Kiongozi wa kikundi kinachotaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ufutwe, Rashid Salum Adiy
Kesi inayotaka Muungano waTanganyika na Zanzibar ufutwe imefunguliwa katika Mahakama Kuu yaZanzibar.Kesi hiyo iliahirishwa jana MahakamaKuu ya Vuga mjini hapa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi hadi Agosti 23, mwaka huu.
Mrajisi aliahirisha kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 1,950 wa Unguja na Pemba kwa vile Jaji Mkuu waZanzibar, Omar Othman Makungu hakuwapo.
Kesi hiyo ya aina yake ambayo imepangwa kusikilizwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, inataka kubatilishwa kwa makubaliano ya muungano kati ya dolahuru za Zanzibar na Tanganyika.
Wadai katika kesi hiyo wakiongozwa na mwanaharakati Rashid Salum Adiy, wanadai kuwa hakuna hati ya makubaliano ya muungano inayodaiwa kusainiwa Aprili 22, mwaka 1964 siku mbili kabla ya siku ya muungano, Aprili 26. Wafunguaji kesi hiyo wanadai kuwa, mambo kadhaa yanayohusu Muungano yalikuwa batili na kwa hiyo wanaitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar itamke hivyo iliiruhusu kuzaliwa kwa dola huru ya Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza, Mwanasheria Mkuu wa Muungano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa.
Mwananchi
1 comment:
nakutakiyeni kheir,kheir tupu kwa sababu bwana rashid salum adiy umechukua uamuzi mzito kweli na kweli wewe ni mzalendo na mwenye uchungu na nchi yako na hauko lege lege lakini bwana ushauri wa bure usisikiye hawa watu kweli watakuachia bure, watatafuta njia ya kukubandikizia kesi na hata wakiweza kuhatarisha uhai wako najua umejitoa kimaso maso na mhanga lakini pia umuombe sana Allah akukinge na shari za hawa watu hawa watu si mchezo wabaya sana na wanaitawala zanzibar lakini wanapata ushauri kutoka tanganyika so wao wako tu kwa manufa ya matumbo yao na family zao si kwa zanzibar so wako tayari pia wakiambiwa wakuangamize.
nimefurahi sana kuosoma habari hii na kuona kuna kweli kidume jasiri kama wewe usiyopenda kula vya kunyongwa na maini ya kuku na kucheka huku nchi ikiangamiaa kweli Allah awe na wewe daima kwa kupigania haki zetu wazanzibara na inshallah inshallah kwa mwezi huu wa ramadhan inshallah one day yest tutapata nchi yetu inshallah kwa mungu hakuna pana wala refu likosalo ncha au mwisho wake
Allah maa barik ya rashid salum adiy tena kila nikisali na kusoma dua nakuombea mungu ufanikiwe kutukomboa wazanzibari katika machucha ya hawa mafisadi amin amin amin.
Allah akupe nguvu na wepesi na mafanikio ya yote yenye kheir unayotaka yatutokea sisi wazanzibari amin amin
Post a Comment