ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 28, 2013

MPAMBANO WA YANGA NA WAGOSI WA KAYA NDANI YA DIMBA LA TAIFA

Askari Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga, ambaye ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' aliyechukizwa na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, leo jioni. 


Chuji alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu kutokana na maamuzi yake ya kuwapa penati wapinzani wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa sahihi. Mwamuzi huyo Martin Saanya, alitoa penati katika dakika ya 90+ kwa kile kilichoonekana kuwa Beki wa Yanga David Luhende aliunawa mpira huo, huku mshika kibendera wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na kushindwa kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye alipuliza kipyenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki na wachezaji wa Yanga.


Katika mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu, katika dakika ya 68, kufuatia pasi nzuri iliyopigwa na David Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo kwa mkwaju huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo. 


HUKO KWINGINEKO Matokeo ya mechi za leo ni:- Rhyno 0-Azam 2, Oljoro 0- Simba 1, Tanzania Prisons 0- JKT 3, Ruvu Shooting 1- Mbeya City 2, Mgambo Shooting 1- Ashanti Utd 0, Mtibwa Sugar 1- Kagera Sugar 0
Kipa wa Coastal Union, Shaban Kado, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
Beki wa Coastal, Juma Nyoso (wa pili kushoto) akiondosha hatari, huku wachezaji wa Yanga, Hussein Javu (kushoto) na hamis Thabit, wakiwania mpira huo.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa Coastal.
Mabeki wawili wa Coastal, wakimdhibiti David Luhende.
Didier Kavumbagu, akishangilia bao lake sambamba na Simon Msuva. Katika mchezo huo mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Simon Msuva na wa Coastal.
Askari Polisi wakilinda mlango wa Chumba alichoingia Mwamuzi wa mchezo huo baada ya kuona usalama wake matatani, ambapo Chuji alijaribu kupangua ngome hiyo ili kuufikia mlango huo bila mafanikio.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu, akishangia bao lake alilofunga katika dakika ya 68, baada ya pasi nzuri kutoka kwa beki wake, David Luhende. Katika mchezo huo mwamuzi alitoa penati katika dakika 90+ ambapo mkwaju huo ulipigwa na Jarry Santo na kumchambua kipa wa Yanga Mustafa Bartez na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Mustafa Bartez, akichambuliwa na kufyngwa mkwaju huo uliopigwa na Jerry Santo, katika dakika ya 90+. MATUKIO ZAIDI YA MCHEZO HUU PAMOJA NA MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YATAKUJIA BAADAYE.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akijikunja kupiga shuti huku beki wa Coastal, Juma Nyoso, akijaribu kumdhibiti, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hivi sasa mpira ni mapumziko na matokeo bado ni 0-0.
Haruna Niyonzima, akiwatoka mabeki wa Coastal, wakati wa mchezo huo kipindi cha kwanza.



Wednesday, August 28, 2013 No comments
YANGA:- Ally Mustafa 'Bartez', Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub 'Canavaro' (c), Mbuyu Twite, Salim Telela, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Haruna Niyonzima.


BENCHI LA AKIBA:- Deogratias Munishi, Oscar Joshua, Issa Ngao, Hussein Javu, Nizar Khalfan, Said Bahanuzi na Hamis Thabit


COASTAL:- Shaban Kado, Juma Hamad, Abdi Banda, Marcus Ndehele, Jerry Santo (c), Uhuru Selemani, Chrispine Odula, Yayo Lutimba, Haruna Moshi 'Boban' na Danny Lyanga.


BENCHI LA AKIBA:- Said Lubawa, Mbwana Hamis, Abdulrahman Omari, Razak Khalfan, Yusuf Chuma, Kassim Selembe na Keneth Masumbuko.


No comments: