Imekuwa ni mazoea kwa jamii yetu kupuuza
na kutokuzipa uzito kauli na mawazo yanayolenga kujenga taifa letu. Badala yake
tumekuwa tukitumia muda mwingi kushabikia na kuongelea mambo yasiyo na tija kwa
taifa. Kwa sababu hii CHADEMA UK tuko mstari wa mbele kuzipigia mbiu na kuzipa
umuhimu na uzito wake kauli za waTanzania zenye nia ya kulijenga taifa tukianza
na kauli nzito iliyotolewa na Shekh Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini
(BAKWATA). Kwanza kabisa Tunampongeza kwa dhati kabisa kwa ujasiri mkubwa
kuzungumzia maswala mabayo viongozi wetu wengi katika ngazi mbali mabli
kitiaifa wanalikwepa aidha kwa makusudi au kutokana nan nidhamu ya uoga. Shekh
Shaban Simba amegusia swala muhimu sana kuhusiana na mustakabali wa siasa na
dini ndani ya nchi yetu. Kwa uwazi mkubwa na kwa nia njema kabisa katika juhudi
za kuliepusha Taifa letu na migangano ya
kiimani katika misingi ya malumbano ya kisiasa, ametutahadharisha WaTanzania
wapenda amani kuwa makini na baadhi ya wanasiasa wanaojenga utamaduni wa
kupenyeza siasa katika nyumba za ibaada kwa kasi kupitia iilimradi wapate
majukwaa ya kuendeleza matakwa yao ya kisiasa. Na zaidi ameelezea mpango wa
kuanzisha vikundi vya usalama ili kulinda amani ndani ya BAKWATA.
Hivi karibuni tumeona jinsi ambavyo
baadhi ya wanaiasa wamejikita kwenye nyumba za kuabudu kwa kile ambacho ni
dhahiri katika kuendeleza (to pursue) ndoto zao za kisiasa. Cha kusikitisha ni
kwamba baadhi ya viongozi hawa kwa nyakati tofauti wameshawahi kuhikilia
nyadhifa mbali mbali za kisiasa na ndani ya serikali. Kwenye nyadhifa zao
ungetegemea wangetumia nafasi zao kuonesha ufanisi na na kudhihirisha uwezo wao
wa kuongoza na kujenga imani kwa wananchi. Badala yake wanatumia nyumba za
kidini kutaka tena nafasi za kuongoza. Cha kusikitisha zaidi ni jinsi ambavyo
baadhi ya viongozi wa dini wanavyokubali kurubuniwa na kutumiwa vibaya na
wanasiasa. Alichozungumzia Shekh Mkuu ni ukweli usiopingika kwamba nyumba za
dini si majukwaa ya kisiasa. Kama waTanzania wenye mapenzi na nchi yetu,
tunapenda kusisitiza na kukazia kauli ya Shekh Mkuu. Nyumba za kuabudu zitumiwe
kwa madhumuni hayo na si vinginevyo.
Shekh Mkuu pia ametoa agizo la kuundwa
kwa kamati za ulinzi ndani ya BAKWATA nchi nzima ili kulinda amani. Alisema
mpango huu ni katika kutekeleza maagizo yaliyopendekezwa na kiongozi mkuu wa
jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema. Nia ni kugundua viashiria vya uvunjaji
wa amani na kuzipeleka kwenye vyombo vinavyohusika. Kwa mukhtasari tu, IGP
ametoa maelekezo haya kwa kuwa uwezo wa jeshi la Polisi kulinda na kuzuia
matukio ya kijangili ni mdogo na hauwezi kufika kila mahali hivyo ni jukumu la
viongozi wa taasisi mbali mbali kuweka mikakati ya ulinzi kwenye mikusanyiko
yao. Kwa mantiki hii Shekh Mkuu ana kila sababu ya kujipanga na taasisi
nyingine zina kila sababu ya kujipanga.
Ni jambo la ushujaa na lenye kuonesha
ukomavu kuona kiongozi mkuu wa dini akiweka bayana hisia zake kuhusu
mustakabali wa siasa na dini ndani ya nchi. Na kwa sababu hiyo CHADEMA UK
tunampongeza Shekh Mkuu kwa kuonyesha mfano wa kuigwa na viongozi wote wa dini
kukemea bila staha utamaduni huu wa kujaribu kuingiza siasa katika nyumba za
ibada. Kila kiongozi angekumbuka wajibu wake kama shekhe Shaban Simba, tuna
imani kuwa mambo mengi ya kijami yaliowashinda wanasiasa kukemea kwa kukosa
(moral authority), yange fanyiwa kazi kwa ufanisi kwa wale wanoaminiwa na jamii
kwa kiwango kikubwa. CHADEMA UK itaunga mkono kwa nguvu zote MTanzania yeyote
atakaye simamia msingi mikubwa ya amani kitaifa kama Shekh Shaban Simba. Kwa
upande wa kauli ya IGP kuhusu vikundi vya ulinzi katika taasisi mbali
mbali, tuna kila sababu ya kuamini
kwamba mapendekezo haya ya IGP kuwataka viongozi wa taasisi mbali mbali
kuanzisha vikundi vya ulinzini ili kusaidiana na vyombo vya dola katika kulinda
mikusanyiko yao , yamekuja wakati muafaka hasa baada ya kiongozi huyo mkuu
kukiri uwezo mdogo wa Polisi katika kulinda amani nchi nzima.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
CHADEMA UK
No comments:
Post a Comment