ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 21, 2013

HUNITAKI TENA KWA SABABU UMEPATA MWINGINE SASA KWA NINI UNANIVUA NGUO KWA MARAFIKI ZAKO

Mimi ni Msichana wa Miaka 25 imetokea bahati mbaya tumeachana na Mchumba wangu baada ya yeye kupata msichana mwingine nimelia sana ili turudiane lakini wapi , kibaya zaidi akiwa na marafiki zake ananiongelea mimi kuwa eti sijui mapenzi ya kitandani kuwa eti huwa tukifanya nalala kama mgomba ...na mengine mengi ya siri ambayo labda ni kweli ama si kweli ....Sasa nashindwa kuelewa kwanini anivue nguo mbele ya rafiki zake baada ya kuachana ....naona aibu hata kupita mtaaani anaongea sana jamani

4 comments:

Anonymous said...

Mtoto pole sana, kwanza bado ni mdogo utapata mwingine, muombe Mungu akusaidie akuletee wa kukufaa. Kumbuka kuwa LIKUEPUKALO na SHARI lina HERI yake.

Anonymous said...

Huyo jamaa wewe muache kama alivyo. Yote hayo kwa sababu hana mazungumzo.manaume alio kua na akili zake asinge fanya ujinga.wewe mwanamke muache yeye awe mpumbavu.wengi mambo haya yametukuta.jamaa sasa hivi yeye ndio anaonekana Mjinga kila sehemu apitazo

Anonymous said...

Kwanza kama hio ni picha yako basi siamini kama maneno ya mwanamme huyo yanakutia aibu. Ulijuwa wewe mwenyewe kwanza kama mwanamke uone aibu kutandaza picha lako hapo na kuendeleza kujitolea hio aibu. Kaa kimya ujistiri na kujiheshimu ndipo wengine watakuheshimu na vile vile ndio ungeonyesha watu kuwa asemayo huyo kijana hayana ukweli. Pole iliobaki katafute shule uendeleze elimu ili uongeze manufaa ya maana mpaka pale mungu atakapokujaalia kuolewa na sio kuzini.

Anonymous said...

Pole sana. Mimi naona umejiongezea matatizo: yeye kawaambia rafiki zake, lakini wewe umeuambia ulimwengu mzima, mpaka picha?!