Moto mkubwa wateketeza nyumba ya Bi Rahma Aboud mkaazi wa kiembe samaki mkunazi wa pili hapo jana.
Inadaiwa kuwa wakati moto huo ulipowaka hakukua na mtu yeyote ndani ya nyumba hio kutokana ilikuwa ni majira takriban ya saa sita mchana hivo wakaaazi wa nyumba hio walikuwa kazini.
Taarifa zilizozipatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao wamesema dada wa kazi wa nyumba hio alikuwa kaenda kusuka hivyo alikomea nyumba hio tena bila ya kuacha moto au kupika kitu ndani ya nyumba hio.
Nikiwa miongoni mwa shuhuda niliefika hapo mapema sana kwa vile nilikuwa karibu na maeneo hayo nilishuhudia wananchi waliojitolea huku wakivunja mlango wa nyumba hio kwa ajili ya kunusuru baadhi ya vitu ndani ya nyumba hio kama vile friji na vitu vyengine.
Cha kusikitisha shirika la kikosi cha zima moto kilichelewa kufika hapo sijui ni kwa sabau gani,lakini pia walifanikiwa kuuzima licha ya kuwa tayari hasara kubwa imeshatokea.
No comments:
Post a Comment