Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishepu Ndugu Isabela Chilumba wakati wa mapokezi yake katika kata ya Isaka.
Wakazi wa Isaka wakiwasikiliza viongozi wa CCM Taifa waliowasili mkoani Shinyanga leo kwa ziara ya siku nne.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye akiwa na mbunge wa Msalala Ezekiel Maige wakishiriki kucheza ngoma ya wakazi wa Isaka kabla ya kuhutubia kwenye mkutano wa Hadhara.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Isaka na kuwaambia muda wa kudanganyika na wanasiasa uchwara umefikia kikomo.
Mwanachama wa CCM akifurahia hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Isaka.
Mbunge wa Msalala Ndugu Ezekiel Maige akizungumza na wakazi wa Isaka wakati wa mkutano wa hadhara .
KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI SHINYANGA NA KUANZA RASMI ZIARA YAKE
Wana CCM wa Isaka wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Hamisi Mgeja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Isaka .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Kagongwa kata ya Kagongwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mwendakulima baada ya kuzindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa kituo cha afya kilichodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Africa Barrick Gold.
kwa picha zaidi bofya read more
Katibu Mkuu akishiriki kupanda mti katika kituo cha afya kilichodhaminiwa na mgodi wa Buzwagi chini ya kampuni ya Africa Barrick Gold .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimwagia maji mti alioupanda kwenye kituo cha afya katika kijiji cha Mwendakulima.
Katibu Mkuu wa CCM akishiriki kupiga lipu ofisi ya kata ya Majengo katika wilaya ya Kahama.
Katibu Mkuu wa CCM akifungua SACCOS ya Mkombozi ya vijana wa CCm mjini Kahama ambapo aliwezesha kutatua masuala yote ya msingi yanayowakabili vijana hapo, hasa yanayohusu elimu ya uraia , uchumi ,elimu za ufundi ambapo vijana kumi watapata nafasi ya kulipiwa na Katibu Mkuu na masuala ya maeneo ya kufanya shughuli za biashara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdul Rahman Kinana akiingia ukumbini kwa ajili ya kufanya mkutano na mabalozi wa nyumba kumi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Kahama.
Katibu wa NEC Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa CDT tayari kwa kuhutubia mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye kiwanja cha CDT kwa ajili ya kutubia wakazi wa Kahama.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akiwapongeza wacheza sarakasi waliokuja kumsabahi kwa staili ya kipekee kabisa.
Sehemu ya Umati uliofurika kusikiliza hotuba za viongozi mahiri wa CCM, Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye leo kwenye viwanja vya CDT mjini Kahama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kahama wakati mkutano wa hadhara uliofanika leo mjini Kahama.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi kutoka vyama vya upinzani baada ya wananchi wengi kuridhika na hotuba yake nzuri, katika mkutano huo zaidi ya wanachama 560 wamejiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu mara baada ya kuwasili katika mji wa Isaka Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga leo asubuhi tayari kuanza ziara yake ya siku nne mkoani humo katika kuimarisha chama na Kuhamasishwa wananchi katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-ISAKA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Khamis Mgeja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kupokelewa katika mji mdogo wa Isaka
hViongozi mbalimbali wa Chama wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana Akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama wakati alipowasili katika mji wa Isaka Wilayani Kahama leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Khadija Kusaga aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Ezekiel Maige mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kipaza sauti Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakati wakiongea na wananchi katika mji wa Isaka, katikati ni Khameja Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo.
Khameja Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akizungumza na wananchi wakati wa mapokezi hayo kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye .
Waananchi wakinyanyua mikono juu wakishangilia wakati Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye hayupo pichani akiongea.





















No comments:
Post a Comment