ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 19, 2013

TANGAZO LA RASIMU YA KATIBA

KAMATI YA MAPENDEKEZO YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
-KAMKATA, USA
 Kwa Wanajamii wa Jumuiya zote za Marekani na Mexico, kwa niaba ya Kamati ya KAMKATA, napenda kuwapongeza kwa kujitokeza kwenu kwa wingi katika kutoa maoni yenu ya katiba mpya. Pia napenda kuwahimiza wale ambao hawajatoa maoni yao, wajitahidi kufanya hivyo.
Ikumbukwe Katiba ni hitajio la kila Mtanzania, na katiba bora ni manufaa Zaidi kwa wale waliochini au mbali na manufaa ya taifa. Pia hili ni suala la kihistoria na nafasi ya kuingiza maono yetu katika nadharia. Unapokosa kushiriki kutoa maoni ni sawa na kujinyima haki yako ya kushiriki katikataifa bora. Katiba mpya inajengwa na watoa maoni, sio wanaoamini kuwa wengine watatoa.
Kwa wale ambao wanaoamini kuwa maoni yao hayatopewa nafasi. Ni bora uamini Mungu yupo usimkute, kuliko kuamini hayupo na ukamkuta.
Ikumbukwe; Tukio hili ni la kihistoria, na kila mmoja wetu atazingatia hima ya kuingia katika historia hii muhimu na yenye manufaa kwetu na vizazi vyetu vijavyo.
 Unaweza kutuma maoni yako kupitia tovuti ifuatayo: www.katibatanzania.org
Au kwenye barua pepe hii: mapendekezo@katiba tanzania.org
 Nawatakia kila la kheri na Imani thabit ya ujenzi wa taifa letu jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Katibu wa KAMKATA
Nassor Basalama

3 comments:

Anonymous said...

Hakuna mtu atakayetuma maoni yake kwa njia hizo, Kama mna nia ya kukusanya maoni basi tumieni njia za kueleweka ambazo ni za wazi kabisa na sio kwa ujanja ujanja ili iweje..!!!?? Msituvuruge kabisa kama hamtaki kuita watu watoe maoni yao LIVE bila chenga... Ni hayo tu halafu hii KAMKATA imefanya kikao lini cha kuweza kuchagua hawa viongozi kama sio uzushi na ujanja janja tu..!!???
Naomba uirushe na wahusika kama kweli wapo waje na majibu na wawekena picha zao tuwajue tafadhali.
Shukrani sana mkuu LUKE na kila la kheri.
-MDAU PAKA JEUSI

Anonymous said...

Hii KAMKATA iko wapi??

Mimi niko hapa Delaware lakini leo ndio naisikia, Bwana hapo juu unachisema ni kweii IFISADI na UDANGANYIFU mpaka kwa mzee OBAMA tutapona kweli???


Anonymous said...

PJ

Huna nyimbo wacha watuendeleze maendeleo ya nchi yao. Kama maisha yamekushinda ndugu tafuta ustaharabu mwingine. Tuachie sisi tunaona mambo haya kwa umbali.

Mdau