Mazoea ya matumizi ya lugha huchangia katika mabadiliko ya kaida za lugha – ziwe ni za kifonolojia au kisarufi maumbo na miundo.
Kwa mfano, siku hizi ni kawaida kuwasikia vijana wakisema ‘mdada’ na ‘wadada’ badala ya umbo lililotawala siku za huko nyuma ambalo ni ‘dada’ (iwe ni umoja au wingi). Pia masikio yetu yameanza kuzoea kusikia ‘mwendo wa lisaa limoja au masaa matatu’ badala ya ‘mwendo wa saa moja au saa tatu.’ Utwasikia wahifadhina wa lugha ya Kiswahili wakilalamikia matumizi haya ya kisasa kwamba ni ukengeushaji wa kaida za Kiswahili. Lakini ukichunguza kwa makini utaona kwamba kuna mantiki ambayo inapelekea matumizi mapya kuwa na mashiko kwamba mdada/wadada inalipa umbo sifa za ngeli ya ubinadamu katika umoja na wingi wake kama ilivyo katika maumbo kama vile mtu/watu, msichana/wasichana, mvulana/wavulana, nk. Kwa hivyo lugha huwa ni mazoea ya matumizi yanayoongozwa na kaida ambayo hatimaye huonekana kama kaida, na hivyo kaida hutokea zikabadilika kutokana kuibuka kwa mazoea mapya.
No comments:
Post a Comment