Wadau habarini za saa hii.........mi leo nna janga moja tu kama kichwa cha habari kinavosema hapo USABATO umekua kama jinamizi kwa wanafunzi wanaosoma The University of Arusha(UoA) ambao si wasabato pia na hata kwa baadhi ya wasabato wenyewe. Kuna maeneo kadhaa ambapo jinamizi hilo limekaba zaidi kama ifuatavyo;-
1. Ajira- Yaani pale chuo kile 98% ya staff ni wasabato hadi walinzi. Mi binafsi naona hilo ni tatizo kwani kwa mazingira hayo inafanya baadhi ya sehemu kukosa ufanisi kwani anaajiriwa mtu asiekidhi vigezo ili hali tu ni msabato.......hilo linaonekana hata kwa baadhi ya walimu majina kaapuni kwa sasa.
2. Huduma generally - Hii includes Cafeteria na hata dispensary......mfano dispensary yaani mtu hata kama yuko serious vipi kuumwa kama imeangukia Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni ujue huyo imekula kwake na ataambulia panadol tu toka kwa marafiki.....yaani kuna wakati wagonjwa hata walio serious wanakua discharged siku za Ijumaa hata kama hawajapona kisa tu sabato inaanza. Thats not business mbaya zaidi watu wanalipia pesa zao tena nyingi tu maana pale ada ni 1.5 up to 1.9M
3. Uongozi serikali ya wanafunzi - Yaani nafasi kuu za juu kama waziri mkuu,raisi na makamu wake wewe kama si msabato basi hiyo imekula kwako hata kama unauwezo wa kuingoza kiasi gani..... hili linafanya unapatikana uongozi wa kupelekwa pelekwa na uongozi wa kanisa bila kujali maslahi ya wanafunzi. Pia hilo limaleak na kupollute the whole students government meaning the cabinet.
4. Mpangilio wa baadhi ya kozi - Mfano mzuri ni hawa wanafunzi wanaotarajia kuingia mwaka wa pili........yaani mwaka wa kwanza tu walikua na vipindi vya masomo ya dini vi3 yaani semester ya kwanza kimoja chenye credit hours 3 kila week na semester ya pili kulikua na vipindi vya dini vi2 vye credit hours 5 kila week sasa tujiulize wameenda pale kusomea uchungaji au ndio kupelekwa pelekwa.....mbaya zaidi vipindi muhimu kama vile Writting skills vinapewa credit hours 2 kila week,basi hata wangefanya hayo masomo optional yaani ni compulsory na kila mwanafunzi lazima awe na biblia............kingne ni pale mtu anapolazimishwa kusoma kozi inayofundisha falsafa za Kisabato tena kwa lazima yaani hapo mwanafunzi atameza quotes za ELLEN G. WHITE bila kupenda.
Hayo ni baadhi tu ya mambo machache ambayo yamepitiwa kwa sasa juu ya usabato uliokithiri chuo kikuu cha Arusha.
Hayo na mengine mengi yanafanya chuo kiwe na maendeleo duni including facilities ambapo wao husisitiza on keeping the values za kisabato basically the old testament lakini kama wameamua kuingia in business they have to forgone some kwa sababu huumiza wanafunzi na mbaya zaidi hata katika kitabu cha TCU wangeidentify kabisa kuwa chuo hiki ni cha kisabato na tunatoaga upendeleo kwa wanafunzi wa kisabato............ Ukimya wa wanafunzi wa dini nyingine si ujinga ila tuu ni kujaribu kuelewa ila hope wote tunajua kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho hivo basi siku mwisho wa uvumilivu wa wanafunzi wa dini nyingne ukifika sijui watafanya nini.
Kwa leo lemmi end here lakini naomba TCU wakipitie chuo kile la sivyo kuna siku patachimbika.
7 comments:
Mimi kwa uelewa wangu hata kama wameingia kwenye business walitaarifu kuwa wanaendesha chuo kisabato fwatilia utaliona hilo, kwa maswala ya masomo ya dini ndio ratiba za vyuo vya kisabato zilivyo, na maswala ya uongozi pia km shule ni ya kisabato lzm wapate waongozaji wasabato na ht km sio wawe tayari kufwata sheria za kisabato, mbona kuna vyuo hata vya wakatoliki nao wana ratiba zao hamsemi mmeona wasabato tuu, na mnajua fika kuna faida za kusoma chuo cha kisabato ndio maana mpk ss mpoo.barikiwa
kaza buti baba bado bado mambo ndo kwanza yanaiva jikoni ukiona jinamizi hili sasa sijui nikuambiyeje akija jinamizi hili lina anza kuruka ruka kama mbawara hapo chuoni ndo utajua kazi bado
halafu uniambiye tanzania haina dini so mnakiona chenu sasa na hii bado ni mchezo wakuigiza tuu bado picha yenyewe kamili.
kaza buti baba kuwa msabato na wewe kwa kujipendekeza ili yako yakuendee ha ha ha tanzania tanzania naipenda tanzania na dini yake tanzania tanzania ha ha ha
"Do your homework mdau" ulisoma curriculum au catalog ya chuo kabla ya kuandika haya malalamiko au kujiunga na chuo?
Sasa labda nikueleze tu mimi sio 'msabato' ila ninachofahamu na kukuomba na wewe ukuze uelewo wako halafu urudi hapa na matokeo ya uchunguzi wako fanya yafuatayo;
-Nenda vyuo vya dini kama Zahrau (Tanga), Catholic, Lutheran, au dini yoyote unayojua wewe na wana vyuo vikuu kisha fanya utafiti uliofanya kwa chuo hicho cha Sabato kupitia vipengele ulivyoweka hapo juu halafu tupe matokeo.
-Mungu ibariki Tanzania kwa sasa tuna vyuo hata majina siyajui. Hakuna mtu amekushikia mtutu kusoma au kufanya kazi katika chuo hicho. Unaweza kwenda katika vyuo vyovyote vile uvipendavyo wewe na vina sifa unazotaka wewe. Kwa kukumbusha zaidi natumaini hicho chuo ni 'private' sasa watafanya wanachoweza wao na kila kilicho katika mkataba wao na aliowapa kibali.
Kwa ushauri zaidi au wewe kama sio mwanadini yeyote nenda vyuo vya serikali.
Asante.
Mleta malamiko unalako jambo, toa mfano wa chuo chochote cha dina ambacho kiko fofauti ya hicho cha kisabato, vyuo vyote kama ni vya dini vinafuata mashart ya dini unauapo join you have to have that in your mind. Ni mtoto wangu akiwa likizo nampeleka tuition katika shule moja ya kiislam Mwanza believe me she has to wear long skirt cover her head akiwa maaneo ya shule otherwise no tuition. Stop being a moaner and attention seeking.
Hivi kweli si kiwango tu cha elimu kimeshuka kumbe hata cha busara. I thought one would never join an institution, academic or otherwise, without having taken the trouble to discern its core values and standing! Hivi by any other name ni baada ya kuingia ukagundua kumbe ni Chuo cha Kisabato! It speaks immensely about the competencies of the complainant! Mwenye tatizo ni mlalamikaji sio Chuo. What a shame. Tumelea kizazi cha walalamikaji tu. This complainant is one such case!
hakuna jinamizi lolote chuo kikuu cha arusha kwa maana hata ukitembelea vyuo vyote vinavyoendeshwa na mashirika ya dini lazima viwe na maadili na viendeshe na taratibu za dini husika mi ni mwanafunzi mmoja wapo wa chuo kikuu cha arusha ELIMU tunayopatiwa chuo kikuu cha arusha ni bora na ya Maadili kuanzia mavazi ya wanachuo ni mazuri kulinganisha na vyuo vingine na hakuna dalili zozote za ubaguzi katika chu kikuu cha arusha watu wote wanaeshimiwa kwa dini zao pamoja na chuo hicho kuendeshwa kwa maadili ya kisabato.na kupitia Utaratibu huo tumejengeka kimaadili kama wasomi
Mungu ibariki UOA Kwa maendeleo ya elimu bora na maadili bora kwa kizazi kijacho.Amina
Me nakipenda chuo changu.... Naomba mungu magufuli asije tuu huku maana atatumbua meengi. Mungu please do something Kwa magufuli aache kufwatilia mambo yasiyomuhusu, aki inaniuma.... Sipendi uongoz wake.... Sijaona faida niliyopata toka kaingia madarakani.... Chuo kikuu cha arusha nakupenda saaana chuo changu. Bora ni private.... Maadili mema na hakina shida.... ������ University of arusha. Mungu atujalie amen.
Post a Comment