ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 19, 2013

SHEIK PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO MJINI MOROGORO.


Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa  na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro..
Sheikh Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi  tarehe 28.08.2013
Ulinzi Ukiwa umeimarishwa mahakamani leo.Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG

4 comments:

Anonymous said...

MTu mmeshasema huyu Shekh Ponda sio Mtanzania halisi sasa serikali ya Tanzania inambeba wa kazi gani??? Kwa kiipi??? Na kwa nini viongozi wa Ngaazi za juu hawamkatai na kupinga sera zake chafu za uchochezi na za vurugu nchini mwetu? Au mpaka Damu na Maji vitiririkeeee?? Hiviii Serikali ya Tanzania mtaogopa kukemeaaa maovu mpaka lini jamaniiiii??? Mmefungia macho madawa ya kulevyaaaa macho mpaka wauzaji wameitia nchi Doa kubwa sana! Sasa hiviii ukionyesha passport ya Tanzania tu unaloooo utapekuliwa mpaka ukomeeee!!!!!! Viongozi Wacheni woooga jamani teteeeni Tanzania na Watanzania!

Anonymous said...

mdau wa mwanzo kama hujui jambo au mambo nikama kisa kikubwa cha usiku unadhani serikali wajinga na nani kakwambia kwamba si mtanzania huyu, mmeshazoea gudanganywa na ccm kila kukicha ndo maana.
wanajua wamembabikia kesi ya uongo ndo maana hawawezi kumuhukumu serikali ya ccm mbaya sana

na kwa nini wanafubia macho madawa ya kulevya jiulize swali hili na kujitapa na kujidai vijidume kama simba kumuonea sheikh wa watu kwa nini jiulize.

mwenye akili na kujua mambo anajua serikali ina mkono wake katika madawa ya kulevya ndo maana wamefumbia macho siku za mwizi arbaini wamebamba ndo maana

mnawakamata watu wadogo wadogo tu watu wanafisidi serikali mnawanyamazia kimya kwa sababu mnakula nao sahani mmoja

watanzani wacheni kuwa wajinga

Anonymous said...

MUNGU ATAKUSAIDIA SHEIKH PONDA NA FITNA ZAO MUNGU KISAWABAINI DAIMA MUNGU HATUKUTUPA MKONO SHIKA KAMBA YAKE BARABARA UKIWA MUUISLAMU KATIKA NCHII HII NA DUNIANI KOTE WANAWABAMBIKIA KESI MARA MAGAIDI MARA SIJUI NINI NA NINI UISLAMU HATOKUFA DAIMA MKITAKA MSITAKE HAMUWEZI KUMSHINDA MUNGU NA DINI YAKE YA KIISLAMU AMESHINDWA FIRAUNI ITAKUWA SERIKALI YA CCM

Anonymous said...

Allah yupo pamoja na wewe sheikh ponda wala usijali hii ni vita ya msalaba kwa nini madawa ya kulevya wasiwakamate kama kweli wanatenda haki serikali ya ccm