Mwanamke mmoja ambaye ametambulika kuwa ni mtanzania amekamatwa kwenye airport ya Dubai akiwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine na alikuwa anatoka Brazil kuja Tanzania ambapo baada ya kuhojiwa na Polisi wa Dubai, kasema rafiki wa mme wake ndio alimuomba ampelekee mizigo yake nyumbani Tanzania.
Huyu mwanamke amesema alikuwa anatoka kwenye mapumziko ya miezi mitatu ambayo aliandaliwa na mume wake huko Brazil lakini anavyorudi ndiyo alipewa huo mzigo kuuleta Tanzania ambao ni dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya zaidi ya bilioni moja nukta tatu za Tanzania(Dhs 3 million).
Alikamatwa wakati anajiandaa kubadilisha ndege ili kupanda inayokuja Tanzania.
Hakujatolewa taarifa nyingine zaidi ila millardayo.com inaendelea kufatilia info zaidi kwa sababu bado Mtanzania huyu anashikiliwa na polisi wa Dubai.
Hiyo picha imezibiwa hukohuko Dubai ilikopigwa.
Hili tukio limetokea siku kadhaa baada ya mabinti wa Kitanzania kukamatwa wakiingiza dawa za kulevya kwenye nchi za Zimbabwe na Afrika Kusini wakati pia kwenye Uwanja wa ndege Dar es salaam mwanaume Mtanzania alikamatwa siku kadhaa zilizopita akiwa anasafirisha dawa za kulevya.
3 comments:
hawa na mules(mapunda) wanatumiwa tu bwana na wao ndo wanaoasirika kila leo wanatumiwa na mwabanyenye na pedejee waliopo katika madaraka makuu serikalini na wafanya biashara maarufu wanajulikana sana watu hawa lakini hawashikiki ndo tatizo la serikali ya ccm watu wameshaamka bwana umaskini mbaya ndo unawaponza mabinti kama hawa na kuwa na tamaa ya kutaka kutajirika haraka haraka mungu awasaidiye lakini kama nilivyosema hapo awali wafanya biashara mapapa wa biashara hii wanajulikana na wamo serikalini ya ccm na pia wanatetewa kwa nguvu zote na serikali hii ya ccm wanakamatwa hawa vidaga na kusota rumba poleni sana madada zetu na mama mama zetu kuna mengi ya kufanya na kutafuta utajiri si lazima muwe punda wa kubeba sembe
nawakilisha
Huyu Dada nimzoefu wa kubeba Unga...nasio Mtz ni msouth africa.alie kulia Bongo.bora mlivyo weka picha yake ilimashoga zake waone na wakome kubeba unga.
Huyu binti wa magomeni -mwembechai .hizi pesa za ulaini zinaponza watu jamani. Tumuombe mungu atuepushe
Post a Comment