Leo katika Vijimambo Luke ametuwekea kipande cha video kama kinavyosomeka kwenye kichwa cha habari hii. Nilipata bahati ya kuangalia kipande hicho cha video na baada ya hapa nikashawishika kufanya utafiti kuhusu hiyo show inayoitwa Jumba la BBA. Nilichogundua ni kwamba kati ya show zinazotazamwa sana na Wafrika na nina maanisha wale wanoishi barani Afrika hii show ya Big Brother
Africa inaongoza tena kwa wingi wa wafuasi kuliko ilivyotegemewa.
Nikaendelea kufanya utafiti wangu wa muda mfupi, na kujiuliza faida gani inayopatika kwenye hii show ambaye Waafrika wanaweza kujivunia? Nikasema kabla ya kujibu swali ngoja niende kwenye maoni ya wale wanaoangalia show hii kila siku. Kwa kweli maoni yaliyo mengi yalikuwa yana walakini, na nikaanza kujiuliza haya maoni yanatoka Afrika au Tanzania nilipozaliwa na kulelewa au kuna watu kutoka nchi za Magharibi wanatoa maoni hayo. Lakini maoni hayo yalitoka Afrika.
Mara nyingi tukileta katika majadiliano suala la utamaduni uwa panatokea kutofautia sana, lakini ndugu zangu lazima tufike mahali tukubali kwamba kwa show kama za Big Brother Africa kweli zinaonesha utamaduni wa wa Kiafrika?

Tuanze na hiyo clip au kipande cha video chenye kichwa cha habari hapo juu kama umepata bahati ya kukiona. Vipi kinachooneshwa na kusemwa kweli kinawakilisha fikra na maisha ya waafrika katika Afrika ususani pale ao vijana wanapotoka?
Ebu fikria una mtoto wako umempata au amezaliwa katika bara la Amerika ya Kasikazini au Ulaya, unafungua video kumwonesha utamaduni wa Kiafrika na Big Brother Africa ikiwa ni moja ya show inayosemekana inawakilisha utamaduni wa kiafrika, jamani hapo kuna ukweli au mimi ndio bado mshamba kama wengi wasemavyo?

Twende mbele turudi nyuma, tupige kelele au tusipige, tuseme tusemalo kuhusu aidha kwamba waafrika hatuna utamaduni au tunao, ukweli utabakia pale pale ya kwamba mambo tunayoyaona kwenye show kama Big Brother Africa sio mambo ya kiafrika.
Sisi tuliopata bahati ya kukaa na ndugu zetu wa African America, wana kiu kubwa ya kutaka kujifunza tamaduni za Kiafrika, na wanasema mara kwa mara kwamba ninyi mna bahati kuwa na tamaduni zenu. Saa nyingine wakianza kusema hivyo najisikia aibu kwani pamoja na kuwa na tamaduni zetu wengi wetu tuliopata kwenda shule ndio namba moja katika kupinga tamaduni hizo na badala yake tunaunga mkono kwa wingi tamaduni za kigeni hasa za Magharibi.

Lazima waafrika tuamke na tuanze kuona mbele, ushabiki ni mzuri lakini ushabiki unatutia hasara ni vizuri tukaanza kuuangalia kwa jicho la pekee.
Kwa tamaduni za kiafrika mtu aheshimiwi kwa wingi wa mali au wingi wa pesa, mtu anaheshimiwa kwa busara zake na mchango wake kwa jamii. Na hapo ndipo tunapotofautia na tamaduni za magharibu ambapo kwao mtu mwenye kumiliki vitu vingi na pesa nyingi ndiye mwenye usemi mkubwa katika jamii.

Wengi tunakubaliana kwamba kila tamaduni uchukua mambo mazuri kutoka kwenye tamaduni nyingine hilo lipo wazi kabisa. Lakini waafrika kama tunakubaliana kwamba tunayoyaona kwenye show ya Big Brother Africa ni mazuri na kwa kuwa tumeyaiga kutoka kwenye tamaduni za magaharibi basi mimi sina pingamizi. Lakini kama tunayaona hayana uzuri wowote katika kuimalisha utamaduni wetu, sasa ni wakati wa kuamuka na kusema hili hapana. Kila tamaduni zina uchanguzi wa kipi kiingizwe kwenye tamaduni au kipi kiondolewe, mfano mzuri ni hivi majuzi amapo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema sasa basi picha zinazonesha utupu kuwekwa kwenye mitandao ambayo watoto wanaitumia mara kwa mara. Na hili alilisema baada ya kushinikizwa na wazazi amabo waliona mwelekeo wa watoto wao sio.
Tuna kesi nyingine ambapo nchi za magharibi zilitaka waafrika wakubali mahusiano ya jinsia moja, kwa kuwa si utamaduni mzuri kwetu waafrika tulisema hapana.
Kwa maoni yangu nafikiri waafrika tukiamuka na tukasema mambo haya si mazuri kwa jamii yetu ya kiafrika, hakuna hatakayetulazimisha.
Kuona show inayoangaliwa na watu wengi Afrika hasa vijana wetu, ikiwa imejaa lugha chafu, kuingilia kimapenzi bila kificho, na kula na kunywa bila kufanya kazi na baadae unakuwa tajiri. Hii ni show ambayo haiwakilishi ukweli kuhusu Afrika.

Afrika ni bara linalokuwa sana na lenye changamoto nyingi, kama watu kwenda shule, upatikanaji wa maji safi, kuamusha hali ya kufanya kazi na kujitegemea, kuleta umoja na mshikamano ambao tunaelekea kuupoteza sasa, na zaidi kujisimamia kama waafrika.
Ni changamoto, hakuna mtu wa kutufanyia ni lazima tufanye wenyewe, ni Obama wala Bush, si Cameron au Puttin ni sisi Waafrika kamuka na kusema haya maonesho yanayowapumbaza vijana wetu sasa basi

Asanteni na karibuni tutoe maoni yetu ya jinsi gani tweweza kuwa makini katika uchaguzi wa lipi liingie kwa utamaduni na lipi litoke
Ni Mimi mkereketwa na tamaduni za Afrika.
1 comment:
Naunga mkono hoja ya muandishi wa makala hii. Kwa kweli huu utamaduni wa kisasa wa kuiga yaliokuwa kinyume na maadili yetu ya Kiafrika ndio kunakoturejesha nyuma kimaendeleo.
Mdau Haji Jingo, California.
Post a Comment