ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 26, 2013

Mazoezi ya Yanga kama jeshini

Yanga mazoezini.

Khatimu Naheka na Joan Lema
KIKOSI cha Yanga kinaendelea na mazoezi makali, lakini endapo utafanikiwa kuyashuhudia ni wazi utadiriki kusema ni kama yale ya jeshini.
Katika mazoezi ya juzi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Loyola, Dar es Salaam, Kocha Ernie Brandts aliwapa wachezaji wake mazoezi magumu, mengi yakiwa ni yale ya kusaka stamina.
Brandts alianza kwa mbio za kuzunguka uwanja, aliwabadilisha dozi kwa kuwataka kubebana mithili ya wale wanyanyua vyuma vizito, huku wakisukumana kwa nguvu wakipewa sharti la kuhakikisha hawaanguki, mazoezi ambayo yaliwapa shida wachezaji hao.
Aidha, aliwataka kutembea kwa kutumia mikono huku mmoja akimshika mwenzake miguu ya nyuma na baadaye akawahamishia kwenye kuruka viunzi, mazoezi ambayo yalionyesha kuwapa shida wengi wao.
Mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Brandts alizungumza na Championi Ijumaa ambapo alisema: “Aina hiyo ya mazoezi inalenga katika kutafuta stamina kwa wachezaji wangu. Sidhani kama ni magumu sana, hata msimu uliopita tuliyafanya haya tukiwa Uturuki.”

No comments: