili ya Vongozi wa umma yanazingatiwa ipasavyo;
(2) Kwa madhumuni ya ibara hii, maana ya kiongozi wa umma na masharti ya maadili ya viongozi wa umma itabidi vifasiriwe kwa mujibu wa 

masharti ya Katiba hii kuhusu Maadili ya Taifa, masharti ya Katiba hii kuhusu sifa za viongozi wa umma na masharti ya sheria ya maadili ya 

Viongozi wa Umma au masharti ya sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge;
80
(3) Sekretarieti ya Maadili itakuwa na Kamishna wa Maadili na wafanyakazi wengine ambao idadi yao itatajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.
(4) Bunge litatunga Sheria itakayoainisha misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma itakavyozingatiwa na watu wote wanaoshika nafasi za 

madaraka zitazotajwa na Bunge.
(5) Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma:-
(a)Itafafanua nafasi za madaraka ambazo watu wenye kushika nafasi hizo watahusika nayo;
(b)Itawataka watu wanaoshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmi kuhusu mapato, rasilimali na madeni yao;
(c) Itaelekeza taratibu, madaraka na desturi zitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji wa maadili;
(d)Itapiga marufuku rushwa katika shughuli za umma;
(e) Itapiga marufuku mienendo na tabia inayopelekea kiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea au inahatarisha maslahi ya ustawi wa 

jamii;
(f) Itafafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa kuvunja misingi ya Maadili.
(g) Itaweka masharti mengine yoyote yayofaa au ambayo ni muhimu kwa madhumuni ya kukuza na kudumisha uaminifu, uwazi, kutopendelea na 

uadilifu katika shughuli za umma na kwa ajili ya kulinda fedha na mali nyinginezo za umma.
(6) Bunge laweza kwa sheria kuweka masharti ya mtu kufukuzwa au kuondolewa kazini kutokana na kuvunja maadili ya viongozi, bila ya kujali 

kama kazi hiyo ni ya kuchaguliwa au kuteuliwa.
SURA YA TISA
MASHARTI KUHUSU FEDHA
81
SEHEMU YA KWANZA
MFUKO MKUU WA HAZINA
106.(1) Fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbali zitawekwa katika mfuko maalum ambao utaitwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya 

Shirikisho.
(2) Fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na Sheria kwamba zitumike kwa shughuli 

maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum.
MGAWANYO WA MAPATO
107. Serikali ya Shirikisho itatunza akaunti mbili maalum yaani “akaunti ya Fedha ya Shirikisho” ambayo itakuwa ni sehemu ya Mfuko Mkuu wa 

Hazina ya serikali ya Shirikisho, ambamo kutawekwa fedha yote ambayo ni mgawo kwa matumizi ya Shirikisho na ‘akaunti ya fedha za 

Tanganyika na Zanzibar’ ambayo itakuwa pia sehemu ya Mfuko Mkuu wa Serikali ya Shirikisho ambamo itawekwa fedha yote ambayo ni mgawo wa 

Serikali za Tanganyika na Zanzibar, ikitaja wazi mgawo wa kila serikali;
108. (1) Kutakuwa na Tume ya Pamoja ya Fedha yenye wajumbe wasiozidi saba angalau watatu toka Zanzibar na wane kutoka Tanganyika na ambao 

watateuliwa na Rais kwa ushauriano na Gavana wa Tanganyika na gavana wa Zanzibar kwa mujibu wa ibara hii na masharti ya sheria iliyotungwa 

na Bunge;
(2) Majukumu ya Tume ya Fedha yatakuwa ni:-
(a)Kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Shirikisho.
(b)Kuamua mgawo toka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa Serikali tatu, kwa kuzingatia vianzo vya mapato na mahitaji.
(c) Kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha ya Shirikisho na pia uhusiano katika mambo ya kifedha ya Serikali tatu.
82
(d)Kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipaita Tume au kama Rais atakavyoagiza, na kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
SEHEMU YA TATU
MASHARTI YA KUTOA FEDHA
109.(1) Fedha hazitatolewa kutoka akaunti ya fedha ya Shirikisho kwa ajili ya matumizi ila kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au Sheria 

nyingine yoyote,
(2) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa serikali, ukuiachilia mbali Mfuko wa Hazina ya Serikali, hazitatolewa kutoka mfuko huo 

kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yawe yameidhinishwa na katiba hii au Sheria nyingine yoyote;
(3) Fedha zilizomo katika akaunti ya Fedha ya Shirikisho hazitatolewa kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yawe yaneidhinishwa na 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali na pia kwa sharti kwamba fedha hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa 

ajili hiyo kwa mujibu waSheria iliyotungwa na Bunge.
110.(1) Rais atatoa maagizo kwa Waziri mwenye dhamana ya mambo ya fedha atengeneze na kuwasilisha kwenye Bunge katika kila mwaka wa fedha 

wa serikali, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali ya Shirikisho kwa ajili ya kipindi cha mwaka wa fedha unaofuata.
(2) Baada ya Bunge kuyakubali Makadirio ya Matumizi kutawasilisha kwenye Bunge muswada ambao utaitwa Muswada wa Sheria ya Matumizi ya 

Fedha za Serikali, kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha, na fedha hizo zitakazotolewa kulipa gharama za shughuli mbali mbali za 

Serikali zinazohusika na Makadirio hayo.
83
(3) Ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekana kwamba:-
(a)Fedha za matumizi zilizoidhinishwa na Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya shughuli fulani hazitoshi au kwamba imekuwa 

lazima kulipwa gharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu wa sheria, au
(b)Kuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli fulani kwa kiasi kinachozidi kiwango cha matumizi yaliyoidhinishwa na sheria ya 

Matumizi ya Fedha za serikali kuhusu shughuli hiyo au kwamba fedha zimetumiwa kulipia gharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za 

matumizi kwa mujibu wa Sheria, kutawasilishwa kwenye Bunge Makadirio ya Matumizi ya Nyongeza au, kadri itakavyokuwa, maelezo ya Matumizi 

ya Ziada, na baada ya Bunge kuyakubali hayo Makadirio ya Matumizi ya Nyongeza au Maelezo ya matumizi ya ziada, kutawasilishwa kwenye Bunge 

Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka akaunti ya Fedha za Shirikisho na 

fedha hizo zitatumiwa kulipia gharama za shughuli zinazohusika na hayo Makaddirio au maelezo.
MAMLAKA YA KUTOZA KODI
111.(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa idhini na Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wa utaratibu 

uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu ya kisheria na sheria iliyotungwa na Bunge.
(2) Masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) y ibara hii hayatalizuia Baraza la Wawakilishi la Tanganyika au Zanzibar kutumia mamlaka 

yake ya kutoza kodi ya aina yoyote kwa mujibu wa madaraka ya Baraza hilo yliyoainishwa na Katiba za Tanganyika na Zanzibar.
112.(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo:-
84
(a) Kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka akaunti ya Fedha ya Shirikisho;
(b) Kuanzisha mfuko wa Matumizi ya Dharura na kumwezesha Rais au Waziri aliyeteuliwa na Rais kwa ajili hiyo kuazima fedha kutoka mfuko huo 

kulipia gharama za jambo la haraka na la dharura ambalo halikutazamiwa kutokea na ambalo halikupangiwa fedha zozote za matumizi;
(c) Kumwezesha Rais au Waziri aliyeteuliwa na Rais kwa ajili hiyo kutumia fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani kulipia 

gharama za jambo la haraka na la dharura kama ilivyoelezwa katika aya ya (a) ya ibara hii ndogo;
(2) Iwapo fedha zimeazima kutoka Mfuko wa Matumizi ya Dharura au fedha zilitengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani zimetumiwa kulipia 

gharama za jambo la haraka na la dharura, basi kutawasilishwa kwenye Bunge la Makadirio ya Matumizi ya Nyongeza, na baada ya Bunge 

kuyakubali Makadirio hayo Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali utakaowasilishwa kwenye bunge kwa ajili ya kuidhinisha 

matumizi hayo ya nyongeza utahakikisha kwamba fedha zozote zilizoazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya Dharura zitarudishwa kwenye Mfuko huo 

kutokana na fedha za matumizi yatakayoidhinishwa na Muswada huo.
113. (1) Deni la Taifa litadhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Fedha za Shirikisho;
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara hii deni la Taifa maana yake ni deni lenyewe na pia riba inayolipwa juu ya deni hilo, na gharama 

zote zinazoambatana na usimamizi wa deni hilo.
114.(1) Watumishi wa Serikali ambao mishahara, posho, malupulupu na pensheni zao vimedhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Shirikisho watalipwa 

kutokana na mfuko huu bila malipo hayo kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya mjadala na idhini ya
85
Bunge kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria iliyotungwa na Bunge;
(2) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya ibara hii pamoja na masharti yake ya kazi havitabadilishwa, baada 

ya mtumishi huyo kuteuliwa, kwa jinsi ambayo itapunguza maslahi ya utumishi huyo.
(3) Iwapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya ibara hii ana hiari ya kuchagua kima cha mshahara au aina ya kazi, basi kwa 

madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo hii, mshahara wa kima hicho atakaochagua vitahesabiwa kuwa vina maslahi zaidi kwake 

kuliko kima cha mshahara kingine chochote angalichoweza kuchagua au aina ya masharti ya kazi nyingine yoyote aliyoweza kuchagua;
(4) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa 

Hesabu za Serikali wa Shirikisho na Gavana wa Benkiki Kuu ya Shirikisho.
115.(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Shirikisho.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na jukumu juu ya mambo yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka akaunti ya Fedha ya Shirikisho matumizi yake yameidhinishwa na kwamba 

zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinishwa fedha 

hizo zitolewe,
(b) Kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa yatatokana na fedha zilizomo katika akaunti ya Fedha ya Shirikisho 

au fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na Sheria iliyotungwa na Bunge, na ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli
86
zilizohusika na matumizi ya fedha hizo zimetolewa kwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Sheria,
(c) Angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya 

Shirikisho hesabu zinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali ya Shirikisho na hesabu za Mahakama za Rufani na Mahakama ya Shirikisho na 

hesabu zinazosimamiwa na Katibu wa Bunge;
(3) Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu na kila mtumishi wa serikali aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na haki ya 

kuchunguza vitabu, kumbukumbu, hati za maelezo, taarifa na hati nyinginezo zote zinahusika na hesabu za aina yoyote iliyotajwa katika 

ibara ndogo ya (2) ya ibara hii na Bunge laweza kutunga shria inayoweka masharti na kutoa adhabu kwa watumishi wa serikali watakaoshindwa 

kuwajibika na kutoa taarifa sahihi za matumizi ya fedha za serikali kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali;
(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha Bungeni taarifa ya ukaguzi aliofanya kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya 

ibara hii na pia kuwasilisha nakala yake kwa Rais;
(5) Baada ya kupokea taarifa hiyo Bunge litaijadili taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea 

nakala ya taarifa hiyo na iwapo Rais hajachukua hatua za kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bunge 

laweza kupitisha azimio litakalowasilishwa serikalini kwa utekelezaji kuhusiana na mapendekezo hayo;
(6) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa pia na jukumu la kutekeleza kazi ns shughuli nyingine, na atakuwa na madaraka mengine ya 

namna mbalimbali, kama itakavyoelekeza na sheria kuhusu hesabu za serikali ya
87
Shirikisho au hesabu za vyombo vya Umma au hesabu za mashirika.
(7) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa 

hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine au yeyote, idara yoyote ya serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo 

hayataizuia mahakama kutum ia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu ametekeleza madaraka yake kwa 

mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.
116.(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Shirikisho atalazimika kuacha 

kazi atakapotimiza umri wa miaka sitini na tano au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge;
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu kushindwa kutekeleza kazi zake, 

kutokana na maradhi au sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya viongozi wa umma na hataweza kuondolewa 

kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya 4 ya ibara hii;
(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji 

kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:-
(a) Rais atateua Tume maalum yenye wajumbe watatu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa mahakama kuu au Mahakama ya Rufaa 

katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuia ya Madola.
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti 

na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
88
maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya;
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu 

aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi 

Rais atamwondoa kazini;
(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa 

masharti ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuata uamuzi 

huo wa kumsimamisha kazi na Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini;
(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au 

kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika au serikali ya Zanzibar;
(7) Masharti ya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyote aliyeteuliwa kuwa kaimu Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu.
SURA YA KUMI
MADARAKA YA UMMA
117.(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Katiba hii, kutakuwa na vyombo vya serikali za mitaa katika kila wilaya na miji na katika 

Jamuhuri ya Muungano, ambavyo vitakuwa vya aina na majina yatakavyowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi na Tanganyika na 

la Zanzibar;
89
(2) Baraza la Wawakilishi, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya serikali za mitaa, miundo na wajumbe wake, 

njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo;
(3) Madhumuni ya kuwapo serikali ya mitaa ni madaraka kuwa mikononi mwa wananchi kwa hiyo vyombo vya serikali za mitaa vitaundwa na 

wananchi na vitakuwa na haki na mamlaka ya kupanga mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa 

jumla;
(4) Shughuli na utaratibu wote wa uchaguzi wa serikali za mitaa zitafanywa na Tume ya Uchaguzi ya Serikali ya Tanganyika na Tume ya 

Uchaguzi ya Serikali ya Zanzibar;
(5) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, kila chombo cha serikali za mitaa, kwa kuzingatia 

masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo:-
(a) Kutekeleza kazi za serikali za Mitaa katika eneo lake.
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi.
(c) Kuimarisha demokrasia katika eneo lake na kuitumia demokrasia kuharakisha maendeleo ya wananchi.
SURA YA KUMI NA MOJA
MAJESHI YA ULINZI
118.(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote, au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho ya 

Tanzania kuunda au kuweka Tanzania Jeshi la aina yoyote;
(2) Serikali ya Shirikisho yaweza, kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya 

ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania;
90
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba atakuwa na haki ya kupiga kura 

kuchagua viongovi kwa mujibu wa masharti ya katiba hii na Sheria ya Uchaguzi;
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, mwanajeshi maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, 

Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Usalama wa Taifa na vikosi vingine vinavyoweza kuundwa kwa amri ya 

Rais na kuthibitishwa na Bunge, ili kutekeleza majukumu maalumu.
119.(1) Rais ni Amiri Jeshi Mkuu na anayo mamlaka ya kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamuhuri 

ya Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali za watu katika hali ya hatari, ajali au majanga na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu 

ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo;
(2).Katika utendaji wa majukumu yake kma Amiri Jeshi Mkuu, Rais aweza kuyaamuru majeshi hayo yatekeleze majukumu yake ndani au nje ya 

Tanzania, ilmradi kwamba atatekeleza taratibu za kupata kibali cha Bunge kwa mujibu wa Katiba hii na sheriia iliyotungwa na Bunge kwa 

ajili hiyo;
(3) Madaraka ya mambo yafuatayo yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu kwa kushauriana na Tume ya Taifa ya Ulinzi na Usalama, yaani:-
(a) Madaraka ya kuteua viongozi katika majeshi ya ulinzi na usalama ya Shirikisho;
(b) Madaraka ya kuajiri na madaraka ya kuwaondoa jeshini wanajeshi;
(3) Madaraka ya kuwateua wanajeshi kwa hati maalumu za uaminifu kwake na kwa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania kuongoza vikosi mbali mbali 

vya Majeshi ya ulinzi na Usalama;
91
(4) Jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kinyume cha amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya 

(1) na (2) ya ibara hii litakuwa batili.
SURA YA KUMI NA MBILI
MAMLAKA YA KUTUNGA KATIBA
SEHEMU YA KWANZA
MKUTANO WA KATIBA
120.(1) Mamlaka yote ya kutunga katiba ni ya wananchi na kwa pamoja wananchi ndio chimbuko la katiba na mamlaka ya nchi;
(2) Katika kutekeleza msingi uliotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, Mkutano Mkuu wa Taifa wa Kutunga Katiba ndicho chombo kikuu 

cha wananchi wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania cha kutunga katiba;
(3) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Katiba watachaguliwa na sekta mbalimbali za umma wa Watanzania , yaani:-
(a) Wawakilishi kumi kutoka kila chama cha siasa kilichosajiliwa;
(b) Wawakilishi kumi kutoka madhehebu makuu ya wakristo na waislamu;
(c ) Wawakilishi kumi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya raia wa Tanzania;
(d) Wawakilishi kumi wa vyama vya wafanyakazi;
(e) Wawakilishi kumi wa vyama vya wakulima;
(f) Wawakilishi kumi wa vyama vya wanafunzi wa vyuo vikuu
(g) Wawakilishi kumi wa vijana
92
(h) wawakilishi kumi wa wanawake
(i) Wawakilishi kumi wa vyama vya waajiri
(j) Wawakilishi kumi wa vyama vya wasiojiweza
(k) Wawakilishi kumi wa vyama vya wafanyabiashara;
(l) Spika na Wabunge wa Shirikisho
(m) Rais, Makamu wa Rais na Baraza la Mawaziri wa Shirikisho;
(n) Majaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho, Tanganyika, Zanzibar na Mahakama ya Rufani;
(o) Gavana wa Tanganyika, Zanzibar na Mabaraza ya Mawaziri wa Tanganyika na Zanzibar;
(p) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na Zanzibar;
(r) Wajumbe 10 wanaowakilisha wasanii;
(s) Wajumbe 10 wanowakilisha vyama vya michezo.
(4) Wajumbe wa Mkutano wa Katiba watakuwa na sifa zifuatazo;-
(i) Umri wa miaka 18 au zaidi.
(ii) Elimu ya kidato cha Nne au zaidi.
(5) Mkutano Mkuu wa Taifa wa Katiba utakutana kwa kipindi kisichozidi siku 5.
(6) Mambo yote yanayohusu katiba mpya au mabadiliko ya katiba yatashughulikiwa, kuandaliwa na kuwasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Taifa 

wa Katiba na Tume ya Katiba iliyoundwa chini ya Ibara 121 ya Katiba hii;
(7) Mkutano Mkuu wa Taifa wa Katiba utakuwa na majukumu yafuatayo:-
93
(i) Kuchambua na kujadili misingi ya Katiba.
(ii) Kuchambua na kuidhinisha rasimu ya Katiba pamoja na utekelezaji wa kura ya maoni kupitisha Katiba.
(8) Maamuzi ya Mkutano yatakuwa mapendekezo ya katiba ambayo yatapelekwa kwa wananchi kupigiwa kura ya maoni kupitishwa kama katiba ya 

nchi au kukataliwa.
SURA YA KUMI NA TATU
TUME MBALIMBALI ZA TAIFA
SEHEMU YA KWANZA
TUME YA KATIBA
121.(1) Kutakuwa na Tume ya Katiba ambayo wajibu wake utakuwa ni kuandaa rasimu ya katiba mpya au mabadiliko ya katiba kila mara inapobidi 

mambo hayo yafanyike kwa ajili ya maisha na uhai wa Taifa;
(2) Tume ya Katiba itakuwa na wajumbe wasiozidi watano waliochaguliwa na sekta kuu za jamii kama ifuatavyo:-
(a) Mwakilishi wa vyama vya siasa visivyo serikalini,
(b) Mwakilishi wa chama au vyama vya siasa vinavyoendesha serikali,
(c ) Mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kiraia
(d) Mwakilishi wa Serikali
(e) Makilishi wa taasisi za kidini
(3) Wajumbe wa Tume ya katiba watakuwa raia wa Tanzania wenye utaalamu wa na ujuzi katika taaluma ya katiba wenye kiwango cha elimu cha 

angalau shahada ya chuo kikuu.
94
121.(1) Tume ya Katiba itakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 5 lakini wajumbe wake wanaweza kuchaguliwa kwa kipindi kingine kimoja cha 

miaka mitano;
(2) Tume ya Katiba itaendeshwa kwa fedha zitakazoidhinishwa na Bunge na na itawajibika kwa Bunge.
(3) Mwenyekiti wa Tume ya Katiba atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwao katika mkutano wao wa kwanza.
(4) Kazi za Tume ya Katiba itakuwa ni:-
(a) Kukusanya maoni ya wananchi kila mara, kuyachambua na kuyajadili mapendekezo au marekebisho hayo ya Katiba, na kisha kuyawasilisha 

kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa Katiba kupitishwa, kwa kufuta utaratibu uliowekwa na na Katiba hii isipokuwa kama marekebisho hayo ni yale 

yaliyokasimiwa kwa Bunge,
(b) Kama marekebisho hayo ni yale yaliyokasimiwa kwa Bunge kwa mujibu wa ibara ya 87(1) ya Katiba hii na kuijadili rasimu ya mabadiliko 

hayo ya Katiba na kuiwasilisha Bungeni kupitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hiyo ya Katiba hii;
(c) Kuandaa na kusimamia kura ya maoni ya Katiba ikiwa ndiyo hatua pekee na ya mwisho katika kutunga Katiba;
(d) Kudhibiti wapiga kura kwenye Daftari ya Kudumu la Wapiga Kura kama sehemu ya usimamiaji wa upigaji kura za maoni ya Katiba;
(5) Bunge litatunga sheria kuhusu upigaji wa kura ya Maoni ya Katiba.
SEHEMU YA PILI
TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA MAADILI YA VIONGOZI
95
122. (1) Kutakuwa na Tume ya Haki za Binadamu na Maadili ya Viongozi ambayo wajumbe wake watatoka sehemu zote mbili za Jamuhuri ya 

Shirikisho la Tanzania na watachaguliwa na Bunge baada ya kupendekezwa na mashirika ya raia yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na 

Haki za Binadamu;
(2) Mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka 35 na 70, mwenye mwenendo na tabia iliyojidhihirisha kuwa njema na ya kuigwa atakuwa na sifa ya 

kuweza kuchaguliwa.
(3) Tume ya Haki za Binadamu iatakuwa na wajumbe wasiopungua 5 na wasiozidi 11 na watashika madaraka yao kwa kipindi cha miaka 5 lakini 

wataweza kuchaguliwa kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano;
(4) Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu watamchagua kutoka miongoni mwao mwenyekiti katika mkutano wao wa kwanza.
(5) Tume ya Haki za Binadamu itakuwa na wajibu wa:-
(i) Kusimamia utekelezaji na uboreshaji wa sura ya Haki za Binadamu kama ilivyoainishwa katika Katiba hii,
(ii) Kufuatilia utekelezaji wa Haki za Binadamu kama zilivyoainishwa katika mikataba na makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania 

imeridhia,
(iii) Kusimamia utekelezaji na uboreshaji wa maadili ya uongozi kama yalivyoainishwa katika Katiba hii na sheria nyingine za nchi;
(6) Tume ya Haki za Binadamu itawasilisha Bungeni taarifa yake kwa kila kipindi cha mwaka mmoja kulingana na mwaka wa fedha wa serikali;
(7) Vyombo vya dola vya Shirikisho, Zanzibar na Tanganyika vinawajibika na kulazimika kutekeleza maamuzi na maelekezo ya Tume ya Haki za 

Binadamu.
96
(8) Uamuzi wa mashauri yaliyosikilizwa na Tume ya Haki za Binadamu na Maadili ya Uongozi kufuatana na mamlaka yake ya kimahakama ya kutoa 

haki za binadamu yatakuwa na nguvu za sheria sawa kama hukumu ya Mahakama Kuu ya Shirikisho:
(9) Bunge litatunga sheria ambayo, pamoja na mambo mengine, itafaanuaa na kuweka wazi zaidi majukumu na wajibu wa Tume ya Haki za Binadamu 

na utekelezaji bora wa shughuli zake na pia kuhusu maadili na iiko ya uongozi.
SEHEMU YA TATU
TUME YA UCHUMI NA FEDHA
123. (1) Kutakuwa na Tume ya Uchumi na Fedha ya Taifa ambayo wajibu wake utakuwa ni kuchunguza, kuchukua hatua na kurekebisha mwenendo wa 

uchumi wa nchi ili kuliwezesha taifa kuwa na ushindani katika maendeleo ya uchumi na bishara miongoni mwa jumuiya ya Mataifa;
(2) Tume ya Uchumi wa Taifa itakuwa na Wajumbe wasiopungua watano na wasiozidi kumi toka sehemu zote mbili za Jamuhuri ya Muungano na 

ambao watateuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge kutoka kwenye orodha ya majina ya mabingwa wa uchumi na mambo ya fedha 

yatakayopendekezwa na Vyuo Vikuu, Vyama vya Wafanyabiashara, na Vyama vya anataaluma wa uchumi na Fedha;
(3)Mwenyekiti wa Tume ya Uchumi na Fedha ya Taifa atachaguliwa na wajumbe wa Tume hiyo kutoka miongoni mwao katika kikao chao cha kwanza;
(4) Gavana wa Benki Kuu ya Shirikisho, Katibu Wakuu wa wizara za fedha na uchumi za Shirikisho, Tanganyika na Zanzibar watahudhuria vikao 

vya Tume;
97
(5) Kazi za Tume zitakuwa ni kufuatilia maendeleo ya uchumi na kutoa ushauri juu ya hali na mwelekeo wa uchumi.
(6) Maoni na mapendekezo ya Tume hii yatawasilishwa Bungeni na kujadiliwa.
(7) Tume ya Uchumi wa Taifa itakuwa na Sekretarieti ya kudumu.
(8) Bunge litatunga Sheria itakayofafanua majuku, kazi, wajibu na muda wa wajumbe kushika madaraka (1) Kutakuwa na Benki Kuu ya Jamuhuri 

ya Muungano itakayosimamia uchumi wa nchi.
(9) Vyombo vya serikali vya Shirikisho, Tanganyika na Zanzibar vitawajibika kupokea ushauri wa Tume ya Uchumi na fedha ya taifa na 

kuufanyika kazi;
SEHEMU YA NNE
BENKI KUU
124. (1) Kutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ambayo itakuwa ndiyo taasisi kuu ya fedha na utawala wa mambo ya fedha 

nchini;
(2) Benki Kuu itakuwa ndiyo Benki ya Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na hivyo itaweka fedha za serikali katika mifuko 

iliyoagizwa na Katiba hii na itakuwa ndicho chombo cha kutoa sarafu na kutawala thamani ya shilingi ya Tanzania;
(3) Benki Kuu itaongozwa na Gavana ambaye atateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Tume ya Uchumi na Fedha ya Taifa na ambaye uteuzi 

wake utathibitishwa na Bunge;
(4) Katika utekelezaji wa madaraka yake Gavana atalazimika kufuata maagizo na maelekezo ya Bodi ya Benki Kuu, masharti ya Katiba hii, 

sheria iliyotungwa na Bunge kuratibu uendeshaji wa Benki Kuu, ushauri wa Tume ya Uchumi na 98
Fedha ya Taifa na mamlaka ya mahakama ya kuchunguza na kudhibiti utekelezaji wa majukumu wa Mamlaka na Taasisi za Umma;
(5) Gavana atashika madaraka kwa muda wa miaka mitano lakini muda huo unaweza kuongezwa kwa kipindi kisichozidi miaka mitano;
(6) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika katiba hii Gavana wa Benki Kuu atalazimika kuacha kazi yake mara ambo yafuatayo 

yyatakapotokea:-
(i) atakapotimiza umri wa miaka sabini,
(ii) kushindwa kutekeleza kazi zake kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya au kwa kuvunja masharti ya 

sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
(7) Bunge litatunga sheria itakayofafanua masharti mengine ya kazi ya Gavana wa Benki Kuu.
SEHEMU YA TANO
TUME YA ULINZI NA USALAMA
125. (1) Kutakuwa na Tume ya Ulinzi na Usalama ya Taifa ambayo itakuwa na wajibu wa kumshauri Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania 

kuhusu mambo ya ulinzi na usalama wa Taifa na hasa kuhusu kutangaza hali ya hatari au vita;
(2) Wajumbe wa Tume ya Ulinzi na Usalama ya Taifa watakuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Gavana wa Tanganyika, Gavana wa Zanzibar, 

Spika wa Bunge, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Spika wa Baraza la wawakilishi la Tanganyika, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa 

Wananchi la Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Jeshi la Magereza na Mwenyekiti wa Kamati ya 

Bunge ya Ulinzi na Usalama wastaafu Marais wa Shirikisho la Tanzania na Wastaafu Magavana wa Tanganyika na Zanzibar;
99
(3) Kazi ya Tume ya Ulinzi itakuwa kama ifuatavyo:-
(a) kumshauri Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania kuhusu mambo ya ulinzi na usalama wa Taifa na hasa kuhusu kutangaza hali ya hatari 

au vita,
(b) Kumshauri Rais juu ya jambo lolote katika Jamuhuri ya Muungano ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kwa haraka kwa maslahi ya taifa;
(4) Bila ya kujali masharti yoyote ya Katiba hii, Tume ya Ulinzi na Usalama ya Taifa haitakuwa chombo cha utendaji chenye mamlaka ya 

kuingilia uendeshaji wa Mamlaka na taasisi za dola katika utendaji kazi wa siku hadi siku;
(5) Tume ya Ulinzi na Usalama inaweza kuwaalika katika vikao vyake raia au wataalamu wenye sifa maalumu ikiwa ni pamoja na wataafu wakuu 

wa majeshi.
SEHEMU YA SITA
MKURUGENZI WA MASHTAKA
126.(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Mashtaka wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania ambaye atateuliwa na Rais na uteuzi wake utaidhinishwa na 

Bunge;
(2) Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa ni mwanasheria aliyebobea mwenye sifa za uzoefu wa kazi kwa miaka angalau 10 na atakuwa na umri 

usiopungua miaka 35;
(3) Masharti ya kazi ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa kama yale ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
(4) Maamuzi ya Mkurugenzi kuhusu kutoshitaki au “Nolle Prosequi” yaweza kusahihishwa na Mahakama Kuu ya Tanganyika, Zanzibar na Mahakama 

Kuu ya Shirikisho;
100
(5) Bunge laweza kutunga sheria kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo:-
(a) Mwenendo wa mashitaka kwa jumla,
(b) Mahakama katika Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania ambazo Mkurugenzi wa Mashitaka atakuwa na haki ya kuhudhuria na kusikilizwa,
(c) Maafisa katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao Mkurugenzi wa 

Mashitaka anaweza kuwakasimu madaraka yake,
(d) Utaratibu wa kukata na muda wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama yoyote katika kesi za jinai,
(e) Haki ya raia ya kuanzisha au kufunga shitaka na mtu binafsi.
SURA YA NNE
MENGINEYO
127.(1) Mtu yoyote mwenye dhamana ya kazi iliyoanzishwa na Katiba hii, aweza kiiuzulu kwa kutoa taarifa iliyowekwa saini kwa mkono wake 

kwa kufuata masharti yafuatayo:-
(a) Iwapo mtu huyo aliteuliwa au alichaguliw na mtu mmoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilisha kwa mtu huyo aliyemteua au 

aliyemchagua, au iwapo aliteuliwa au alichaguliwa na kikao cha watu, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye kikao hicho.
(b) Iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
(c) Iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu wa Spika wa Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilisha kwenye Bunge, na
(d) Iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika;
101
(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku 

ile ambayo taarifa yake ya kijiuzulu ilipokelewa na mtu anayehusika au kikao kinachohusika lakini kama taarifa hiyo ya kujiuzulu imeeleza 

kwamba mtu huyo atajiuzulu tangu siku nyingine baada ya taarifa hiyo kupokelewa na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, basi mtu huyo 

atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku hiyo nyingine ya baadaye;
(3) Iwapo mtu yoyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii amejiuzulu, basi ikiwa anazo sifa zote zinazohitajika na 

kwa kila hali anastahili, aweza kuteuliwa au kuchaguliwa tena kushika madaraka ya kazi hiyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
128.(1) Shirikisho laweza kuvunjwa iwapo wananchi wa sehemu zote mbili za Shirikisho, yaani Tanganyika na Zanzibar wataamua hivyo kwa kura 

ya maoni na Shirikisho litakuwa limevunjika siku hiyo uamuzi huo utakapowasilishwa kwa maandishi kwa Spika wa Bunge na Tume ya taifa ya 

Katiba.
(2) Masharti ya kura ya maoni ya kupitisha katiba yatatumika kuhusu kura ya maoni kwa mujibu wa ibara hii.
129.(1) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya 

Shirikisho, ifahamike kuwa mtu yoyote mwenye mamlaka kwa mujibu wa Katiba hii ya kumteua au kumchagua mtu mwingine kushika madaraka ya 

kazi fulani anao pia uwezo wa kumteua au kumchagua Kaimu au mtu ambaye atamkasimu kwa muda madaraka ya kazi au cheo chake, isipokuwa ruksa 

ya kukasimu madaraka haipo kwa madaraka ya kazi ya Waziri, Naibu Waziri, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama ya Shirikisho au 

Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(2) Kanuni zifuatazo zitatumika pia kwa madhumuni yaufafanuzi wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wa
102
kukabidhiana madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho, yaani:-
(a) Iwapo kuna mtu mwenye madaraka ya kazi fulani alikabidhiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na mtu huyo yupo likizoni na wakati 

huo huo anangojea kuacha kazi hiyo, basi anaweza kuteuliwa mtu mwingine, na kukabidhiwa madaraka ya kazi hiyo, bila ya kujali kuwapo kwa 

yule mtu anayengojea kuacha kazi hiyo,
(b) Iwapo kuna watu wawali au zaidi ambao kwa wakati mmoja wote wanashika madaraka ya kazi fulani kutokana na uteuzi wao uliofanywa kwa 

mujibu wa Kanuni iliyoelezwa katika aya ya (a) ya ibara hii ndogo, basi katika hali hiyo kukitokea haja ya kutekeleza shughuli yoyote 

inayohusika na madaraka ya kazi hiyo yule mtu wa mwisho kuteuliwa ndiye atakayehesabiwa kuwa mtu pekee mwenye dhamana ya kazi hiyo,
(c) Iwapo mtu ameteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, kuwa kaimu au kushikilia madaraka ya kazi fulani wakati mtu maalum 

aliyeteuliwa kushika madaraka ya kazi hiyo anashindwa kutekeleza shughuli zinazohusika na kazi hiyo, basi haitaruhusiwa kufanya uchunguzi 

wowote au kutoa hoja yoyote juu ya uteuzi wa huyo Kaimu eti kwa sababu kwamba huyo mtu maalum aliyeteuliwa kushika madaraka ya kazi hiyo 

kushindwa kutekeleza shughuli zinazohusika na kazi hiyo.
TAFSIRI
130.(1) Katika Katiba hii, iwapo maelezo yahitaji vinginevyo:- “amri ya Jeshi” maana yake ni sheria au amri iliyotolewa kwa mujibu wa 

sheria, ya kusimamia nidhamu katika jeshi.;
“askari” likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya jeshi hilo ni mtu 

anayewajibika kinidhamu.
103
“Baraza la Wawakilishi” maana yake ni Baraza la Wawakilishi la Tanganyika au la Zanzibar linalotekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba 

hii, Katiba ya Tanganyika au Katiba ya Zanzibar.
“Chama cha siasa”maana yake ni taasisi ya kiraia inayowajumuisha na kuwashirikisha wananchi kujenga hoja kisiasa kulingana na mtazamo 

fulani wa kiitikadi kwa madhumuni ya kupata ridhaa ya umma kutwaa mamlaka ya dola na kuongoza nchi.
“Jaji Mkuu”maana yake ni Mkuu wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania.
“Jaji Kiongozi” maana yake ni Mkuu wa mahakama Kuu ya Tanganyika au Mahakama Kuu ya Zanzibar.
“Jeshi” maana yake ni lolote kati ya majeshi ya ulinzi na ni pamoja na jeshi lolote jingine lililoundwa na Katiba hii au kwa mujibu wa 

Sheria na linalotawaliwa kwa amri ya jeshi.
“Jumuiya ya Madola” maana yake ni jumuiya nchi zilizokuwa makoloni au chini ya himaya ya Uingereza;
“Kiapo” maana yake ni tamko rasmi la mtu binafsi lenye nguvu ya kisheria linalomfunga anayelitoa kutenda kulingana na ahadi au wajibu 

mbele ya shuhuda ambaye ni kamishna wa kiapo;
“Kiapo cha uaminifu” maana yake ni ahadi ya kisheria ya kuwa mwaminifu kwa Nchi na kwa serikali ya Shirikisho.
“Maadili ya Kazi ya Jaji” maana yake ni masharti ya kimaadili yanayoongoza mwenendo wa watu wafanyao kazi ya Jaji au ya Hakimu.
“Mahakama” maana yake ni Chombo rasmi cha kiraia cha kusikiliza mashauri na kutoa haki kilichoundwa na sheria ya nchi.
“Mahakama Kuu” maana yake ni mahakama Kuu ya nchi yenye mamlaka yasiyo na mipaka na kwa mujibu wa Katiba 104
hii ina maanisha Mahakama Kuu ya Shirikisho, Mahakama Kuu ya Tanganyika au Mahakama Kuu ya Zanzibar.
“Mambo ya Shirikisho” maana yake ni mambo yote ya umma ambayo, yametajwa na ibara ya 4 ya Katiba hii kuwa ni Mambo ya Shirikisho.
“Mamlaka ya nchi” maana yake ni Serikali, Bunge la Shirikisho na Mahakama Kuu ya Shirikisho na kwa madhumuni ya Katiba hii inajumuisha 

Serikali na Baraza la Wawakilishi na mahakama Kuu za Tanganyika na Zanzibar.
“Rais wa Mahakama ya Rufani” maana yake ni Rais wa Mahakama ya Rufani aliyeteuliwa chini ya ibara ya [111?] ya Katiba hii.
“Mwanasheria Mkuu” maana yake ni Mshauri Mkuu wa mambo ya Sheria wa Serikali ya Shirikisho.
“Serikali” maana yake ni pamoja na Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Halmashauri ya 

Wilaya au ya Mji, na pia mtu yoyote anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya serikali au Halmashauri.
“Serikali za Mitaa” maana yake ni vyombo vya kiserikali viliundwa kwa mujibu wa Katiba hii kwa madhumuni ya kutekeleza madaraka ya umma.
“Uchaguzi Mkuu au Uchaguzi unaofanywa na wananchi” maana yake ni uchaguzi wa Rais na uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya 

uchaguzi unaofanywa baada ya Bunge kuvunjwa.
“Waziri” maana yake ni kiongozi wa kisiasa anayekabidhiwa dhamana ya kuongoza Wizara ya serikali.
(2) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Katiba yaani:-
(a)Kila yanapotajwa madaraka ya Rais, ifahamike kuwa madar aka yanayohusika ni pamoja na mamlaka ya
105
kutekeleza shughuli za kazi mbali mbali na vile vile wajibu wa kutekeleza shughuli na kazi mbali mbali kama Mkuu wa Serikali ya 

shirikisho, na pia mamalaka mengine kama hayo au wajibu mwingine kama huo ikiwa imeelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine 

yoyote kwamba mamlaka hayo mengine ni ya Rais au kwamba wajibu huo mwingine ni wa Rais.
(b) Kila yanapotajwa madaraka ya kazi katika utumishi wa serikali, ifahamike kuwa kazi inayohusika ni kazi katika Utumishi wa Serikali ya 

Shirikisho isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo, na kila inapotajwa Idara ya Serikali ifahamike kuwa idara inayohusika na ni idara ya 

Serikali isipokuwa kama imeelezwa vingine.
(c) Iwapo kwa mujibu wa masharti ya katiba hii kuna jambo lolote linalotakiwa litekelezwe au lishughulikiwe na chama chochote cha siasa, 

basi, jambo hilo litekelezwa au litashulikiwa na chama hicho kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na chama hicho kwa ajili hiyo, na pia kwa 

kuzingatia masharti ya Katiba hii au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.
(d)Kwa amadhumuni ya Katiba hii, mtu hatahesabiwa kuwa ana madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho kwa sababu tu kwamba 

anapokea malipo ya uzeeni au malipo mengine ya aina hiyo kwa ajili ya utumishi wake wa zamani katika Serikali ya Shirikisho./
(e) Katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitaji vingine, kila anapotajwa mtu mwenye dhamana ya kazi fulani kwa kutaja madaraka ya kazi 

yake ifahamike kuwa mtu anayehusika ni pamoja na mtu yoyote ambaye ni kaimu au aliyeteuliwa kwa njiaa ya halali kushikilia dhamana ya kazi 

hiyo.
(f) Katika Katiba hii, kila yalipotajwa mamlaka ya kumwondoa mtu katika utumishi wa Serikali ya Shirikisho ifahamike kuwa mamlaka 

yanayohusika ni pamoja na mamlaka yaliyotolewa kwa mujibu wa 106
masharti ya Sheria yoyote yanayomtaka mtu huyo au yanayomruhusu mtu huyo kustaafu. Isipokuwa kwamba maelezo ya kanuni hii yasifahamike 

kuwa yanampa mtu yeyote mamlaka ya kumtaka jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama ya Shirikisho na Jaji wa Mahakama Kuu au Mdhibiti 

na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu astaafu.
(g) Katika Katiba hii, kila alipotajwa au kufuata sheria nyingine, ifahamike kuwa sheria inayohusika ni pamoja na sheria ambayo 

inarekebisha Sheria hiyo nyingine, ama bila mabadiliko au baada ya kubadilishwa au kurekebishwa, au Sheria ambayo inaweka masharti mapya 

katika Sheria nyingine.
131.(1) Jina kamili la Katiba hii ni Katiba ya Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania ya mwaka.......
(2) Katiba hii itaanza kutumika tarehe.........
(3) Katiba hii itatumika Tanganyika na vile vile Zanzibar.
(4) Makao Makuu ya Serikali ya Shirikisho yatakuwa Dar es Salaam.
NYONGEZA YA KWANZA
(Imetajwa katika ibara ya 4)
(Mambo ya Shirikisho)
1. Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Mambo ya Nchi za nje
3. Ulinzi na Usalama.
107
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Utumishi katika Serikali ya Shirikisho.
9. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na masharika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania 

unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
10. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
11. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halai (pamoja na noti) mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) 

na shughuli zote za mabenki, fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha.
12. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa yanamotoka na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na 

gesi asilia.
13. Usafiri na usafirishaji wa anga.
14. Utafiti.
15. Takwimu.
16. Mahakama ya Rufani ya Shirikisho..
17. Uandikishaji wa Vyama vya Siasa na Mambo mengine yanayohusiana navyo.
18. Haki za Binadamu
19. Mahakama ya Shirikisho.
108
20. Tume za Shirikisho.
21. Tamko kuwa Ardhi ni Mali ya Umma.
NYONGEZA YA PILI
MAMBO YASIYO YA SHIRIKISHO
1. Public Service of States
2. Industrial Lincensing and Statistics
3. Umilikaji wa ardhi
4. mambo mengine yote ambayo hayakutajwa katika Nyongeza ya kwanza ya Katiba hii.
NYONGEZA YA TATU
WIZARA ZA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA
1. Mambo ya Nchi za nje
2. Ulinzi na Usalama.
3. Mambo ya ndani na usalama wa raia
4. Elimu.
5. Fedha na Mipango. 109
6. Utumishi katika Serikali ya Shirikisho.
7. Posta, Simu na mawasiliano
8. Maliasili
9. Nishati
10. Katiba ya sheria
11. Adhi na makazi

1 comment:

MARY PHESTO said...

tafadhali iwezeshe wengine tuweze kuikopi kwani wengine ni wasafiri hivyo mtu akiwa nayo ataweza kuisoma wakati yuko safarini. kupitia blog yenu hii.