UONGOZI wa Simba upo katika hatua za mwisho za kumsainisha mkataba kiungo wao wa zamani, Henry Joseph.Awali, kiungo huyo alikuwa akikipiga nchini Norway katika Klabu ya Kongsvinger ambayo aliamua kuachana nayo baada ya kushindwa kukubaliana na matakwa ya viongozi wa timu hiyo ili kuingia mkataba mpya.
Zakaria Hans Pope, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, tayari kamati yake imeshafanikiwa kukutana na nyota huyo na kufanya naye mazungumzo na kwamba sasa kilichobaki ni kuingia naye mkataba.Hans Pope amesema kiungo huyo atasajiliwa na timu hiyo akichukua nafasi ya beki wao, Shomari Kapombe, aliyetimkia nchini Ufaransa katika Klabu ya Cannes. “Tumezungumza naye (Henry), hakuna shida tutamsajili, kuna mambo tunayaweka sawa kabla ya kumsainisha, tutaingia naye mkataba maalum ambao utamuwezesha kuondoka wakati wowote akipata timu nje ya nchi, amekuwa muwazi kwetu kuwa, bado ana mipango ya kucheza soka nje ya Tanzania,” alisema Hans Pope. kauli hiyo ya Hans Pope, Championi Jumatatu lilizungumza na Henry ambaye alikiri kufanya mazungumzo na Simba, akadokeza kuwa bado hajamalizana na timu hiyo ingawa mazungumzo yapo katika hatua nzuri.“Ni kweli nipo katika mazungumzo na Simba ya kuingia nao mkataba, lakini bado hatujamalizana lakini kila kitu kipo sawa, kuna uwezekano mkubwa tukakubaliana, ngoja tusubiri kidogo,” alisema Henry ambaye aliwahi kuwa nahodha wa kikosi hicho cha Simba kabla ya kutimkia nchini Norway
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment