ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 8, 2013

HARUSI YA YA LUTHER NA ESIDAY, GIUTHERSBURG, MARYLAND

Padri akifungisha ndoa ya Luther Guy Ligate na Esiday Boaz Mollel iliyofanyika Jumamosi Sept 7, 2013 Kentlands Mansion, iliyopo barabara ya 320 Kent Square, Gaithersburg, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wazazi wote wa bwana na bi harusi waliokuja kutoka Tanzania.
Juu na chini ni Bwana na Bi harusi wakiingia ukumbini kwa mara ya kwanza kama Mr & Mrs Ligate
Bwana na Bi harusi wakisindikizwa na wapambe wao walipokua wakiingia ukumbini  huku ndugu, jamaa na marafiki wakishuhudia .
Bwana na Bi Harusi wakiwa kwenye meza yao huku Bi harusi akiongea jambo na mpambe wake.
Brigedia Jenerali mstaafu wa Jeshi la Tanzania JWTZ, Ligate akiwahusia Bwana na Bi harusi, kulia na Mrs Ligate ambao wamekuja maalum kwenye harusi hiyo.
Mrs Ligate akielezea maana ya zawadi walizowaletea maharusi toka Tanzania kabla hawajawakabidhi.
Mama mzaa chema akiwakabidhi maharusi moja ya zawadi alizokuja nazo toka Tanzania. 
Familia ya Bi Harusi ikiongozwa na Mr. Mollel nao wakiongea machache kwa maharusi na baadae kuwakabidhi zawadi walizokuja nazo toka Tanzania.
Maharusi wakisaidiwa na wapambe wao kukata keki.
Esiday akimlisha keki baba mwenye nyumba wake ambaye kuanzia jana amekula kiapo cha kuwa mdhamini wa pendo lake kwa shida na raha mpaka hapo mwenyezi Mungu atakapo watenganisha.
Luther akimlisha keki mama mwenye nyumba wake  ambae nae kuanzia jana amekula kiapo cha kuwa mdhamini wa pendo lake kwa shida na raha mpaka hapo mwenyezi Mungu atakapo watenganisha.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Bwana na Bi harusi wakichum baada ya kulishana keki
Kutoka kushoto ni Obed Ligate, Luther Guy Ligate, Vupe Ligate na Phanule Ligate
kutoka kushoto ni Obed Ligate, Esiday Mollel (mke wa Guy), Luther Guy Ligate, Vupe (dada yao Obed, Phanuel na Guy), Phanuel Ligate na Mercy Mfanga (Mke wa Phanuel) katika picha ya pamoja.
Maharusi katika picha ya pamoja na Bwana na Bibi Maganga.

1 comment:

Anonymous said...

Diva ndani ya mjengo