ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 21, 2013

MLIE TUU ! WASTARA HATAOLEWA BONGO TENA

Na Imelda Mtema
KAKA wa staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Juma Juma ameliambia Risasi Mchanganyiko kwamba dada yake hatafunga tena ndoa nyingine hapa nchini.

“Iwapo dada yangu akitaka kuolewa atafanya hivyo Uarabuni siyo hapa kabisa,” alisema kaka huyo na kudai kuwa ameshuhudia mateso mengi ya dada yake kwa wanaume wa Kitanzania.

Kaka huyo amesisitiza kwamba wanaume wasipate tabu ya kumuuliza dada yake kuhusu suala la ndoa kwani watajisumbua bure.
Juma alizungumza kwa niaba ya dada yake ambaye awali alipigiwa simu ili kuulizwa kama alikuwa na mpango wa kufunga ndoa nyingine hapa nchini.

Hata hivyo, Wastara alimwachia kaka yake huyo kujibu badala yake, ingawaje kaka huyo hakufafanua kama dada yake ameshapata mtu wa kufunga naye ndoa huko Uarabuni.

Wastara alifunga ndoa tatu na wanaume tofauti na mume wake wa mwisho alikuwa msanii wa filamu, Juma Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

Source:Global Publishers

3 comments:

Anonymous said...

Je, random sampling ya wanaume wanne inawakilisha wanaume wote wa ki-Tanzania? Ndoa zote za uarabuni ni nzuri kuliko ndoa zote za Tanzania? Tanzania hakuna ndoa hata moja nzuri ikilingalinganishwa na zile za uarabuni?

Anonymous said...

J'amani wasichana wa Kibongo kueni na muelekeo wa maisha na mambo muhimu ya kujiendelezaaa wacheniii kuongelea NDOA na WANAUME Kila wa kati
!!! Inashangaza kuwa mdada mrembo Kama huyu anajiweka kwenye magazeti na mitandao Kila Mara na anachozungumzia ni Wanaume, mapenzi na NDOA!!!!! Hata siku moja sijawahi kumsoma akizungumzia Kendall shule,kufungua biashara hata ya kuuza machenza sokoni, au kitu chochote cha kumuingizia kipato, basala yake yeye nikutuambia maisha yake na mapenzi na wanaume na Mara ya mwisho alitueleza jinsi wanaume wanavyo mgombania!!!!! Wanna wake jiwezesheni wachaneni na blah blah za wanaume!!!!! Msiwe mateka wa wanaume jamani, Dunia ya Leo ni kujiendelezaaa na kujinyanyuwaaaa! Mungu wabariki wanawake wa Tanzania!