Unaweza kufikiri hujafikia malengo yako kwa sababu kuna vitu fulani unakosa, lakini kiukweli hakuna hata kimoja ulichokosa. Yaani kila unachohitaji ili kufikia malengo yako tayari uko nacho karibu yako, ni wewe tu kuvitumia ili kufika kule unakotaka.(soma; unacho kila unachohitaji)
Jessica Cox alizaliwa bila mikono ila ndie binadamu wa kwanza asiekuwa na mikono kuweza kuendesha ndege.
Kama angeamua kutumia hali yake ya kutokuwa na mikono kwa kujiona ana bahati mbaya leo hii tusingemjua.
Jessica anatufundisha kwamba kila mtu anaweza kufanya kile anachoamua na hakuna cha kumzuia.
Hebu chukua dakika tatu na sekunde thelathini kutazama hiyo video hapo chini ya maajabu yanayofanywa na dada huyu.
No comments:
Post a Comment