ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 8, 2013

LOWASSA APONGEZWA NA BAKWATA KWA KUVISHWA JOHO MAALUMU.....MILIONI 590 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipongezwa na kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho la kilemba baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikrakinachomilikiwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza. 
Anayeshuhudia ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Sheikh Salum Hassan Fereji. 
Katika harambee hiyo zaidi ya sh. mil. 590zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. mil 500. 
WAZIRI Mkuu mstaafu Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na makampuni mbalimbali, watu binafisi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.

9 comments:

Anonymous said...

anatafuta kura zenu shauri zenu mmeyasahau yote kwa aliyokufanyiyeni? msiwe mabwege na tizama joho halimfai halimpendezi enyi waislamu msiuze dini yenu kwa pesa hamjui siku atakayo kuiteni Allah,mtukuzeni na muugopeni

Anonymous said...

ndo unafiki wa kinasara ndo huu chungeni sana waja wa Allah

Anonymous said...

Ahsanteee mweshimiwa Lowassa, naomba uendeleee kutuuunganisha sie woote. Yaani watanzania woote tuwe kitu kimoja bila kujali itikadi za dini, chama, sura au rangi. Mungu wabariki waislamu woote na wakristo woote na watanzania wooote.

Anonymous said...

Kweli siasa sio mchezo!

Anonymous said...

and where did he get all those millions he is distributing around the country? I fail to understand, leo 15m, kesho 20m. Alizipataje hizo kama siku zote alikuwa mtumishi wa umma wa kutegemea mshahara? Wabongo, wake up!!!

Anonymous said...

Jamaa ni bilionea, hela mingi sana.

Anonymous said...

Duuuu.........

Anonymous said...

Makubwa haya jamani!!!! Siasa si mchezo, wala sintaongea maneno mengi ila hiyo picha inaongea yenyewe!!!Duuu! kumekuchaaa!

Anonymous said...

Mr President wanna be. People are working he goes around campaigning. With all the crap he did, still want to be awarded by becoming head of state. He better find another alternative.