Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.
8 comments:
Anapendaga makubwa sijawahi Ona .mwafrika shurti ujitutumue.
He he he!! na huyo ndo Rais wa Dunia bwana ulinzi wake ni muhimu sana, warusha maboma sasa hilo mnalo!!!! Hakirushwi kitu hapo mwanangu mzee amejizatiti impasavyo!! Haya Mwee we cant wait to see you in our great Nation of Tanzania Mr. Obama. See you soon.
Mtoa maoni namba moja, ulinzi wa rais wa marekani haupangwi na rais. Intel examines security threats before determining what security level needs to be deployed. So 'kujitutumua' is not one of the determinants on how much security Obama needs while travelling overseas.
I agree with maoni #3, sio mambo ya kujipenda wala kujitutumua, bali kufatia mkatba + we're talking about the USA president here, not like you and me!
Namba 2 na 4. Wazembe watupu kama huna la kuzungumza huna haja ya kujidhalilisha ufahamu wako katika ulimwengu watu wanawacheka
ugeni huo au fujo? mmmhh! yumkini!
rais wa China alikuja na meli ngapi?
Mwenye kutumia lugha *wazembe" yeye ndie mzembe coz akili yake iko tu huko uzembeni. Let's be civil pple! Maoni bila matusi, sioni ovu lolote la #2 n 4 above, for anyone to call them names.
Wazembe? Hii lugha ya uzembe yaletwa na nini tena? Yaani pple can't share ideas without insults? Pleese let's polish our language n try think above the belt. WaTZ twasifiwa kwa matusi na kuingiliana, si sifa nzuri kamwe, can't even bliv mwenye blog posted #5 comment aaaiiii...!!!!!
Post a Comment