ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 20, 2013

LIYUMBA AKWAA BALAA JIPYA,YEYE NA MKEWE HAPATOSHI

MNAMKUMBUKA 
aliyekuwa kigogo wa Benki Kuu ya Tanzania aliyefungwa jela miaka miwili kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa mali za umma, Amatus Joackim Liyumba? Basi amekwaa balaa jipya, Uwazi linajua kila kitu
Liyumba na mwanamke aliyedai ni mke wake, Aurelia Paulo Ngowi wamefikishana Mahakama ya Kinondoni, Dar kisa kikidaiwa ni mzee huyo kumtaka mwanamke huyo kuondoka haraka kwenye nyumba anayoishi na watoto wao wawili.
Nyumba hiyo ipo Mbezi ya Afrikana, jijini Dar. Mbali na kuwa makazi, lakini sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ni Hoteli Amjen yenye kupata wateja kila siku.
Jina la Amjen linadaiwa ni muuganiko wa majina ya Amatus na Jennifer ambaye ni mtoto mmoja kati ya hao wawili wa mzee huyo. 
Aurelia ndiye aliyekimbilia mahakamani kuomba msaada ambapo shauri lake lilifunguliwa kwa namba 59, 2013 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Rugemalira.
Baada ya ombi hilo, mahakama ilimwamuru Liyumba kumwacha mkewe na watoto hao waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka shauri hilo litakapotatuliwa kisheria.
Haikujulikana mara moja kama Liyumba anataka mkewe na watoto waondoke kwenye nyumba hiyo na yeye kwa sasa anaishi wapi. 
Jitihada za kumtafuta zilifanyika, simu yake ya mkononi haikuwa hewani huku ikidaiwa kwamba namba husika haitumii tena.
Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia Uwazi kwamba, kwa sasa Liyumba anaishi Kinondoni, Dar es Salaam lakini kupatikana kwenye simu ni ishu nyingine.

3 comments:

Anonymous said...

jamani huyu mama hana akili kiruuu...anaitwa fausta ngowi. alizaa na liyumba miaka 30iliyopita lakini hakuwahi kuolewa nae! huyu baba amatus kazaa na wanawake kama watano lakinu hakuwahi kumuoa yoyote! mke halalu wa huyu liyumba alikuwa chotala wa kijelumani ambaye kaisha fariki sasa! sasa huyu mchaga katokea wapi! eti mke wake! huyu mama anakaa kwenye mafleti ya ubungo miaka mingi na amedanfanya

Anonymous said...

huyu mama ni tamaa tu hizi maskini! kisa kazaa nae.. kweli mchaga ni mchaga tu , anadai mari isiyomuhusu! tena bora wamfunge kwa kyiongopea mahakama! wamwache mzee wa watu apumzike hee

Anonymous said...

huyu mama anataka tu umaarufu hana mpya. mbona kila mtu anajua kama mke halali wa liyumba kashafariki? na wala sio huyu mchaga alizaaga nae tu . ye mke wake alikuwa mixa wa kijerumani!