ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 29, 2013

CCM YAKOMALIA SERIKALI MBILI

Chama cha Mapinduzi kimesisitiza kuwa bado mfumo wa sasa wa serikali mbili ndio mfumo mwafaka licha ya kuwapo changamoto mbalimbali zilizopo.

Aidha kimesisitiza kuwa hakiogopi utaratibu wa mgombea binafsi na kimeeleza kuwa utaratibu huo unakipa ahueni chama hicho kuliko ilivyo kwa vyama vya upinzani.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza katika mjadala wa mchakato wa katiba mpya ambao umeshirikisha vijana wa CCM toka wilaya tatu za mkoa wa Dar es salaam.

Amesema kuwa CCM inapendekeza kuundwa kwa utaratibu wa kisheria utakao wezesha kuratibu namna mgombea binafsi atakavyo shiriki katika utaratibu wa kisiasa katika chaguzi mbalimbali.

Amesema kuwa muundo wa serikali tatu unatengeneza utata katika mfumo wa kisheria sanjari na urasimu katika kuendesha shughuli za maendeleo na unapunguza uwajibikaji katika uendeshaji wa serikali.

Nnauye amefafanua kuwa kwa mujibu wa rasimu ya katiba mpya inaoyesha kuwa Katiba za serikali zilizopendekezwa zinanguvu kuliko Katiba mama ya Muungano.

Kwa upande wa kisiasa amesisitiza kuwa mfumo wa serikali tatu sio sera ya CCM ambayo inaamini katika serikali mbili ambapo mfumo huo wa serikali unawezesha kuwepo kwa utaratibu wa uwajibikaji na kuwafikia wananchi.
Kuhusu mapendekezo ya umri wa kuwania uongozi uwe ni miaka 25 amesema kuwa bado msimamo wa CCM bado umri wa miaka 21 unafaa kwa vijana nchini kuwania uongozi

No comments: