ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 3, 2013

MTANZANIA AJINYONGA ULAYA

Habari kutoka kwa baadhi ya Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba Mtanzania aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani Japhari ameaga dunia kwa kujinyonga.

Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo, alisema ” I hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha shughuli zote zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu", alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara. Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi ki masomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji. 

Marehemu Shabani, ameacha mke na watoto Kandhaa, na dua zetu tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia yake nyingine kubwa, iliyopo Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na msiba huu, ambao bado umetuacha na maswali mengi, bila majibu.

3 comments:

Anonymous said...

Duu!! Kweli hili nalo janga!!! Nisingependa kabisaa kumuongelea marehemu kwa ubaya ila naswali jamani, sasa mtu unapojinyonga kwenye nchi za watu inakuwa je? Halafu aliacha pesa za kusafirisha mwili wake amaa inabidi achaangiwe tena? maana hichi si kifo cha ghafla alipanga kujinyonga mwenyewe!!! Mmh! Mungu aitie nguvu familia yake maana hao ndo watapata taabu. Watanzania wenzangu mlio mbali na Tanzania na wasihiii sana tena nawaomba kabisa msijinyongee nchi za watu jamani, maana sasa mnawapa taabu kubwa mlio waacha nyuma! Kama ni kifo cha ghafla hakika hatuwezi zuia ni mipango ya Mwenyezi Mungu, Ila kuutoa uhai wako mwenyewe jamani tufikirie kidogo walu turudi makwetu tukafie makwetu. Nihilo tu wandugu. Roho ya marehemu ipumzike kwa amani, sisi sooote tu safarini.

Anonymous said...

Hakuna maana kumlaumu limeisha tokea ni kuangalia kitakachofuata NA si kumlaumu marehemu. Kesha jinyonga. Tumwombee kwa mungu mwenye huruma amsamehe NA aipokee roho yake mahali pema peponi.

Anonymous said...

mdau wa kwanza naelewa unachosema kuishi nje ya nchi kwa sisi watanzania tatizo kubwa linalotukuta ni michango ya wenzetu wakifariki inabidi kuchanga ili wafikishwe nyumbani, wanaposhikwa na polisi kwa makosa ya kujitakia kutokua na vibali vya kuishi tunaambiwa tuchange pesa ya lawyer na pesa ya kusaidia kesi, wakioana michango wakizaa watoto mchango ninachokwambia jiandae kuchanga tu lazima ameacha usia azikwe Tanzania atafikaje? nakushauri kuepuka adha hiyo jitose kwanye maisha ya wenye nchi usijihusishe na makundi ya watanzania ukijihusisha hutaepuka michango