ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 29, 2013

DAYNA NYANGE ATEMBELEA KABURI LA NGWEA

 Dayna akiweka Mshumaa juu ya Kaburi 
     Mwimbaji wa nyimbo  za mafungu ya nyanya, Fimbo ya mapenzi, Nivute kwako na ule unaotamba sasa wa Leo, Dayna Nyange  mkali wao,  ndani ya mwezi mtukufu, amefanya ziara ya kumkumbumbuka na kutembelea kabuli alilozikwa mwanamuziki mwenzie toka Moroghoro, Albert Mangwea


 Kabuli alilozikwa Mangwea
     Dayna ameonekana katika kaburi la Mangwea, mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza na mwandishi wa Habari hii mara baada ya tukio, Dayna amesema Albert Mangwea  ni mmoja  ya wasanii aliokuwa nao karibu sana na alikuwa  akimsaidia kwa mambo mengi sna katika mziki
   "Unajua Albert Mangwea ni zaidi ya msanii mwenzangu, alikuwa kama ndugu kwangu. Albart alikuwa akinishauli mambo mengi sana juu ya mzikim na hata maisha pia. Hivyo ni wajibu kwangu kumkumbuka mara kwa mara.  Pia kitu ambacho hukijui, Ngwea ni mmoja ya wasanii walionisaidia sana hasa kusambaza wimbo wangu huu wa sasa nilioimba na Mr: Blue - Leo. sitamsahau my Brother Ngwea  na ndiyo maana ndani ya mwezi mtukufu nimetenga siku ya leo kuja kumtembelea. Pumzika kwa amani japo pengo lako bado lipo'' Amemaliza huku akibubujikwa na machozi.
Dayna akipiga saluti ishara ya kumkubari Marehemu Albert Mangwea

3 comments:

Anonymous said...

Kabuli. .... Kabuli, kabuliiii EEEKKKK!!!!!
DUUUUH
Ni KABURI jamani...
Kiswahili gani hki. Halafu mnajigambe eti Watanzania tuna lugha YETU ..... Aibu tupu!

Anonymous said...

We kabuli mimi moroghoro mhh au morogoro

Machaku said...

Pumzika kwa amni Ngwea. Na Dayna uzidi kuwa na moyo huwo howo .