
Andrew Chenge
Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.
Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.
“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope
.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”
Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.
Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.
Kamati ya Bajeti
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.
“Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi,” alisema.
Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.
“Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo,” alisema.
Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.
Umoja wa nchi tatu
Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.
Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.
Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.
Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.
Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.
Mwananchi
5 comments:
I hope people will learn how to listen...
Tuone sasa kama wao wamejitoa mizigo ya wengine itashughulikiwa na kutolewa haraka. Shame on Tanzania!!!
I hope so too man, viongozi wetu wameshindwa kazi.
Mimi nanona hapo its more of a political issues(reasons),trust me Kenya kuna matatizo kama ya Tanzania if there is a difference kuna slight difference ,kumbukeni Kenya is the one of the top corrupt countries in the world Tanzania hata haifikii corruption ya kenya ,kwa hiyo tusikae tu kusema na kulalamika,sikatai Tanzani bandari ni wasumbufu na corrupt na wizi lakini hili suala sio the main reason za hawa jamaa..na tatizo hapo ni Uganda na Rwanda ndio wana hasira na matatizo na Tanzani na kuamua kufanya maamuzi na Kenya hapo ni beneficiary wa hilo dili so yeye anaangalia maslahi yake na ndio anayenufaika.
Kingine hiyo reli kutoka kenya mpaka Rwanda umbali wake kujengeka sio economic and strategic ukifananisha reli kutoka Bandari ya Tanga au Hata Dar ES Salaam mpaka Rwanda na kwenda uU ganda, Yaani ukiangalia umbali wa hiyo reli kutoka Mombasa mpaka Rwanda ni vichekesho sana kwa mtu anayejali muda na gharama mpaka mizigo kufika...ata the end of the day my guess and take when Mapenzi na ushirikiano wa kinafiki utakapoisha between these 3 countries watarudi tuu Tanzania na kuona jinsi gani wanaweza kuimarisha ushirikiano na kudumisha uduma za maendeleo east Africa!..because without ushirikiano wa Tanzania hamna UMOJA na AMANI YA KUDUMU ..nchi zote hizi tatu kuna ukabila sana na may be thats the only thing in common kati ya nchi hizi tatu, na bila ya wao kuimiarisha misingi na kumaliza matatizo yao ya kikabila hawataweza kuwa na urafiki na ushirikiano wa ukweli baina yao , misingi hii uanzia ndani nyumbani kwanza !!!!!!!!.
mdau.
Hapo wadau hata tanzania ingekuwa perfect vipi na customer service hawa jamaa wawili( Uganda na Rwanda) tayari walishaamua tangu zamani kufanya hivo, reli hiyo inayojengwa it doesnt make sense umbali wake almost mara mbili kutoka Tanzania, waswahili wanasema baada ya siku kwenye ukweli uongo ujitenga, ngoja siku vumbi likashatulia tutapata kuna picha halisi!, hapo kila mtu ana sababu zake na maslahi kati ya nchi hizo tatu na ndio tatizo , sidani kubwa ,sidhani kama kuna common interests hapo hiy ni hatari kubwa.
Post a Comment