ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 27, 2013

HESABU MAKOSA HAYA 7, HAKIKISHA HUYAFANYI KATIKA UHUSIANO WAKO - 4 (GPL)

Tunaendelea kuchambua makosa mbalimbali katika uhusiano wa kimapenzi, Endelea kuelimika...

Sasa kama wewe unashindwa kukubali ulivyo, unataka nani akukubali? Kadhalika, hiyo ni dalili kwamba hujiamini. Je, kama wewe hujiamini, unataka nani akuamini?

Achana na maigizo, jiamini na uache mguso wako wa asili ndiyo umvute. Wengi wanaoendeshwa na kujivika uhusika ambao hawana ni washamba wa mapenzi. Hata kama baadhi hufanikiwa kutimiza matarajio yao mwanzoni lakini mwisho hubaki na aibu.

KUZIDIWA NA HISIA MAPEMA
Jambo lingine ambalo ni hatari kubwa ni kuzidiwa na hisia mapema. Hakuna anayeweza kupinga ukweli kuwa mapenzi ni mchezo wa hisia, kwa hiyo siyo kosa kuzionesha kwa mtu ambaye umempenda. Tatizo ni wakati wa kuzionesha. Haifai kuzidiwa mwanzoni mwa uhusiano.
Ikae akilini mwako kuwa maisha ya sasa, mpaka unakuja kukutana na mwenzi wako, utakuwa umeshapita kwa wengine, naye ni hivyohivyo, kwa hiyo kila mmoja anajua matarajio ya mapenzi. Kitendo cha kuzidiwa na hisia huamsha hali fulani ya usumbufu kwa mwingine.
Nitoe msisitizo kuwa watu wazuri kwenye mapenzi ni wachache lakini wanatolewa macho na wengi. Kwa kulitambua hilo, unapaswa kuishi kwa akili ili usigeuke kero. Endapo atakuona msumbufu, hatasita kumkaribisha yule ambaye anamuona atampa furaha badala ya karaha.
Lazima atakuwa na uzoefu wa kimapenzi, bila shaka anaujua utulivu katika uhusiano. Kama ndivyo, unadhani atakubali kupoteza muda kwako, wakati kila siku unachemsha kichwa chake kwa maswali au vitendo ambavyo chanzo chake ni kuzidiwa na hisia za mapenzi juu yake?
Ieleweke kuwa hisia hutokana na ukweli wa mapenzi. Yaani, unapozidiwa na hisia, maana yake moyo wako haudanganyi. Unapenda kupitiliza, kwa hiyo unakuwa unahitaji na mwenzako naye akutendee haki. Ni hapo ndipo usumbufu huibuka. Upendo hugeuka kero kwa anayependwa.
Mapenzi siyo maneno, vitendo ndiyo hutafsiri upendo. Vema ukatia akilini kuwa kama kweli unampenda, utamsaidia pia kupata utulivu. Wewe ndiye utamfanya awe na utulivu, endapo hutampa usumbufu wa hapa na pale. Inahitaji busara kidogo kulitambua hilo, kwani wengi wamefeli.
Mara nyingi mtu anayezidiwa na hisia, hushindwa kujidhibiti. Mwenzi wake akichelewa kujibu SMS, hugeuka tatizo kubwa linalohitaji suluhu ya mtu wa tatu. Akimpigia simu, ikaita mara saba bila kupokelewa, akipokea tu shari. Kabla ya salamu ni swali: “Mbona hupokei simu?”
Katikati ya mazungumzo, kama upande wa pili utaonekana kuna utulivu, shari inaanza: “Mbona upo sehemu iliyotulia hivyo? Upo wapi?” Kwa akili ya haraka, inamtuma mwenzi wake yupo nyumba ya kulala wageni, hoteli au sehemu yoyote akishiriki tendo la faragha na mtu mwingine.
Hisia mara nyingi hudanganya, kwani huzalisha mawazo mabaya na matokeo yake ni karaha ndani ya uhusiano. Hakuna anayeweza kuvumilia tuhuma za kila mara. Mapenzi maana yake ni amani na furaha, wewe hiyo amani humpi, furaha ndiyo hana kabisa. Lazima atakukimbia au atakuumiza zaidi kwa sababu anaweza kutafuta mlango wa kutokea wakati hujajiandaa kuachwa.

KUSHINDWA KUSOMA ALAMA
Zipo alama muhimu ambazo ni vema kuzijua na uzibaini kwa mwenzi wako kabla hujazama kwenye dimbwi la mapenzi. Bahati mbaya wengi hutawaliwa na papara, matokeo yake hushindwa kubaini vitu ambavyo vinaweza kumfanya apate uelekeo wa uhusiano wake.
Katika pointi hii, nashauri watu kwenda kwa mwendo wa kinyonga badala ya kupiga mbizi bila kujua kina cha maji. Kusoma alama muhimu kwa mwenzi wako mapema ni sawa na kutegua kitendawili. Itakusaidia kujua kama kweli uliyenaye ana mapenzi ya kweli au anaweza kuwa laghai.
Wengi wanapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi hueleza kuwa wanapenda, tena huweka wazi kuwa hisia zimeanguka kwa wale wanaowapenda. Hata hivyo, huacha mambo mengi ndani ya uvungu wa nyoyo zao. Wewe utakuwa mshindi, endapo utaweza kumsoma mwenzi wako na kumuelewa kinagaubaga.

Itaendelea wiki ijayo.

1 comment:

Anonymous said...

HII ISUU imenigusa sana na nikweli mimi niko hivyo nampenda mtu kiyama yani nimepitiliza ni nature yangu nikiwa nampenda mtu na naona yeye hana mapenzi kama yangu so nimeachana naye japo kuwa bado roho inaniuma nanampenda ile mbaya ja kujiuliza jamani hata kama ukisema ni kero but to me naona ni mapenzi ya dhati ya kweli sina longa longa bwana na nafahamu pia mapenzi ni vitendo lakini nimejaribu kutendea naona ananizingua na cha kushangaza nampenda demu mwenzangu jamani si danganyi na najua na yeye ananipenda lakin naona anasita sababu najua aliye naye ndo anamsaidia kimaisha so hapendi kumkosa na demu mwinginewe
yani usisikiye mapenzi si mchezo si mchezo muandishi uliyeandika nadhani hujapenda usisikiye hata mume wangu simpendi hivi na najiuliza kwa nini na nilikuwa sina taabia hii najaribu kuwa katika ndoa yangu lakini jamani si mchezo usisikiye mapenzi si mchezo hakuna papara wala kero mtaandika na kuandika maneno na misemo na utafiti wote mlio nao ukimpenda mtu kiukweli utakuwa kama chizi zaidi ya mtu uliyorogwa NA KWA VILE HIVI SASA HAKUNA MAPENZI YA UKWELI BASI NDO MAANA MTU ATAKUSHANGA NA KUKUONA WA JAABU NA KUKUONA ZOBA AU LIBUKENI WA MAPENZI AU UNA KASORO KWENYE AKILI ZAKO WHICHI IS NOT TRUE una mapenzi ya kweli na wewe binadamu you expect the same to your partners siyo longa longa za siku hizi katika ulimwengu wetu

I NEVER THOUGHT I WILL LOVE LIKE THIS YANI HATA MUME WANGU SIMPENDI HIVI SI MCHEZO NAJIULIZA KILA SIKU WHY AND WHY TENA KWA DEMU MWENZANGU WHY MUNGU WANGU WEEE WHY