Baba wa kambo wa Sylvia amekua akiona malezi yake kama mzigo hasa elimu, lakini kwake Sylvia anasema elimu ni njia pekee ya kubadilisha maisha ya familia yake.
Sylvia ni msichana wa miaka minane anaishi kijiji kimoja Tanzania, licha ya maisha yake amejitolea kupata elimu na kila siku hutembea kwa saa moja unusu kwenda shuleni. Yeye ni miongoni mwa wasichana waliobahatika kupata elimu Barani Afrika
Safari ya msichana huyu kisha inampeleka barabara kuu. Wakati mwingine kuna jua kali, vumbi nyingi. Msimu wa jua barabara hujaa mapote na inampa changamoto msichana huyu katika safari yake shuleni
Ikiwa msichana huyu hataki vumbi na matope ya barabara, huamua kupitia kwenye njia ya reli. Hata hivyo kuna hatari zake, treni huenda ikaamkanyanga. Wakati mwingine watoto wa shule wamekua wakitekwa nyara.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na Utawaduni-UNESCO asili mia 62 ya wasichana Afrika wameweza kuingia shule za upili, hata hivyo nchini Tanzania ni asili mia 32 pekee ya wasichana ambao wanaweza kujiunga na shule za upili.
2 comments:
Wadau contact za huyu mtoto ziko wapi tumsaidie ?
Anon wa kwanza I'll support you in this, contacts please!
Post a Comment