ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 9, 2013

KIFO CHA MTANZANIA MSAKO MKALI WAENDELEA



BABA WA MAREHEMU KUINGIA MAREKANI LEO

Familia ya  mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu faimilia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na baba mkubwa  wake bwana Ilyasa Sykes.

Marehemu ambaye alikuwa na  miaka 22,  ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na  pia ni  wa  msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.

Omar  aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC)  na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilichaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV*, licha ya upepelezi wanaoendelea nao  pia wanaomba ushirikiano wa wananchi kwajili ya kufanikisha uchunguzi wao. zawadi ya dola 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao. 

Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University Polisi  pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes, kwa mujibu wa maelezo yao  mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi huu. stay tuned kwa exclusive story.
tembelea Blog hii ya Vijimambo, Pamoja na Blog za  http://swahilitv.blogspot.com/ ikishirikiana  na blog ya www.dmk411.blogspot.com

1 comment:

Anonymous said...

inna lillahi waina illahim rajiun so you people are gone kazi ya mungu haina makosa Allah amlaze mahali pema peponi na amghufiriye na sisi pia tuliopo duniani Allah atuongoze katika njia yake ya haki amin we are travels not tourist in this world innna lillahi waina illahim rajiun

poleni sana wazazi,ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu omar ametutangulia na sisi tuko njiani hatujui siku yetu tumuombe malazi mema amin

mdau NY