ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 20, 2013

FAHAMU HATUA NNE ZA UKIMWI

NI hatua zipi anazozipitia mtu aliyeambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi (VVU) mpaka kufikia hatua yakuitwa mgonjwa wa Ukimwi.
Zipo hatua nne ambazo mtu aliyeathirika hupitia na akiona dalili mojawapo ni vyema akawahi katika kituo cha afya ili kupima afya yake na akigundulika ana tatizo awahi kupewa matibabu.

1. Hatua ya kwanza
Hatua hii ya kwanza kitaalamu huitwa Primary HIV Infection. Huwa na dalili ambazo siyo kubwa sana na huwa zinaweza kuonekana kwa mtu ambaye hajapata uambukizo wa virusi vya Ukimwi.
Dalili hizo ni kuvimba tezi, kupatwa na homa kali, kuumwa koo, kujihisi mchovu na maumivu sehemu mbalimbali mwilini , kutokwa na vipele mwilini (skin rash) kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo.
Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba mgonjwa mwingine anaweza asipate magonjwa hayo kutokana na kinga yake ya mwili.

2. Hatua ya pili
Katika hatua hii ya pili inaweza kudumu kwa muda wa miaka kumi, mgonjwa vilevile anakuwa haonyeshi dalili yoyote ile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba. Kiwango cha VVU kwenye damu huongezeka kulingana na jinsi mgonjwa anavyochukulia ugonjwa kwa mfano kutokufuata masharti aliyopewa na daktari baada ya kugundulika kuwa na maambukizi.
Dalili ya mgonjwa kufikia hatua hii ni kupungua chini ya asilimia 10 ya uzito wa mwili bila sababu maalum au kukumbwa na magonjwa ya mara kwa mara kwenye mfumo wa upumuaji , magonjwa ya masikio, kinywa, tezi la koo, mkanda wa jeshi (Herpes zoster), vidonda pembezoni mwa mdomo, vidonda vya mara kwa mara kwenye kinywa, vipele mwilini, ugonjwa wa ngozi, maambukizi ya fangasi katika kucha.
Tafiti mbalimbali zimeonesha kwamba VVU katika mwili huwa vinazaliana na hujificha kwenye tezi . Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa Virusi vya Ukimwi (Viral load test) katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

Itaendelea wiki ijayo.

GPL

No comments: