Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Dkt. Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habariKwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya.
Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.
“Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo…,” alisema.
“Picha yake itasambazwa kila sehemu…sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.
Imeandaliwa na www.thehabari.com
3 comments:
Tatizo hapa sio tu hao punda bali ni hasa matajiri wenyewe wenye mizigo. Huku US serekali inatumia hao punda kukamata wenye mizigo mfano plea deal, badala ya miaka 30 jela sema kila kitu unapata miaka mitano. Badala ya watu kunyongwa huko China na nchi nyingine serekali ingeweza ku negotiate na hizi nchi kwa vifungo vingine ikiwa punda wataelezea kila kitu. Ukitaka kuondoa mti ni kwenye shina na sio unakata matawi.
Let me just start by saying Muheshimiwa Harrison Mwakyembe ni jemedari,mpambanaji, na mfanya Kazi bora sana sana sana na tena ni Mfano wa kuigwa hapa nchini na nchi zoote za Africa!!!!! Amekuwa akikemeaaaa maovu mengiiiii bila kuogopa mtu yeyoteeeeee yuleeee! Viongozi Africa wangekuwa hivyo Kama Mwakyembe Africa ingekuwa mbaali sana Hakikaaaa! Viongozi Wengi Kama mawaziri, Wabunge na hata Watu wa Wilaya na wakuu wa mikoa wamejisahau kabisaaaa! Wametusahau sisi wanna nchi na wamesahau kufanya Kazi zao!!! Tanzania inaongoza kwa Madawa ya kulevya sasa, ni aibu tupuuuuu! Tanzania inaongoza kwa mauaji na hatakumwagiana tindikali kitu ambacho kinajitokezaa all the time, it's like fashion now kumwagia mtu tindikali na tuna ona waendesha boda boda wamekuwa wakibeba bastolla na kufanya matukiooo ya mauaji kila kona!!!!!! Hizo bastolla wanazitoa waapi? Mtu unaogopa hata kwenda benki kuchukuwa pesa!!!!!! Mie naona viongozi waanze kuiga Mfano toka kwa Muheshimiwa baba Mwakyembe! Kazi Yake ni nzuuuuri sana sana sana!! Viongozi waache Kujali maslahi Yao wenyewe Bali ya wananchi woote wa Tanzania, viongozi waache uoga jamaniiiiii! Uoga ni dhambi kubwa sana! Eeeh Mungu ibaraki Tanzania na Afrika yooote.....
Baba yetu wa mbinguni jina lako baba litukuzwe! tunaomba umlinde huyu baba yetu aliyebaki wa Taifa hili Mheshimiwa Mwakyembe,maana ndiye Kiongozi tunayemwona anayefuata nyayo za Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,muepushe na mabalaa yote ambayo mafisadi na waporaji wa mali za nchi yetu watataka kumwangamiza,baba yetu wa mbinguni tuwezeshe na utupe nguvu na uwezo wa kumchagua kuwa kiongozi wa nchi yetu katika uchaguzi unaokuja wa mwaka 2015 AMINA!
Post a Comment