Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa TASWA, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Maulid Kitenge, amefiwa na baba yake mzazi, Baraka Kitenge. Msiba umetokea jana Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa MauliD ni kuwa msiba upo JET Lumo na maziko yanatarajiwa kufanyika leo Jumatano makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Kwa mawasiliano zaidi namba ya Maulid ni 0713-248740
KATIBU TASWA
No comments:
Post a Comment